Rais wa Jamhuri ya Lithuania mjini Vatican Rais wa Jamhuri ya Lithuania mjini Vatican  

Papa akutana na Rais wa Lithuania Bi Grybauskaitė!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya nchi ya Lithuania Bi Dalia Grybauskaitė tarehe 28 Machi 2019,na baadaye kukutana na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican,akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher,Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 28 Machi 2019 Baba Mtakatifu Francisko, amekutana na Rais wa Jumhuri ya Nchi ya Lithuania Bi. Dalia Grybauskaitė. Mara baada ya mkutano huo amekutana na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, akisindikizana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican

Katika mazungumzo yao, wamepongeza juu ya ushirikiano na mahusiano mema yaliyopo baina ya nchi hizo mbili aidha kwa  mchango mkubwa wa Kanisa Katoliki utolewao katika jamii Lithuania. Na kwa namna ya pekee wameweza kukumbuka hata zaiara ya hivi karibuni mwaka 2018 ya Baba Mtakatifu Francisko katika nchi hiyo wakati wa fursa ya kuadhimisha miaka 100 tangu nchi hiyo ipate uhuru wake.  

Baadaye wamezungumzia juu ya  baadhi ya mada zinazohusiana na hali halisi kijamii na kisiasa nchini humo. Hatimaye wamisisitizia juu ya mantiki zenye tabia ya kimataifa kama vile amani, usalama na ulazima wa mshikamano wa pamoja ili kuweza kukabiliana na changamoto mbali mbali za Ulaya na za Kanda.

28 March 2019, 13:17