Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu akitia sahini katika Wosia wa Kitume wa “Vive Cristo, esperanza nuestra”yaani “Kristo anaishi,Tumaini letu”, kwa ajili ya vijana Baba Mtakatifu akitia sahini katika Wosia wa Kitume wa “Vive Cristo, esperanza nuestra”yaani “Kristo anaishi,Tumaini letu”, kwa ajili ya vijana  (Vatican Media)

Papa ameadhimisha Misa katika Kanisa Takatifu na kutia sahini katika Wosia wa kitume

Maadhimisho ya Misa Takatifu katika nyumba ya Loreto na kutia sahini kwenye Wosia wa Kitume baada ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana ndiyo vimechukua uzito wa ziara ya Baba Matakatifu Francisko asubuhi huko Loreto,wakati Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya Kupashwa Habari njema Bikira Maria

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Neno lake kutoka kinywani mwa Bikira Maria: “Iwe kwangu kama ulivyo nena”, ndiyo imekuwa mbiu iliyorudia kusikika katika nyumba Takatifu ya Loreto, mahali ambapo Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 25 Machi 2019,amekwenda mjini Loreto asubuhina kuadhimisha Misa Takatifu  wakati Mama Kanisa anadhimisha Sikukuu ya Kupashwa habari Bikira Maria. Nje ya madhabahu, alisindikizwa na waamini wengi na  kati yao ni wagonjwa. Hata hivyo Baba Mtakatifu, hakufanya mahubiri, bali ametoa maneno mafupi ya utangulizi  katika sala kwa waamini wakati wa misa kwamba:Tazama mimi hapa  ndiyo ya kwanza ikifuatia na nyingine. Ni ndiyo ambayo wakristo wa nyakati zote na wale ambao wameitwa kurudia kuitkka katika maisha yao na katika wito wao. Maria ni sanduku la agano jipya na la milele: Kwake yeye inatimizwa kazi ya Roho Mtakatifu katika fumbo la Mwana wa Mungu aliyefanyika mtu. Tumwelekeze Bwana kwa imani na unyenyekevu katika sala zetu. Tuombe, ee Bwana na iwe kwako kama ulivyonena!

Kutia sahihi Wosia wa Kitume baada ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana 2018

Mara baada ya Misa katika Nyumba Takatifu, mbele ya altare ya Picha ya Bikira Maria mweusi, Baba Mtakatifu Francisko ametia sahini katika Wosia wa Kitume baada ya Sinodi ya Maaskofu unayoongozwa na kauli mbiu “Vive Cristo, esperanza nuestra”yaani “ Kristo anaishi, Tumaini letu” kwa ajili ya vijana, ambayo ilifanyiwa kazi mjini Vatican mwezi Oktoba 2018. Na waliokuwa na Baba Mtakatifu katika Kanisa Takatifu la Nazareti asubuhi  ni Askofu  Fabio dal Cin, Askofu Mkuu wa Loreto, Askofu Mkuu Georg Gänswein, Rais wa nyumba ya Kipapa, Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, Katibu msaidizi wa Uchumi wa  Sekretarieti Vatican, Kardinali Gualterio Bassetti, Rais wa Baraza la Maaskofu Italia, Kardinali Edoardo Menichelli, Askofu Mkuu mstaafu wa Ancona-Osimo, na baadhi ya ndugu wakapuchini, ambao wamekabidhiwa shughuli ya kichungaji kwa wanahija, wakiwa na  baadhi ya vijana ambao kwa kipindi hiki wanaishi kujitafakari juu ya wito wao.

Ni tukio la kihistoria nje ya Vatican kama lile la 1995

Ni tukio la kihistoria kwa wengi kwani kutia sahini ya Wosia wa Kitume nje ya Vatican ilitokea kwa Mtakatifu Yohane Paulo II kunako mwaka 1995 wakati wa ziara yake ya kitume barani Afrika, kwa kwa wosia unaojulikanao, “Ecclesia in Africa” yaani “Kanisa la Afrika”. Na siyo  hiyo tu bali hata kutaka kuthibitisha juu ya uhusiano kati ya vijana na madhabahu ya Loreto, mahali ambapo Mtakatifu Yohane Paulo II na Benedikto XVI walipendelea kukutana na vijana katika eneo hili la Loreto. Kabla ya Misa, Baba Mtakatifu Francisko amesali kwa muda mrefu, kwa ukimya mbele ya Picha ya Mama Maria inayotunzwa katika Nyumba Takatifu. Nje waamini na mahujaji walikuwa wanamsindikiza vile vile kwa ukimya wa sala.

25 March 2019, 11:36