Tafuta

Vatican News
Papa Francisko anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kusimama kidete kulinda na kutetea Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo! Papa Francisko anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kusimama kidete kulinda na kutetea Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo!  (Vatican Media)

Papa Francisko: Utamaduni wa kifo unatishia Injili ya uhai!

Baba Mtakatifu Francisko anasema, Kanisa libataka kujitosa kuwahudumia kwa ukarimu na upendo, watoto wadogo ambao bado hawajazaliwa zaidi ya wengine wote, kwani hawa ni watu wasio na ulinzi wala hatia. Inasikitisha kuona kwamba, katika baadhi ya nchi, utamaduni wa kifo unalindwa kisheria, jambo linalokwenda kinyume cha haki msingi za binadamu, utu na heshima yake!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kila mwaka ifikapo tarehe 25 Machi, Mama Kanisa anaadhimisha Siku kuu ya Bikira Maria kupashwa habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mkombozi. Siku hii imekuwa ikitumiwa na Mabaraza mbali mbali ya Maaskofu Katoliki kwa ajili ya kuhimiza utamaduni wa maisha, kwa kuwalinda na kuwatunza watoto ambao hawajazaliwa dhidi ya utamaduni wa kifo, unaofumbatwa katika sera za utoaji mimba! Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii, tarehe 25 Machi 2019 amewaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kupokea zawadi ya uhai kwa moyo wa upendo, shukrani na ukarimu.

Hata watoto ambao hawajazaliwa wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Jamii isipojifunza kuwalinda na kuwatunza watu dhaifu, sheria ya mwenye nguvu mpishe, itatawala dunia! Baba Mtakatifu anasema, maskini wanao upendeleo wa pekee mbele ya Mwenyezi Mungu. Wao ni walengwa wa kwanza wa Habari Njema ya wokovu, ni amana na utajiri wa Kanisa. Wao ni dira na ufunguo wa kuingilia mbinguni. Baba Mtakatifu anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kusimama kidete kulinda na kutetea zawadi ya uhai tangu pale mtoto anapotungwa mimba hadi mauti ya kawaida yanapomfika kadiri ya mpango wa Mungu. Baba Mtakatifu anakaza kusema, Kanisa linataka kujitosa kuwahudumia kwa ukarimu na upendo, watoto wadogo ambao bado hawajazaliwa zaidi ya wengine wote, kwani hawa ni watu wasio na ulinzi wala hatia. Inasikitisha kuona kwamba, katika baadhi ya nchi, utamaduni wa kifo unalindwa kisheria, jambo linalokwenda kinyume cha haki msingi za binadamu, utu na heshima yake!

Ikumbukwe kwamba, maisha ya binadamu ni matakatifu yanapaswa kulindwa na kuendelezwa. Utoaji mimba si kitendo cha maendeleo bali ni ukiukwaji wa haki msingi za binadamu! Kanisa lingependa kuwasaidia wanawake kutekeleza vyema dhamana na wajibu wao wa kulea na kutunza vyema watoto ambao ni zawadi kubwa kutoka kwa Mungu! Hii itawezekana ikiwa kama haki msingi zitadumishwa na kuendelezwa; wanawake watawezeshwa kiuchumi ili kupambana na umaskini wa hali na kipato! Baba Mtakatifu anasisitiza kwamba, kitendo cha utoaji mimba ni uhalifu na ukatili mkubwa! Madaktari watambue kwamba, wamekula kiapo cha kulinda na kudumisha uhai wa binadamu! Kifo laini ni kielelezo pia cha utamaduni wa kifo! Baba Mtakatifu anawaomba Mapadre waungamishaji, kuwasaidia wanawake wanaokimbilia huruma ya Mungu kwa njia ya Sakramenti ya Kitubio, kwa kuwapatia ushauri na faraja ili waweze kujipatanisha na Mungu pamoja na watoto wao ambao hawapo tena!

Wanawak
26 March 2019, 12:11