Tafuta

Vatican News
Papa kuitembelea manispaa ya Roma Papa kuitembelea manispaa ya Roma   (ANSA)

Papa:Ukuu wa Roma na historia yake iweze kukabili changamoto ya kukaribisha!

Historia ya milenia ya Jiji la mielele ni kitabu kikubwa sana katika tunu za kitasaufi,kihistoria,kisanaa na kikatiba;mazungumzo na heshima ya pamoja,utawala wa sasa na ule wa kiroho;masuala ya makaribisho na huduma kwa ajili walioachwa pembezoni ni mambo yaliyomo katika hotuba ya Papa kwa viongozi wa Manispaa ya Roma,26 Machi 2019

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 26 Machi 2019 Baba Mtakatifu Francisko ametembelea Ofisi tawala ya Manispaa ya jiji la Roma kwa mwaliko wa Meya wa mji Bi Virginia Raggi , wakati wa hotuba yake anashukuru kwa mwaliko wa Meya na salam zake alizomwelekeza wakati wa hotuba yake. Kwa viongozi wote tawala na Baraza kuu la manispaa na wawakilishi wa selikali na pia wazalendo wa Roma amewasalimia. Baba Mtakatifu ameonesha shauku yake aliyokuwa nayo kwa siku nyingi kwenda kutembelea ofisi hiyo tawala ili kuwashukuru kwa ushirikiano ambao waliuonesha ikiwa  viongozi wa nchi na ule wa Vatican wakati wa Jubilei maalum ya Huruma, kama ilivyo hata maadhimisho ya matukio mengine ya Kanisa. Mambo hayo yote yanawezekana kufanikiwa kutokana na utayari wa kushirikiana nna shughuli yenye kiwango inayojionesha katika  utawala wa jiji hilo,ushuhuda wa historia ya milenia ambayo kwa kupolewa na Ukristo imekuwa kwa karne nyingi kama  kitovu cha Ukatoliki.

Roma ni baba asili wa kuzaa sheria inayosimamia hekima; watakatifu na wafia dini

Roma ni baba asili wa kuzaa sheria, inayosimamia hekima ya utendaji wa watu wake na kwa njia hiyo imeaangaza dunia na msingi yake na taasisi zake. Ni mji ambao ulitambua thamani na uzuri wa falsafa, wa sanaa na kuunda utumaduni ulitokana na  Ellade, yaani mji wa kizamani ambao wakazi wake waliishi zaidi ya karne ya sita a.C na ilikuwa inapanuka hadi kufika ugiriki. Na walikaribishana na kushirikishana hadi kupata ustaarabu wa kujulikana wagiriki-warumi. Na wakati huo huo Baba Mtakatifu Francisko anathibitisha  kuwa haiwezekani kutoona ugumu ambao katika mji wa Roma  taarifa zinaonesha wafiadini kwa ajili ya  utume wao wa kimisionari, kama vile watakatifu Petro na Paulona katika damu yao, inayounganishwa  na mashuhuda wengi kwa pamoja kuliundwa mbegu mpya ya kizazi cha kikristo. Hawa walichangia kutoa sura mpya katika dunia licha ya matendo ya kuishi ya kihistoria na matukio yao ya mwanga na vivuli, bado leo hii vinaangaza kwa  utajiri wa minara, ya  kazi za sanaa, makanisa na majumba makuu, vyote vikiwa vimepangiliwa kwa namna isiyoweza kuigwa katika vilima saba, ambapo kimojawapo cha kwanza ni mahali alipokuwa yaani Campidoglio.

