Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa  Sudan Kusini Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Sudan Kusini   (Vatican Media)

Papa amekutana na Rais Salva Kiir Mayardit

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Salva Kiir Mayardit, wa Jamhuri ya nchi ya Sudan Kusini, tarehe 16 Machi 2019 na baada ya mkutano huo amekutana na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican,akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher,Katibu Mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 16 Machi 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Salva Kiir Mayardit, wa Jamhuri ya  watu wa nchi ya Sudan Kusini na baada ya mkutano huo pia  amekutana na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican, akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa. Katika mazungumzo yao, viongozi hawa pande zote mbili wameonesha mahusiano mema yaliyopo kati ya nchi hizi mbili na zaidi katika mchango wa Kanisa Katoliki kwa mantiki ya elimu, afya na mchakato wa mapatano na ujenzi wa Taifa.

Kadhalika kwa pamoja wametazama masuala yanayohusu hali halisi ya sahini ya mkataba wa pamoja uliowekwa hivi karibuni kati ya wadau wa kisiasa, wakati wakingojea kupata suluhisho la mwisho wa migogoro na kuwawezesha kurudi makwao wakimbizi, kadhalika hata wimbi la watu waliokusanyika ndani ya nchi hiyo, na kutazama maendeleo faungamani ya nchi kwa ujumla. Hata hivyo katika mtamzamo huo, mapema Baba Mtakatifu Francisko ameelezea hata shauku ya uhakikisho wa usalama wa hali halisi ya kumwezesha aweze kutembelea nchi ya Sudan Kusini,kama ishara ya ukaribu wa watu na kuwatia moyo katika mchakato wa amani ya nchi!

16 March 2019, 14:37