Tafuta

Sala ya Malaika wa Bwana Sala ya Malaika wa Bwana  

Papa:Mungu ni mvumilivu,anasubiri uongofu wetu!

Sisi sote tunahitaji uongofu,kupiga hatua mbele na wakati huo kuna uvumilivu wa Mungu na huruma yake,vinatusindikiza kwa ajili hiyo.Japokuwa na utasa ambao mara nyingi unazunguka katika kuishi kwetu,Mungu ni mvumilivu na anatoa fursa nyingine tena ili kuweza kubadilika na kufanya maendeleo katika njia ya wema

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Dominika ya tatu ya Kwaresima (Lk 13,1-9) inazungumzia juu ya huruma ya Mungu na uongofu wetu. Yesu anasimulia juu ya mti usio zaa matunda. Mtu mmoja alikuwa na mti umepandwa katika shamba lake la mizabibu; na kwa matumaini makubwa kila kiangazi alikwenda kutafuta matunda lakini hakupata hata moja kwa sababu mti ulikuwa tasa. Kwa msukumo wa hasira baada ya kwenda karibia mara tatu, alifikiria kuukata mti huo ili aweze kupanda mwingine. Kwa hiyo alimwita na kumwambia mtunza shamba la mizabibu hali halisi ya kutoridhika kwake na kumweleza juu ya uamuzi wake wa kuukata mti huo unapoteza nafasi tu bila kuzaa matunda. Lakini mtunza shamba akajibu na kumwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate. Hii ndiyo simulizi ya neno, je inawakilisha nini? Je watu hawa katika simulizi wanawakilisha nini ? Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko Dominika ya Tatu ya Kwaresima, tarehe 25 Machi 2019 kabla ya sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na wahujaji wote, walio kusanyika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican ili kusikiliza takari yake.

Bwana anao uvumilivu kwa watu wake wasiokuwa na uwezo wa kutazama hali halisi ya umasikini

Akiendelea na ufufanuzi, Baba Mtakatifu Fracisko anasema, Bwana wa shamba hili anawakilisha Mungu Baba, na mtunza shamba ni picha ya Yesu, wakati huo huo, mti ni shara ya binadamu mwenye utofauti na aliyenyauka. Yesu anamwomba Baba kwa ajili ya binadamu, na daima nafanya hivyo, anamwomba ili  aweze kusubiri na kuruhusu  kipindi kingine, kwa sababu  mti huo uweze kutoa vichupukiza vya kutoa  matunda ya upendo na haki. Mti unaoshughulikiwa na mtunza shamba huyo katika neno hili, unawakilisha uwepo wa utasa, yaani wa kutokuwa na uwezo wa kutoa na  kutokuwa na uwezo wa kutenda yaliyo mema. Ni ishara ya yule anayetaka kuishi binfsi, aliyetosheka, kuwa na utulivu wakati analalia mali zeke; hasiye kuwa na uwezo wa mtazamo kwa moyo zaidi kwa wale walio yake, lakini katika hali ya mateso, umaskini na mahangaiko. Tabia ya ubinafsi na utasa wa kiroho, ni kunyume na upendo mkuu wa mtunza shamba mbele ya mti ule. Yeye anataka Bwana asubiri, awe na uvumilivu na anatambua kusubiri, anatumia muda wake wote na kazi yake yote. Anatoa ahadi kwa Bwana ya kwamba ataweza kuutunza mti huo usio kuwa na furaha.

Japokuwa na utasa Mungu ana uvumilivu na kutoa uwezekano mwingine

Baba Mtakatifu Francisko anasema, ulinganifu huo wa mtunza shamba la mizabibu, ni maonesho ya huruma ya Mungu, ambaye anatoa fursa ya muda kwa ajili ya uongofu. Sisi sote tunahitaji uongofu, kupiga hatua mbele na uvumilivu wa Mungu na huruma yake, inatusindikiza kwa ajili hiyo.Sisi sote tunahitaji uongofu,kupiga hatua mbele na wakati huo kuna uvumilivu wa Mungu na huruma yake,vinatusindikiza kwa ajili hiyo. Japokuwa na utasa ambao mara nyingi unazunguka katika kuishi kwetu,Mungu ni mvumilivu na anatoa fursa nyingine tena ili kuweza kubadilika na kufanya maendeleo katika njia ya wema. Lakini, maombi yaliyo ridhiwa ni kwamba, hatimaye mti huo uweze kutoa matunda na hivyo ni kuonesha dharura ya uongofu. Mtunza shamba anamwambia Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate. Uwezekano wa uongofu hauna kizingiti; kwa maana hiyo ni lazima kuupokea kwa haraka; la sivyo ungeweza kupoteza daima. Na sisi tunaweza kufikiria kuwa ni jambo gani ninapaswa kufanya kwa ajili ya kukaribia Bwana katika kipindi cha  Kwaresima na kuongoka, hasa kwa kukata mambo yale ambayo hayatakiwi?

Baba Mtakatifu anatoa mfano au ndiyo unasema: Hapana hapana mimi nitasubiri kwaresima ijayo… je unajua kuwa utakuwa hai kwaresima ijayo? Ni swali na jibu Baba Mtakatifu anauliza na kujibu. Tufikiri leo hii, kila mmoja anashuri Baba Mtakatifu kwamba, ni jambo gani la kufanya mbele ya huruma ya Mungu ambaye ananisubiri na ambaye daima anasamehe? Je ni kitu gani nifanye? Sisi tunaweza kufanya makubwa ya kujiaminisha katika huruma ya Mungu, lakini bila kuutumia. Hatupaswi kutafuta sababu hasa za uvivu kiroho, bali kukuza jitihada zetu za kujibu kwa utayari wa huruma hii katika roho ya kweli.

Katika kipindi cha kwaresima ni mwaliko wa uongofu

Kwa kuhitimisha tafakari yake, Baba Mtakatifu Francisko anasema, katika kipindi cha Kwaresima, Bwana anatualika katikauongofu. Kila mmoja lazima ahisi mwaliko huu, akosoe kile chochote katika maisha yake  kwa namna ya kufukiria, kutenda na kuishi uhusiano wake na jirani. Na wakati huo huo, lazima kuiga uvumilivu wa Mungu ambaye kwa imani ana  uwezo wa kutusimamisha sisi sote na kuanza kwa upya safari. Mungu ni Baba na hazimi cheche dhaifu, bali anasindikiza na kutunza aliye mdhaifu ili aweze kusimama na  kutoa mchango wa upendo katika jumuiya. Bikira Maria aweze kutusaidia tuishi siku hizi za kujandalia na Pasaka kama kipindi cha kujipyaisha kiroho na imani ya kujifungulia neema ya Mungu na huruma yake.

24 March 2019, 14:50