Katekesi ya Baba Mtakatifu 27 Machi 2019 Katekesi ya Baba Mtakatifu 27 Machi 2019 

Katekesi ya Papa:Mkate unaotolewa kama zawadi kwa binadamu ushirikishwe!

Katika Katekesi ya tarehe 27 Machi 2019,Papa ametafakari sehemu ya pili ya sala ya Baba Yetu ambapo anasema inawakilisha Mungu katika mahitaji yetu ya kuishi kama vile mkate wetu wa kila siku.Kwa hiyo amewafikiria baba na mama wengi ambao leo hii wanakwenda kulala bila kupata chakula kwa ajili ya watoto wao.Ni lazima kukumbuka wanaoteseka

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Leo hii tunaaza kufafanua sehemu ya pili ya Baba Yetu ambayo inawakilisha Mungu katika mahitaji. Katika sehemu ya pili inaanza na neno linalonukia kila siku yaani mkate. Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 27 Machi 2019 wakati mwendelezo wa katekesi yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro  mjini Vatican kuungana katika tafakari hii ya kila Jumatano. Katika mwendelezo wa ufafanuzi wa sala ya Baba Yetu, anasema, katika sala ya Yesu, inaanza na swali la kujiuliza na ambalo linAfanana na maombi ya mtu omba omba. “Utupe leo mkate! Sala hii inatoka mahali ambapo sisi tunasahau daima. Ina maana ya kusema, sisi ni viumbe tusiyo jitosheleza,ambao kila siku tunahitaji kulishwa. Maandiko matakatifu yaonaonesha kuwa, watu wengi waliokuwa wanakutana na Yesu waliweza kujikamilisha kuanzia katika maombi. Lakini Yesu hataki maombi ya kijuuu juu tu, badala yake anataka mahitaji ya kweli ya binadamu na kila siku hayo yanaweza kugeuka kuwa maombi.

Yesu hakufanya sintofahamu mbele ya maombi  hata uchungu

Katika Injili tunakutana na watu wengi wanao omba omba, ambao wanaomba uhuru na wokovu. Kwa mfano kuna anayeomba mkate, anayeomba uponywaji; baadhi wanaomba kutakaswa na wengine wapate kuona; au kumwombea mtu mpendwa wao aweze kupona… Katika maombi hayo, Baba Mtakatifu Ffrancisko anaongeza, Yesu hakufanya sintofahamu mbele ya maombi hayo na uchungu huo. Kwa njia hiyo Yesu anatufundisha kumwomba Baba mkate wa kila siku. Anatufundisha kufanya hivi kwa kuungana na wanaume na wawake ambao wanasali sala hii mara nyingi ndani ya mioyo yao wakiwa na wasiwasi wa kila siku. Je ni mama wangapi na mababa wangapi leo hii wanakwenda kulala usingizi wakiwa na hisia mbaya ya kutoweza kupata mkate kesho yake kwa ajili ya watoto wao? Ni vema kufikiria sala hii inayo ombwa, na si katika usalama wa wenye majumba mazuri, lakini  ni katika sehemu ambazo wanahitaji mahitaji ya lazima ya kuishi. Maneno ya Yesu yanajikita katika mtindo mpya  na sala ya kikristo inaanza kwa ngazi hiyo. Siyo sala ya mchazo, bali  inaanzia na hali halisi; inaanzia katika moyo na mwili wa mtu ambaye anahitaji au anashirikishana na hali halisi na yule ambaye anahitaji ili awze kuishi. Hata wakristo watafakari wakuu katika sala, hawakwenda kunyume na sala hii ya maombi. "Baba wajalie wote, leo hii wapate mkate wa lazima". Pamoja na mkate vinafuatia hata vitu vingine kama maji, dawa, nyumba na kazi. Ni kuomba kwa ajili ya mahitaji ya lazima ya kuishi Baba Mtakatifu akabainisha.