Roma imetambua historia ya kupokea watu wote kutoka mataifa mbalimbali

Kwa kipindi kirefu karibu mika 2,800 ya historia, Roma imetambua kupokea na kushirikisha tofauti za watu, kutoka kila pande ya dunia, ambao wanatokana na kila aina ya kijamii na kiuchumi bila kuondoa utofauti za sheria, bila kuwanyenyekeza au kukandamiza kila tabia zao na utambulisho. Badala yake kwa kila mmoja imekuwa ni ardhi yenye rutuba, inayofaa kutoa ubora wa kila mmoja na kuupa muundo wa pamoja wa mazungumo na utambulisho mpya. Baba Mtakatifu anaedelea, mji huu umepokea wanafunzi na mahujaji, watalii, wakimbizi na wahamiaji kutoka kila kanda ya Italia na nchi nyingi duniani. Umekuwa mji wa kuvutia na ni  kama zip. Zip kati ya bara la Kaskazini na dunia ya mediterranea, kati ya ustaarabu wa kilatino na kijerumani,kati ya mamlaka na mali zilizohifadhiwa kwa nguvu za kiraia na nguvu za kiroho. Inawezekana kabisa kuthibitisha kwamba ni kwa neema ya nguvu ya maneno ya kiinjili, imewezesha kutoa neema katika kuheshimiana na kushirikiana kwa ajili ya wema wa watu, kati ya mamlaka ya umma na ile ya kidini, ambayo kwa wema inaunda hadhi ya mtu, mwanadamu na kutoa nafasi ya uhuru na ushiriki.

Roma ni kituo cha ukatoliki

Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake anasema, Roma kwa maana nyingine  imekuwa ni sehemu ya kufikia na ishara kwa ajili ya wale ambao wanatambua kama mji mkuu wa Italia na kituo cha Ukatoliki , wamejikita katika njia ili kuweza kuona  mshangao wa minara na njia za wakati uliopita, kwa ajili ya kutoa ibada ya kumbukumbu ya wafiadini, kwa ajili ya kuandhimisha sikukuu msingi za mwaka wa  kiliturujia na hija za jubilei kubwa, lakini pia hata kutoa huduma yao katika Taasisi  ya Taifa la Italia na Vatican. Kwa maana nyingine Roma inalazimika kuwa na nguvu ya kipindi cha sasa na ile ya kiroho na kuzungumza daima, kushirikiana kwa dhati kwa pamoja na kwa heshima; inataka kuwa na wabunifu, kuwa  na wafanyakazi wa kila siku wenye kuwa na  mahusiano mema, kama vile kukabiliana na matatizo mengi, ambayo katika uendeshaji wa urithi huu kubwa unaojikita ndani mwake!

Mji wa milele ni kama kitabu cha kuandikia tunu za kitasaufi,kihistoria na kisanaa

Mji wa milele ni kama kitabu cha kuandika thamani za kitasaufi, kihistoria, kisanaa na katiba, wakati huo huo ni mahali pa kuishi karibu milioni tatu za watu ambao wanafanya kazi, wanasoma, wanasali, wanakutana na kupeleka mbele historia yao binafsi na familia na ambayo kwa upamoja japokuwa na ugumu wa kila uendeshaji , na kwa kila mmoja kadiri anavyojitahidi  kwa ajili ya wema wa mji.  Roma ni kiungo ambacho kinahitaji kutunzwa kwa unyenyekevu bila kusita, na kwa ujasiri wa ubunifu ili kuweza kuutanza mji vema, uonekane na  ili wanga wake usipotee  bali ukusanye sifa zilizopita na ambazo zinaweza kuwa mchango mkubwa kwa kizazi kipya, na endelevu  katika akili yao petevu , shauku za matarajio mema ya mipango yao.

Aidha Baba Mtakatifi akitazama ofisi ya Manispaa ( Campidoglio)  pamoja na Paa la Michalangelo na Kolosseo, unaweza kuona kuwa  kweli kuna maana ya alama na ufupisho wake. Kwa hakika ukuu wa sehemu hizi zote, Roma wanasema ina uwezo wa kutunza wito wa dunia, kuwa wabebeji wa utume na mawazo yanayostahili kupanda milima na bahari na kusimulia historia kwa wote, wa karibu na mbali na kila aina ya watu , lugha, kila rangi au ngozi. Roma inapaswa itunzwe ukuu wa zoezi lake na historia yake, iweze kuelendelea leo hii na  kuwa taa ya uzalendo na mwalimu wa kupokea. Mji usipoteza hekima yenye uwezo  wa kujionesha katika kufungamanisha, kuhisi kila mmoja anashiriki kwa dhati hatima ya pamoja. Kanisa ambao la Roma linataka kusaidia waroma wapate maana ya ushiriki katika jumuiya na kwa neema ya mitandao yake ya kama parokia, shule na taasisi za upendo, kama vile mapana ya jitihada za watu wa kujitolea, wanaoshirikiana na vyombo vya umma na raia wote  ili kuweza kutunza mji huu upate sura hai, hisia zake za upeo wa kikristo na maana ya uzalendo kamili.

