Tafuta

Vatican News
Marehemu Kardinali  Godfried Danneels Marehemu Kardinali Godfried Danneels 

Papa:Salam za Rambi rambi kwa kifo cha Kard Danneels

Tarehe 14 Machi 2019 ameaga dunia Kardinali Godfried Danneels Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Malines-Bruxelles akiwa na umri wa miaka 85.Ni uchungu wa Baba Mtakatifu Francisko na maaskofu wa Ubelgiji. Kwa kifo chake,Baraza la makardinali kwa sasa wanabaki 222, kati yao 122 wanaweza kupigiwa kura,wakati 100 hawawezi kuchaguliwa

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kardinali Godfried Danneels Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Malines-Bruxelles aliye kuwa na   umri wa miaka 85 amefariki dunia asubuhi ya Alhamisi, tarehe 14 Machi 2019 akiwa katika nyumba yake jimbo Kuu Malines. Mazishi yatafanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Rombaut huko Malines, tarehe 22 Machi 2019. Aliyetoa taarifa hizo ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Malines-Bruxelles na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Ubelgiji, Kardinali Jozef De Kesel, na ambaye ataongoza maadhimisho pamoja na Balozi wa Vatican nchini humo, Maaskofu, mapadre na mashemas wa Jimbo Kuu.

Telegram ya salam za rambi rambi kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko

Kufuatia na kifo hicho Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kupitia telegram yake, kwa Askofu Mkuu wa Jimbo, akionesha masikitiko ya kupoteza mtumishi wa Mungu. Baba Mtakatifu anasema, “baada ya kupata habari kwa mshituko wa kifo cha Kardinali Godfried Danneels, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Malines-Bruxelles, ninatoa salama zangu za rambi rambi kwako, familia, maaskofu, makleri, watawa  na waamini wanao omboleza kwa kumpoteza Kardinali.

Aidha anaongeza kusema ni “Mtumishi wa Mungu aliyehudumia Kanisa, si tu katika jimbo lake, lakini pia kwa ngazi ya kitaifa kama Rais wa Baraza la Maaskofu wa Ubelgiji, pamoja na kuwa mjumbe wa Mabaraza kadhaa ya kipapa Roma. Alikuwa makini katika changamoto za Kanisa la sas;Kardinali Danneels alishiriki kwa uhai wake hasa katika baadhi ya Sinodi za Maaskofu, ikiwemo hata ya mwaka 2014-2015, juu ya familia. Na sasa ameitwa na Mungu katika kipindi hiki cha utakaso na safari kuelekea katika ufufuko wa Bwana”. Ninaomba kwa Kristo mshindi wa ubaya na kifo ampokee katika amani yake na furaha yake”; kwa ishara ya kutia nguvu, ninawatumia Baraka maalum ya kitume ninyi nyote, ndugu wa marehemu Kardinali, wachungaji, waamini na wote ambao watashiriki maadhimisho ya mazishi.

Katika taarifa kutoka kwa maaskofu wa Ubelgiji kuhusu maisha yake

Katika taarifa kutoka kwa maaskofu wa Ubelgiji kuhusu maisha yake, marehemu Kardinali Godfried Danneels, alizaliwa  tarehe 4 Juni 1933 huko  Kanegem, (Fiandre Magharibi). Majiundo ya ukasisi katika Seminari ya Bruges na baadaye kuendelea na mafunzo ya falsafa katika Chuo Kikuu katoliki cha Lovanio. Baada ya shahada aliendelea katika chuo cha Kipapa cha Gregoriana, Roma katika masomo ya taalimungu  (1954-1959).

Alipata daraja la upadre kunako mwaka 1957 katika parokia ya Kanegem, baada ya miaka miwili akapewa shughuli ya kuwa mwalimu wa  kiroho, profesa wa taalimungu ya sakramenti na liturujia katika seminari kuu ya  Bruges. Mwaka 1961 aliendelea na uzamivu wa udaktari wa Taalimungu katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana Roma. Tangu mwaka 1969, alinedelezad kufundisha kozi katika Seminari Kuu ya Bruges, alifundisha pia katika Kitivo cha Taalimungu cha Lovanio. Na Mtakatifu Paulo VI alimteua kuwa askofu wa Anversa kunako tarehe 16 Novemba 1977.

Kuwa Askofu Mkuu tarehe 21 Desemba 1979

Alikuwa ni Mtakatifu Yohane Paulo II aliyemteua Askofu  Godfried Danneels kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la  Malines-Bruxelles tarehe  21 Desemba 1979. Alichagua ngao: “Apparuit humanitas Dei nostri”,  kutoka katika Barua ya Mtakatifu Paulo kwa Tito. Tarehe 2 Februari  1983  akateuliwa kuwa Kardinali na kupewa Kanisa Kuu la Mtakatifu Anastasia.  Aliudhuria uchaguzi wa mwezi Aprili 2005 alipochanguliwa Baba Mtakatufu Benedikto XVI na ule wa  tarehe 13 Machi 2013 alipochanguliwa Baba Mtakatifu Francisko. Kwa kufuata sheria ya Kanisa, Kardinali Daneels aliwakilisha barua ya kung’atuka uaskofu  Mkuu wa Jimbo Kuu la Malines-Bruxelles kwa Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI, tarehe 4 Juni 2008 akiwa na umri wa miaka 75 lakini karidhiwa maombi yake tu  tarehe 27 Februari 2010 na kuanza maisha yake ya ndani katika Jimbo Kuu.

15 March 2019, 10:00