Tafuta

Vatican News
Papa Francisko anatoa salam za rambi rambi kwa waathirika wa mafuriko nchini Iran Papa Francisko anatoa salam za rambi rambi kwa waathirika wa mafuriko nchini Iran 

Papa atoa Salam za rambi rambi kwa waathirika wa mafuriko nchini Iran

Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kwa ajili ya waathirika wa mafuriko,yaliyoikumba hivi karibuni kanda tofauti za nchi ya Iran.Telegram yake imetumwa na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican kwa niaba yake

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni uchungu kwa ajili ya kupoteza maisha ya binadamu kutokana na mafuriko yaliyo ikumba kanda za Iran. Ndiyo maelezo ya Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wa salam za rambi rambi uliotiwa sahini na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin. Akisali kwa ajili ya watu watu walioko katika jitihada za dharura, Baba Mtakatifu Francisko anawakabidhi kwa Mungu mwenyezi watu wote wa Iran.

Mvua inatarajiwa kunyesha zaidi

Kwa mujibu wa taarifa mahalia vifo vingi vilivyo sababishwa na mafuriko ni karibia 19. Katika nchi bado wataalam wa hali ya hewa wanathibitisha kwamba mvua itaendelea kunyesha, na wakati huo huo viongozi wakuu wa nchi wanawaalika wazalendo wasisafiri katika siku hizi za likizoza mwaka mpya ulioanza tarehe 21 Machi 2019. Idadi kubwa ya waathirika inapatikana katika eneo la Shiraz ambao ni mji Mkuu wa Mkoa wa Fars Kusini. Hata hivyo taarifa zinasema kwamba mvua kubwa inatarajiwa kunyesha hata  zaidi hasa kaskazini na mashariki ya nchi na ipo dharura ya mafuriko hivyo wanatoa taarifa ya kuwa makini sana kwa upande wa wilaya, ikiwemo hata mji Mkuu Teheran.

 

28 March 2019, 09:00