Tafuta

Vatican News
Ziara ya Papa katika Madhabahu ya Mama Maria wa Loreto Ziara ya Papa katika Madhabahu ya Mama Maria wa Loreto  (Vatican Media)

Papa anasema kwa mfano wa Maria tupeleke Injili katika dunia iliyo changanyikiwa!

Nje ya uwanja wa Madhabahu ya Nyumba Takatifu ya Loreto,Papa amezungumza na vijana na kuwashauri watembee katika njia ya amani na udugu;wanafamilia wafikirie dhabahu la upendo;kwa wagonjwa watulizwe na Bikira Maria anayebeba huruma zote za Bwana.Kadhalika ameeleza kuhusu Wosia wa Kitume baada ya Sinodi,“Christus vivit"

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika  hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko kwa mahujaji na waamini waliokusanyika katika uwanja wa Madhabahu ya Bikira Maria Loreto tarehe 25 Machi 2019, wakati wa ziara yake katika madhabahu hayo, ni mara baada ya kumaliza misa Takatifu na kutia sahini katika Wosia wa Kitume baada ya Sinodi ya Maaskofu iliyofanyika mwezi Oktoba mwaka jana, kwa ajili ya vijana unaoongozwa na kauli mbiu "Christus vivit"yaani Kristo ni hai. Akianza hotuba hiyo anasema, asante kwa sana kwa makabaribiso yenu ya nguvu. Neno la Malaika Gabrieli kwake Maria:"furahi umejaa neema" (Lk 1,28) lilitangazwa kwa namna ya pekee katika madhabahu hayo, ambayo ni sehemu maalum ya  pekee ya kutafakari fumbo la Mwana wa Mungu aliyefanyika mwili. Kwa hakika kuta hizo kwa mujibu wa utamaduni zinatoka Nazareti, mahali ambapo Bikira Maria alitamkia, “tazama mimi mjakazi” na akawa Mama wa Yesu. Ndiyo nyumba ya Maria na ambayo inayotajwa  na kugeuka kuwa uwepo na kupendwa katika kilima hicho. Ni Mama wa Mungu ambaye hakosi kuwajalia neema za kiroho wale ambao kwa imani na ambao wanakuja kusali. Baba Mtakatifu anaongeza kusema, “kati ya hawa, nami ni mmojawapo na ninamshukuru Mungu kunijalia kufika  katika siku hii ya tukio la Kupashwa habari Bikira Maria".

Shukrani kubwa kwa ndugu wadogo wakapuchini kwa kuungamisha katika madhabahu

Baba Mtakatifu anawasalimia viongozi wote na kuwashukuru ukarimu wa makaribisho na ushirikiano wa Askofu  Mkuu Fabio Dal Cin, ambaye ni  Askofu Mkuu wa Madhabahu  ya Loreto, kwa hotuba yake akiwakilisha jumyai nzima; kadhalika shukrani kwa  ndugu wadogo wakapuchini ambao wanalo jukumu la  kusimamia madhabahu hiyo pendevu kwa watu wa Italia anathibitisha Baba Mtakatifu . Anawasifu kwamba daima wako makini katika taaluma yao na ili kuwafanya watu waingie katika madhabahu  hiyo kwa utataribu, na wakati huo huo  hawakosi kuwapo mmoja, wawili, watatu au wanne, lakini daima wapo kuwaungamisha  watu daima kila siku. Na hiyo ni kazi kubwa, kwa njia hiyo nawashukuru kwa namna ya pekee katika hilo na kwamba ni shughuli  yenye thamani ya maungamo ambayo inaendeelea kwa siku nzima. Kadhalika shukrani  zake amezitoa kwa raia wa Loreto na mahujaji wote amewapa salam.

