Tafuta

Vatican News
Tamaa ya kupenda kuwa navyo daima,utukufu wa kibinadamu na kumtumia Mungu kwa manufaa binafsi. Hizi ni njia tatu zinazo tupeleka katika uharibifu Tamaa ya kupenda kuwa navyo daima,utukufu wa kibinadamu na kumtumia Mungu kwa manufaa binafsi. Hizi ni njia tatu zinazo tupeleka katika uharibifu 

Angelus:Husifanye mazungumzo na ibilisi bali mjibu kwa neno la Mungu!

Katika tafakari ya la Neno la Mungu wakati wa sala ya Malaika wa Bwana,Baba Mtakatifu, ametoa angalisho kwa waamini na mahujaji wote tarehe 10 Machi 2019 kuwa wawe makini kutengeneza maisha yao kiundani katika imani kwa Mungu,uhakika wa upendo wake na ndiyo njia ya kuthibiti vishawishi dhidi ya ibilisi na waepuke mazungumzo na ibilisi

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ndugu wapendwa, Injili ya Dominika ya kwanza ya Kwaresima (Lk 4,1-13) inasimulia juu ya uzoefu jaribio la Yesu katika Jangwa baada ya kufunga kwa siki arobaini. Yesu alijaribiwa mara tatu na ibilisi. Kwanza anamwalika abadili mawe kuwa mkate ( Lk 4,3); baadaye akampadisha juu na akamwonesha miliki zote za ulimwengu akimlaghai kuwa atakuwa masiha mwenye nguvu na utukufu akimsujudia (Lk 4,5-6); na mwisho akamwongoza mpaka juu ya kinara cha Hekalu la Yerusalemu na kumwalika ajitupe chini ili kuonesha maajabu na  nguvu zake kimungu (Lk 4,911).

Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 10 Machi 2019 kwa mahujaji na waamini waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican, ikiwa ni dominika ya kwanza ya Kwaresima ambayo imefunguliwa na Injili ya Mtakatifu Luka akionesha majaribu aliyopata Yesu akiwa amemaliza siku arobaini jangwani akifunga na kusali. Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari hii anabainisha kwamba vishawishi vitatu vinaeleza njia tatu ambazo daima dunia  imekuwa inapendekeza na kuahidi mafanikio makubwa, njia tatu za kutulaghai. Kwanza tamaa mbaya ya kupenda kuwa navyo daima, utukufu wa kibinadamu na kumtumia Mungu kwa manufaa binafsi. Hizi ni njia tatu zinazo tupelekea katika uharibifu.

Njia ya kwanza ni tamaa ya kutaka kuwa navyo daima. Imekuwa daima ni mantiki mbaya ya ibilisi. Yeye anaanzia katika asili na sheria ya mahitaji ya mwanadamu kama chakula, kuishi, kujikamilisha, kuwa mwenye furaha na kutusukuma tuamini kwamba kila kitu kinawezekana bila kuwa na msaada wa Mungu na hadi kufikia kumshambulia na kumkana Yeye.

Kishawishi cha pili  ni njia ya kutaka sifa za kibinadamu. Ibilisi anasema kama utanisujudia mbele yangu, yote yatakuwa yako (Lk 4,7). Baba Mtakatifu anathibitisha kwa kukumkubuka safari ndefu ya watu wateule kupitia jangwa, Yesu anathibitisha ule utashi wa kujikabidhi kwa imani kubwa kwa Baba yake ambaye daima anawajali watoto wake. Unaweza kupoteza hadhi binafsi,inaharibiwa na mihungu fedha, mafaninikio na madaraka,ili kufikia majivuno binafsi. Hii inahusika na kuonja furaha za utupu ambazo zinayoyoma mapema.Kwa namna hiyo Yesu anajibu ;imenenwa , msujudie Bwana Mungu wako mwabudu yeye peke yake(Lk 4,8).

Kishawishi cha tatu: kutumia Mungu kwa ajili ya faida binafsi: Katika maandiko matakatifu, wanaonesha ibilisi akimwalika amtafuta Mungu katika miujiza ya kushangaza, Yesu anampinga kwa maamuzi thabiti ya kubaki na unyenyekevu, kubaki na imani mbele ya Baba kwa maana anasema: imeandikwa hivi usimjaribu Bwana Mungu wako (Lk 4,12). Na kwa njia hiyo anazuia vishawishi hivi vya kichini chini, hasa vile vya kutaka kuvuta Mungu kwa upande wetu, kuomba baraka ambazo ki ukuwli ni kwa ajili ya matakwa viburi binafsi.

Hizi ndizo njia ambazo tunawekewa mbele za kutaka kuwa na faida binafsi na furaha. Lakini ki ukweli ni ni ambazo ni tofauti na mtindo wa Mungu; na zaidi nji hizi zinatutenganisha na Mungu kwa maana ni kazi ya Ibilisi. Yesu anakabiliana hawali ya yote majaribu haya na anashinda kwa mara tatu ili kuweze kuendelea na mpango wa Mungu. Yesu anatuelekeza njia ya kufanya, kwanza maisha ya kundani, imani kwa Mungu uhakika wa jina lake, uhakika kuwa Mungu anatupenda , na ni Baba, na kwa uhakika huo tutaweza kushinda vishawishi.

Lakini kuna jambo moja ambalo  Baba Mtakatifu anasema ni lazima watambue hasa kuwa wote wawe na makini na muhimu. Yesu katika kumjibu ibilisi hakuingia naya katika mazungumzo, bali alimjibu changamoto zake tatu kwa kutumia Neno la Mungu. Hiyo inatufundisha kuwa nasi tusiwe na mazungumzo na ibilisi, kuwa makini na mazungumzo na ibilisi, tusimpatie nafasi na badala yake ni kumjibu tu kwa kutumia neno la Mungu. Tutumie kipindi cha Kwaresima hii kama kipindi mwafaka cha kujitakasa na kufanya uzoefu wa faraha kutokana na uwepo wa Mungu katika maisha yetu. Kwa maombezi ya Mama Bikira Maria, sura aminifu kwa Mungu atusaidie katika safari na kusaidia kutupilia mbali mabaya na kupokea yaliyo mema.

 

11 March 2019, 09:39