Roma inapaswa kufanyiwa kazi,kuwa na hekima na ukarimu wa kushirikiana na wote

Roma inastahili kufanyiwa kazi,kuwa na  hekima, kuwa na ukarimu wa kushirikiana na wote;inastahili sana kazi wazalendo na nguvu za kijami na taasisi za umma. Kanisa Katoliki na jumuiya nyingine za Kanisa na wote ambao wanajikita katika shughuli za wema wa mji, watu ambao wanaishi humo na  zaidi kwa  wale ambao kwa sababu nyingine wanajikuta wako pembezoni, wamebaguliwa na kusahauliwa au wanafanya uzoefu wa mateso ya magonjwa, wako peke yao na wapweke. Imepata miaka 45 tangu ufanyike mkutano uliopewa jina “uwajibikaji wa wakristo mbele ya matarajio ya upendo na haki katika majimbo ya Roma”, kwa zaidi ilijulikana kuwa ni mkutano juu ya mabaya ya Roma. Mkutano huo ulijikita kutafsiri matendo ya dhati na kutoa maelekezo yaliyotolewa na Mtaguso wa II wa Vatican na kuruhusu kukabiliana kwa kiasi kikubwa cha utambuzi wa hali halisi za maneneo ya pembezoni, mahali ambapo walikuwa wanafika wahamiaji kutoka katika sehemu mbalimbali za Italia. Leo hii katika meneo hayo na mengini, Baba Mtakatifu anathibtisha inaonesha wazi wanafika idadi kubwa ya wahamiaji na wakimbizi wanaokimbia vita na majanga mbalimbali ya maisha ili kutafuta kujenga hali yao, yenye kuwa na usalama na maisha ya hadhi.

Roma ni mji mkuu ambao unaalikwa kukabiliana na changamoto ya sasa

Roma ni mji mkuu ambao unaalikwa kukabiliana na changamoto ya sasa katika historia yake kuu; kufanya kazi na nguvu yake za kupokea na kushikirisha, ili kuweza kubadili mivutano na matatizo katika fursa ya kukutana na kukua. Roma iliyo jengwa juu damu ya wafiadini, itambue kuvutia utumaduni wake,isambaze imani katika Kristo, rasilimali zake za ubunifu na upendo ambao ni muhimu katika kushinda hofu yenye hatari ya kuzuia mipango mingi inayoanzishwa. Kwa kufanya hivyo inaweze kufanya  mji uchanue , udugu na kuunda fursa ya maendeleo na zaidi  kiraia na utamaduni kama vile uchumi na kijamii. Baba Mtakatifu anawaomba wasiogope wema na upendo! Kwa maana hizo ni shughuli zinazozalisha jamii ya amani, yenye uwezo wa kupongeza zaidi nguvu na kukabiliana na matatizo kwa dhati, bila kuwa na wasi wasi, kwa hadhi kubwa na heshima ya kila mmoja na kujifungulia katika fursa mpya za maendeleo

Vatican inatamani kushirikiana zaidi kwa ajili ya wema wa wote

Vatican inatamani kushirikiana daima zaidi kwa ajili ya wema wa mji, kwa huduma ya wote hasa kwa ajili ya masikini na wale wasio kuwa na fursa, kwa ajili ya utamaduni wa makutano, kwa ajili ya ekolojia fungamani. Vatican inawatia moyo taasisi na majengo yote ya kutoa huduma kama vile watu na jumuiya zinazohusika, ili kujikita kwa uhai wote kushuhudia kwa dhati na kuangaza imani kwa kile kinachofanyika, na ubunifu kwa ajili ya huduma ya wote. Baba Mtakatifu anawatakia ufanisi mwema ili wote wahisi kushiriki na kufika lengo hili na kuthibitisha, kuwa na uwezo mawazo na nguvu ya ushuhuda wa kila siku katika utamaduni wa Roma na utume wake,kwa maana hiyo waweze kukuza na kuzaliwa kwa upya kimaadili na tasaufi wa mji. Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha akiwakabidhi kwa ulinzi wa Mama Maria Afya ya Waroma na Watakatifu wasimamizi Petro na Paulo kwa kila mmoja, kazi yao mapendekezo yao mema yanayowaongoza. Wanaweza kuwa na maelewano katika kutoa huduma katika mji huo unaopendwa sana, mahali ambapo Bwana alimwita yeye aje kutumikia kama Askofu.

26 March 2019, 14:10