Madhabahu ya Loreto ni Oasis ya ukimya na uhuruma

Katika Oasis hii ya ukimya, ya huruma, ni  watu wengi wanakuja  kutoka Italia na sehemu mbalimbali za dunia, ili kuchota nguvu na matumaini. Baba Mtakatifu Francisko anafikiria kwa namna ya pekee vijana, familia na wagonjwa. Nyumba Takatifu ni nyumba ya vijana, kwa sababa Bkiria Maria, kijana aliye jaa neema anaendelea kuzungumza kwa kizazi kipya na kuwasindikiza kila mmoja katika kutafuta wito wake. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anathibitisha juu ya utashi wake wa kutia sahini  katika  Wosia  wa Kitume na kwamba ni tunda la Sinodi iliyokuwa ya vijana. Wosia huo ni wenye kauli mbiu “Christus vivit” yaani “Kristo ni hai”.Na katika  tukio la kupasha habari, anasema, kuna mwendelezo wa wito ambao unajifafanua katika hatua tatu ambazo walijikita nazo katika Sinodi. Ya kwanza ni kusikiliza neno ambalo ni  mpango wa Mungu; pili ni  kufanya mang’amuzi;  na tatu ni Maamuzi.

Ufafanuzi wa hatua tatu hizo: ya kwanza kusikiliza neno

Baba Mtakatifu Francisko anafafanua kuwa sehemu ya kwanza ya kusikiliza imejionesha kutoka katika neno la Malaika lisemalo; “usiogope Maria(…) utazaa mtoto na utamwita jina Yesu” (Lk 1,30-3). Daima ni Mungu anayeanza kuita ili kumfuasa. Ni Mungu anayeanzisha akiwa wa kwanza daina na ndiyo anakwenda akiwa wa kwanza kwa kufungua njia ya maisha yetu. Wito katika imani na udhati wa safari ya maisha ya kikristo au wito maalum wa kutiwa wakfu ni jambo gumu na  makini   lakini ni nguvu ya Mungu katika maisha ya kijana,ili kuweza kumtolea zawadi kwa ajili ya upendo. Baba Mtakatifu anabasisitiza kuwa inahitajika utayari na uwezekano wa kusikiliza na kupokea sauti ya Mungu ambayo haiwezi kutambulika katika kelele na vurugu. Ishara yake katika maisha binafsi na kijamii haiwezi kuchukuliwa na kubaki ya kijuu juu tu, lakini ni kushuka kwa ngazi ya chini kabisa, mahali ambapo nguvu za kimaadili na kiroho hufanya kazi ndani mwake. Na ndiyo mahali ambamp Maria anawaalika vijana washuke chini na washikamane na matendo ya Mungu.

Hatua ya pili ni kufanya mang’amuzi

Na hatua ya pili ya kila wito Baba Mtakatifu anathibitisha ni kufanya mang’amuzi, ambayo yamejifafanua katika maneno ya Maria: “itawezekanaje hiyo hali mimi ni bikira?” (Lk 1,34) Maria hakuwa na wasi wasi; na swali lake siyo la kukosa imani, badala yake ni kuelezea utashi wake wa kutaka kugundua zaidi mshangao wa Mungu. Kwake yeye yupo makini na kutaka kupokea kila dharura ya mpango wa Mungu juu ya maisha yake, na anamtambua hivyo katika sura zake, ili aweze kuwajibika zaidi, na kukamilisha ushirikiano wake. Hii ndiyo tabia ya mfuasi, Baba Mtakatifu anasisitiza na kwamba kila ushirikiano wa kibinadamu na shughuli ya Mungu lazima itafakariwe kwa kina katika uwezo wake na tabia zake, lakini kwa kutambua kwa dhati ya kuwa Mungu daima anatoa na kutenda; kwa njia hiyo hata umasikini na udogo kwa wale ambao Bwana anawaita kumfua katika njia ya Injili anawabadili katika utajiri wa mwonekano wa Bwana, na kwa nguvu ya mwenyezi.

