Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko ametoa shukrani baada ya  mafungo ya kiroho huko Ariccia kwa Abate Bernardo Francesco Maria Gianni Baba Mtakatifu Francisko ametoa shukrani baada ya mafungo ya kiroho huko Ariccia kwa Abate Bernardo Francesco Maria Gianni 

Papa Francisko:Kumbu kumbu,matumaini na uvumilivu ni njia ya wakati endelevu!

Mara baada ya mafungo ya kiroho huko Ariccia nje ya mji wa Roma Baba Mtakatifu Francisko kwa niaba yake na wote ametoa shukrani kwa Abate Maria Gianni kutokana na kuwasindikiza sekretarieti kuu Vatican kutambua kwamba Mungu yupo na anajionesha kwa kila binadamu,hivyo kumbu kumbu,matumaini na uvumilivu ni njia ya wakati endelevu!

Na Sr Angela Rwezaula - Vatican

Mara baada ya mafungo ya Baba Mtakatifu Francisko na waandamizi wake wa karibu katika nyumba ya mafungo huko Ariccia nje ya mji wa Roma, Ijumaa asubuhi tarehe  15 Machi 2019, Baba Mtakatifu Francisko amemshukuru Abate Bernardo Francisko Maria Gianni kwa msaada wake katika siku hizi zote za mafungo. Anaelezea alivyo shangazwa na kazi yake  hasa ya kuwafanya waweze kuingia kama vile Neno lilivyfanyika mwili katika ubinadamu; kuwafanya waelewe Mungu ambaye daima yupo kwa  binadamu. “Alifanya hivyo kwa mara ya kwanza, Neno lilipofanyika Mwili, lakini Yeye yupo hata katika ishala ambazo anamwachia binadamu. Anafanana tangu Neno kufanyika mwili, hasiye gawanyika au kuchanganyikana,yeye yupo hapo, anathibitisha Baba Mtakatifu na kuongeza kusema “ Shughuli yetu labda ni ile ya kwenda mbele”. Asante kutuelekeza njia ya kumbu kumbu ya wakati ujao”.

Asante kuelekeza kufanya kumbu kumbu

Akitazama mada za tafakari,  Baba Mtakatifu anasema: “Ninakushukura sana kwa kazi hiyo, ninakushukuru kwa kuzungumzia juu ya kukumbu kumbu. Ukuu ambao unatoka katika kitabu cha  Kutoka na ambao tunausahau”, anathibitisha Baba Mtakatifu Francisko na kuongeza, “ kwa kuzungumzia matumaini, kazi, uvumilivu na kutuelekeza njia ya kuweza kuwa na kumbu kumbu, wakati ujao na ambao unatupeleka mbele. Asante!

Mtazamo wao wa tafakari ya mafungo katika siku ya kwanza

Baba Mtakatifu akilezea mtazamo wao wa mafungo hasa kwa mara ya kwanza ya utangulizi  anasema, “Umenifanya nicheke sana uliposema kuwa mtu mmoja aliposoma mada za tafakari, labda alikuwa hajuhi ni kitu gani wameandaa Sekretarieti Kuu. Na labda alifikiri kuwa wamekodisha mtu wa kuwaongoza  wa kitalii ambaye aweze kuwapeleka katika mji wa Firenze ili  kuujua na watunga mashairi ” (…), aidha Baba Mtakatifu ameongeza kusema: “Hata mimi katika tafakari ya kwanza nilibaki bila mwelekeo, lakini baadaye nilitambua ujumbe wako”. Asante!

Zawadi ya Baba Mtakatifu kwa Abate ni hati ya  Mtaguso Gaudium et Spes kwa sababu ya ujasiri wa Mababa wa Mtaguso

Vile vile Baba Mtakatifu akiendelea kumshukuru Abate Maria Gianni anasema: “nimefikiria sana juu ya hati ya Mtaguso ya Gaudium et Spes na labda ndiyo hati ambayo imepata kuvumilia zaidi hata leo. Na wakati mwingine nilikuona hivyo: kama ujasiri wa Mababa wa Mtaguso wakati wanatia sahini katika hati hiyo”. Kwa maana hiyo, ninakushukuru sana. Usali kwa ajili yetu wadhambi, wote ee!, lakini tunataka kwenda mbele hivyo, kwa kuhudumia Bwana. Asante sana na uwasalimie wamonaki kwa niaba yangu na kwa upande wetu. Asante ! Ndivyo alivyo malizia kumshukuru Abate aliye toa takari ya Mafungo ya kiroho kuanzia Jumapili 10-15 Machi katika nyumba ya mafungu huko Ariccia nje ya mji wa Roma.

15 March 2019, 14:43