Tafuta

Vatican News
Papa amtunukia zawadi ya heshima Sr. Maria Concetta Papa amtunukia zawadi ya heshima Sr. Maria Concetta  (Vatican Media)

Papa Francisko amtunukia zawadi ya heshima Sr Maria Concetta

Mara baada ya katekesi yake Jumatano 27 Machi 2019,Baba Mtakatifu Francisko amemtunikiwa zawadi ya heshima ya Kipapa kwa mmisionari Sr.Maria Concetta kwaajili ya shukrani katika huduma ya kutumikia watu, hasa watoto wengi waliozaliwa huko Bangui nchini Afrika ya Kati

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko Jumatano 27 Machi 2019 imehitimishwa kwa jambo maalum katika uwanja wa Mtakatifu Petro ambapo Baba Mtakatifu Francisko amemtunukia zawadi ya heshima, mmisionari mmoja Sr. Matia Concetta Esu ambaye kwa miaka mingi amesaidia kuzaliwa kwa watoto wengi katika  nchi ya Jamhuri  ya Afrika ya Kati, hivyo ni kama ishara ya kumpongeza na kumshukuru kwa miaka 60 aliyotimiza akiwa katika huduma ya  maisha yanayozaliwa. Hata hivyo uwepo wake na sura yake ya mzee huyo, umisionari wake wa ujasiri na ushuhuda wake wa kazi ya upendo kwa jina ya Yesu, ulikuwa umegusa sana Baba Mtakatifu Francisko miaka 4 iliyopita huko Bangui, wakati wa ziara yake ya Kitume nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati alipoweza kukutana naye na ambapo kwa  muda mfupi aliporudi  Roma  aliweza kuzungumzia juu yake kwa waamini wakati wa katekesi yake baada ya ziara.  Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko ameweze kwa mara nyingine kukutana naye na kumsalimia kwa furaha kubwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Amemwita yeye mwenyewe mbele ya maelfu ya waamini na mahujaji wote  ili kumtunukia zawadi ya heshima ya Kipapa na shukrani kwa kazi ambayo ameitenda katikati ya dada zake na ndugu waafrika akiwa anajikita katika kutoa huduma ya maisha ya watoto, mama na  familia zao kwa ujumla

Katika ishara hiyo Baba Mtakatifu anataka kuelezea utambuzi  kwa wamisionari  wote wa kike na kiume, mapadre, watawa na walei ambao wanapanda mbegu ya ufalme wa Mungu kila kona ya Dunia. Kazi yao wamisionari wote ni kubwa, kwa maana anasema wao wanaunguza maisha wakiwa wanapanda neno la Mungu kwa njia ya ushuhuda na hivyo amethibitisha kwamba hawa hawatangazwi katika vyombo vya habari. Wao siyo habari katika magazeti. Aidha akiendelea na ufafanuzi juu ya utume amekumbuka historia aliyomweleza Kardinali Hummes ambaye amekabidhiwa katika Baraza la la Maaskofu wa Brazil na kanda ya  Amazoni yote, kwamba mara nyingi anatembelea miji na vijiji vya Amazon. Na  mara nyingi afikapo huko anakwenda kutembelea makaburi ya wamisionari wengi, vijana wengi waliokufa kutokana na kuambukizwa magonjwa bila kuwa na kinga ya kuzuia. Kwa maana hiyo anasema alimwambia kuwa, wamisionari hao wanastahili kutangazwa watakatifu kwa sababu waliunguza maiisha yao katika huduma.  Kutokana na mfano huo ameongeza kusema: Sr Maria Concetta baada ya shughuli hii atarudi Afrika, na hivyo asindikizwe kwa sala na mfano wake uwasaidie wote kuuishi Injili kila mmoja mahali alipo.

Mama Maria  na watoto wa Afrika: Mwanzilishi wao wa Shirika ambaye ni mtumishi wa Mungu Felice Prinetti, baba Mtaktifu anasema, anaomba watoto wake waweze kuwa huduma ya upendo na wepo wa dhati wa upendo upeo wa Mungu. Kila mtu aweze kungia katika madonda ya kila binadamu wa kila wakati, ili kuweza kutia divai ya kutibu na mafuta ya faraja katika utambuzi ya kwamba kila kifanyikacho kwa wale walio  wadogo ni kufaya kwa ajili ya Yesu. Kwa njia hiyo hata Sr. Maria Concetta amegeuka kuwa mama Maria kama wote wanavyo mwita, wawe watoto wadogo, babu na bibi katika kijiji cha  Zongo karibu na mto wa Ubangi, mahali ambapo ameweza kuona vizazi vitatu vinakua na amewafanya mama wazae watoto wengi. Ni mikono iliyo barikiwa, leo kama jana, hakuna kilicho badilika, Baba Mtakatifu amesema.

27 March 2019, 12:35