Baba Mtakatifu Francisko anataka kuyakabidhi matunda ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana 2018 chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa. Baba Mtakatifu Francisko anataka kuyakabidhi matunda ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana 2018 chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa. 

Papa Francisko: Wosia wa Kitume "Vive Cristo, esperienza nuestra"

Tarehe 25 Machi 2019 kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Loreto, Baba Mtakatifu Francisko atatia mkwaju kwenye Wosia wa Kitume baada ya Sinodi ya Maaskofu unaoongozwa na kauli mbiu “Vive Cristo, esperanza nuestra” yaani “Muishi Kristo, Tumaini letu” ambao kwa mara ya kwanza umeandikwa kwa lugha ya Kihispania. Ufafanuzi unatarajiwa kutolewa baadaye!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Maadhimisho ya Siku kuu ya Bikira Maria kupashwa habari kwamba, atakuwa ni Mama wa Mungu kwa mwaka 2019 yanabeba uzito wa pekee, katika maisha na utume wa Kanisa, kwani Baba Mtakatifu Francisko anapenda kumkabidhi Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa, matunda ya maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana, iliyoadhimishwa mjini Vatican kuanzia tarehe 3-28 Oktoba 2018. Sinodi hii, imeongozwa na kauli mbiu “Vijana, imani na mang’amuzi ya miito”.

Tarehe 25 Machi 2019 kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Loreto, Baba Mtakatifu Francisko atatia mkwaju kwenye Wosia wa Kitume baada ya Sinodi ya Maaskofu unaoongozwa na kauli mbiu “Vive Cristo, esperanza nuestra” yaani “Muishi Kristo, Tumaini letu” ambao kwa mara ya kwanza umeandikwa kwa lugha ya Kihispania. Askofu mkuu Fabio Dal Cin, Msimamizi wa Kitume wa Madhabahu ya Bikira Maria wa Loreto anasema, Baba Mtakatifu Francisko amewapatia heshima kubwa kwa kuamua kutia sahihi Wosia wa Kitume “Vive Cristo, esperanza nuestra” kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Loreto.

Kwa kawaida matukio kama haya, yanafanyika mjini Vatican, lakini kwa heshima na Ibada kwa Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa, Mwaka huu, Baba Mtakatifu anatia mkwaju Wosia huu, akiwa nje ya Vatican. Tukio hili litakuwa ni sehemu ya historia endelevu ya Madhabahu ya Bikira Maria wa Loreto anasema Askofu mkuu Fabio Dal Cin. Huu ni mwaliko kwa vijana kumkimbilia Bikira Maria kwa sala na tunza yake ya kimama!

Papa: Wosia wa Kitume

 

21 March 2019, 09:43