Tafuta

Vatican News
Ziara ya Baba Mtakatifu katika Manispaa ya Roma Ziara ya Baba Mtakatifu katika Manispaa ya Roma  (ANSA)

Papa:Kanisa la Roma linatunza upendo!

Manispaa ya Roma imempokea Baba Mtakatifu Francisko tarehe 26 Machi 2019 akiwa ni Papa wa nne kupanda kilima hicho kwa mwaliko rasmi wa Meya wa jiji la Roma

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu akiwa katika Manispaa ya Roma tarehe 26 Machi 2019 ameweza kuwasalimia watu waliowakilishwa mji wa Roma. Katika hotuba yake anasema kama Askofu, wa Roma mara nyingi anakutana nao katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Mtakatifu Yohane, au katika Parokia.., lakini leo hii amekuwa na fursa ya kuwasalimia akiwa katika kilima cha manispaa hiyo ambayo ni mwoyo wa mji, unaotoa maisha ya mamlaka tawala na raia wake. Anawashukuru kwa uwepo wao na upendo mkuu wanao uonesha kwa mfuasi wa Mtakatifu Petro.

Kanisa la Roma linatunza upendo

Kanisa na mbalo kama Roma Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa linatunza upend, kwa mujibu wa msemo wa Mtakatifu Ignazio wa Antiokia,(rej. barua kwa waroma, Proemio). Na zaidi anaongeza kusema, ni zoezi la Askofu wake, papa, lakini pia kwa wakristo wote wa Roma kufanya kazi kwa dhati ili kuweza kutunza uso wa Kanisa hilo  liweze kuwa na  mwanga daima unaoangaza mwanga wa Kristo anayepyaisha mioyo. Vilevile  Baba Mtakatrifu amethibitisha kwamba, katika moyo wa Papa, ipo hata nafasi ya wale wasio shirikishana imani; na kwa wote lakini yuko karibu nao kiroho na kuwatia moyo kila siku ili waweze kuwa wajenzi wa udugu na kimshikamano.  Na ndiyo zoezi la mzalendo, yaani la kuwa mjenzi wa udugu na mshikamano amesisitiza tena.

Hata wazalendo wa Roma wanahangaikia ustawi na elimu kwa watoto wao

Akiendelea na hotuba yake Baba Mtakatifu Francisko amesema kama ilivyo kwa watu wote duniani, hata wazalendo wa Roma wanahangaikia ustawi wao  na elimu kwa ajili ya watoto wao, pia Sayari iliyo bora iko rohoni mwao, yaani ule mtindo wa dunia ambao utaachwa kwa ajili ya kizazi kijacho. Lakini leo hii na kila siku, Baba Mtakatifu ameowaomba kila mmoja wao kwa kadiri ya uwezo wake, washirikiane na wakae karibu na wengine na kuheshimiana. Kwa kufanya hivyo watavalia njuga zile thamani nzuri zaidi za mji huo, kama jumuiya iliyoungana na ambayo inaishi kwa maelewano na ambayo si tu kwa ajili haki, lakini pia katika roho ya haki.  Amehitimisha kwa kuwashukuru uwepo wao katika mkutano huo na kuwaombea ili Mungu awakirimie neema na baraka zake na zaidi wasisahau kusali kwa ajili yake!

26 March 2019, 14:00