Hatua ya tatu ni ile ya kufanya maamuzi

Baba Mtakatifu anasema, uamuzi ambao ndiyo hatua ya tatu na wenye tabia ya kila wito wa kikristo umefafanuliwa katika jibu la Maria kwa Malaika: “mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe kama ulivyosema” (Lk 1,38). Jibu lake Tazama mimi hapa katika mpango wa wokovu wa Mungu kwa njia ya Neno kufanyika mwili, ndiyo makabidhiano na yeye katika maisha yake yote. Baba Mtakatifa anafafanua kuwa ni “ndiyo” iliyojaa imani na utayari wa dhati katika mapenzi ya Mungu. Maria ni mfano wa kila wito, ni mfano wa kuigwa kwa kila uchungaji wa miito. Kwa vijana ambao wanatafuta au kujiuliza wenyewe juu ya wakati wao endelevu, wanaweza kupata kutoka kwa Maria ambaye anawasaidia kung’amua mpango wa Mungu juu yao binafsi na kwa nguvu ya kuweza kuwa wafuasi wake.

Maombi ya Baba Mtakatifu

Hata hivyo Baba Mtakatifu ametbitisha kwamba Loreto ni sehemu mwafaka mahali ambapo vijana wanaweza kwenda kutafuta wito wao binafsi katika shule ya Maria! Ni ncha ya kitasaufi katika huduma ya miito kichungaji. Kwa maana hiyo ametoa matashi yake ya kufanya kituo cha Yohane Paulo II kwa ajili ya huduma ya Kanisa la Italia na kwa ngazi ya Kimaifa ili kiweze kuendelea kama maelekezo unaojikita ndani ya Sinodi. Iwe ni sehemu ambayoVijana na walimu wao wanaweza kuhisi kusikilizwa, kusindikizwa na kusaidiwa mang’amuzi yao.  Aidha ameomba kwa shauku kubwa Ndugu wadogo wakapuchini waweze kutoa huduma yao na kuongeza masaa ya kufunga Nyumba Takatifu wakati wa usiku sana, kwa ajili ya kuwapatia fursa makundi ya vijana wanaokwenda kusali kwa ajili ya kujitafuta miito yao.

Na kwa wale ambao wanafanya ibada katika Madhabahu hiyo kwa njia ya Mama Maria anawakabidhi utume katika nyakati hizi, hasa kukuba Injili ya amani na ya maisha kuwapelekea watu wa nyakati zetu ambao wamejisahau, wakiwa wanahangakia mambo ya kidunia na katika hali ya ukavu wa kiroho. Kuna haja ya watu rahisi na busara, wenyenyekevu na wajasiri, masikini na wakarimu. Kwa hakika ni  watu ambao katika shule ya Maria wanapokea bila kujibakiza Injili katika maisha yao. Na kwa njia ya utakatifu wa watu wa Mungu katika eneo hilo wanaendelea kueneza nchini Italia, Ulaya na duniani kote ule ushuhuda wa utakatifu na kila aina  ya maisha, ili kupyaisha Kanisa na kuhamasisha jamii kwa njia ya chachu ya Ufalme wa Mungu.

Maria chemi chemi ya kila faraja, awe msaada na kuwatia moyo kwa wale wote wanaojaribiwa

Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu anasema Bikira Maria awasaidie wote hasa vijana, watembee katika njia ya amani na udugu unaojikita juu ya makaribisho na juu ya msamaha, heshima kwa wengine na juu ya upendo ambao ni zawadi hai. Mama yetu, nyota angavu ya furaha na utulivu, awapatie familia dhabahu la upendo, baraka na furaha ya maisha. Maria chemi chemi ya kila faraja, awapatie msaada na kuwatia moyo kwa wale wote wanaojaribiwa. Na kwa njia ya nia hizo, waungane pamoja katika sala ya Malaika wa Bwana, amehitimisha Baba Mtakatifu.

 

25 March 2019, 14:06