Mkate ambao mkristo anaomba katika sala siyo mkate wangu

Mkate ambao mkristo anaomba katika sala siyo mkate wangu, hivyo lazima kuwa na umakini huo, Baba Mtakatifu ametoa angalisho. Kwa sababu, ni mkate wetu na ndiyo Yesu anapenda hivyo. Yeye anatufundisha kuomba, si kwa ajili yetu binafsi, bali kwa ajili ya ndugu wote duniani. Iwapo hatusali kwa namna hiyo, yaani  Baba Yetu, hakuna sala ya mkristo anathibitisha Baba Mtakatifu. Akendelea na tafakari anasema: Iwapo Mungu ni  Baba Yetu, tunawezaje kujiwakilisha kwake bila kushikana mkono sisi sote? Je  iwapo mkate ambao yeye anatujalia tunauiba kati yetu, tunawezaje kusema sisi ni watoto wake?  Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu anafafanua kwamba, sala hii ina ina tabia ya mtazamo wa huruma, na tabia ya mshikamano! Ni  kihisi njaa yangu kama njaa ya wengine, basi nitasali kwa Mungu ili hata maombi yao yaweze kusikilizwa. Na ndiyo jinsi ambavyo Yesu anaelimisha jumuiya yake, Kanisa lake ili kupeleka kwa Mungu mahitaji ya wote kuwa: “ sisi ni wana wako, au Baba utuhurumie”. Kwa maana hiyo anathibitisha kuwa, itakuwa vema kusimama na kufikiria watoto wenye njaa. Kufikiria watoto ambao wanaishi katika nchi zenye migogoro ya kivita; watoto wenye njaa nchini Yemen, watoto wenye njaa Siria na watoto wenye njaa katika nchi ambazo hakuna mkate kama vile Sudan ya Kusini.

Kifikiria watoto hawa na kusali kwa sauti ya juu “utupe leo mkate wetu wa kila siku

Kwa kufikiria watoto hao, Baba Mtakatifu Francisko anasema, kwa pamoja ni kusali sala kwa sauti ya kuu; "Baba utupe leo mkate wa kila siku"…. Wote wamerudia sala hiyo ….. Mkate  tunaoomba kwa Bwana katika sala ndiyo mkate huo ambao kila siku unatuhukumu. Na Bwana  anatukaripia kutokana na ukawaida wa kukosa kuumega mkate kwa yule aliye karibu na ukawaida wa kukosa kushirikishana. Ni mkate ulitolewa bure kwa binadamu, na badala yake umeliwa na mmoja tu. Upendo hauwezi kuvumilia hili. Upendo wetu hauwezi kuvumilia;hata upendo wa Mungu hauwezi kuvumila ubinafsi, yaani ile tabia ya kutoshirikisha mkate, amekazia Baba Mtakatifu! Akirudia kusoma soma la Injili iliyosomwa mwanzo anasema: kulikuwa na umati mkubwa mbele ya Yesu  na watu walikuwa na njaa, Yesu akaulizwa iwapo kulikuwapo na chochote cha kuwapatia umati huo,  lakini alikuwapo kijana mmoja tu aliyekuwa tayari kushirikisha alichokuwa nacho yaani mikate mitano na samaki wawili. Yesu aligawa mikate hiyo katika ishara ya ukarimu. (rej Gv 6,9). Baba Mtakatifu anaongeza kusema  kijana huyo alitambua somo la Mkate wetu ya kwamba, chakula siyo mali binafsi, kwa maana hiyo, zingatieni katika  vichwa,  kwamba chakula siyo suala la binafsi, bali ni zawadi ya kushirikishana na neema ya Mungu.” Miujiza ya kweli iliyotengenezwa na Yesu kwa siku ile, siyo wingi wa mikate hata kama ni kweli, lakini ilikuwa ni ushirikishaji. IKiwa na maana: "toeni kile ambacho mmepokea bure na mimi nitafanya miujiza". Yeye mwenyewe katika kutoa mikate mingi, alionesha utangulizi wa sadaka yake katika Fumbo la Mkate wa Ekaristi. Kwa hakika ni katika Ekaristi ina uwezo wa kushibisha njaa isiyo isha na tamaa ya Mungu ambayo inamwongoza mtu hata katika kutafuta mkate wa kila siku.

 

 

27 March 2019, 12:10