Tafuta

Baba Mtakatifu ametuma ujumbe kwa njia ya video katika jukwa la Kimataifa huko Dubai Baba Mtakatifu ametuma ujumbe kwa njia ya video katika jukwa la Kimataifa huko Dubai 

Ujumbe wa Papa kwa njia ya video katika Jukwaa la Dubai

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya video katika Jukwa la Kimataifa huko Dubai. Ni Jukwaa la siku mbili tarehe 10-12 Februari 2019 ambapo anawataka washiriki watafute njia zipi za kujenga dunia iliyo bora kwa pamoja na kufikiria watu masikini zaidi ya mambo ya kiuchumi

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Kunzia tarehe 10 hadi 12 Februari 2019 mjini Dubai nchi za Falme za Kiarabu kunafanyika Jukwa la Mataifa duniani. Hili ni jukwaa kubwa duniani kwa ushiriki wa wawakilishi wa viongozi wakuu wa mataifa na mashirika ya kimataifa, wataalam mbalimbali ili kujadiliana matendo ya dhati yanayotakiwa kwa serikali na ubunifu wa  maendeleo katika huduma ya sekta ya umma. Katika fursa hiyo la jukwa ya kimataifa, hata Baba Mtakatifu Francisko, ametuma ujumbe wake kwa njia ya video akianza na salama ya, Al Salamù Alaikum /  Amani iwe kwenu!

Katika ujumbe wake, anawatakia matashi ya kazi njema na kuwasimulia juu ya kumbukumbu aliyo nayo bado moyoni mwake kufuatia na ziara yake ya hivi karibuni ya Falme za Kiarabu, wakati huo huo akikumbuka hata makaribisho mema aliyoyapata. Katika nchi ambayo inatafuta kubadilika kwa  kuanzishwa kwa maneno ya uvumilivu, udugu, heshima ya pamoja na uhuru,Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba wameona ni kwa jinsi gani maua yanaweza kuchanua katika jangwa. Amerudi nyumbani akiwa na matumanini ya kwamba hata katika majangwa mengi duniani, yanaweza kuchanua maua. Hilo analiamini na kwamba  inawezekana japokuwa ni kwa njia tu  kukua kwa pamoja karibu na mwingine, ufunguzi na heshima, uwezekano wa kuchukuliana matatizo ya wote ambayo katika kijiji cha dunia matatizo ni ya kila mmoja. Amebainisha!

Baba Mtakatifu anasisitizia juu ya kufikiria jitihada zao katika siku hizi, mahalia ambamo wanakabiliana na mada msingi na kati ya hizo ni changamoto za kisiasa, maendeleo ya kiuchumi, kulinda mazingira na jitihada za kiteknolojia. Ni matashi yake mema kwamba maswali msingi katika tafakari yasiwe fursa tu  ya kujiuliza ni kwa namna gani ya kuweza kuzaa matunda, badala yake iwe tafakari ya kutafuta ni  kwa njia zipi wanaweza kujenga dunia ili bora ya pamoja. Tafakari hiyo iwapelekee kujikita katika kufanya kazi pamoja kwa kufikiria watu zaidi wale ambao wanajikita katika mambo ya kiuchumi; tafakari ambayo haitazami kwa haraka mambo ya  kesho, badala yake ya kutazama hata wakati endelevu na uwajibikaji  ambao kwa wote wanapaswa na wamebeba ili kuonesha ulimwengu huu na wale ambao watafuata baada ya sisi, kwa kufukiria zaidi majanga ya mazingira zaidi ya maadili.

Huwezi kuzungumza maendeleo endelevu bila mshikamano: Baba Mtakatifu akikumbuka waraka wake wa Laudato si, (kipengele 159) anathibitisha kwamba kwa hakika uwezi kuzungumza juu ya maendeleo endelevu bila mshikamano. Tunaweza kufikiria kusema kuwa wema  kama siyo wa pamoja hauwezi kweli kuwa wema. Katika kipinid cha nyakati hizi kufikiria na kutenda ndiyo inahitaji mazungumzo ya kweli na mwingine kwa sababu bila mwingine hakuna wakati endelevu hata mtu binafsi. Kwa maana hiyo anawatakia mema mengi na kwamba katika shughuli zao waanzie na sura za watu, wahisi kilio cha watu na masikini na watafakari juu ya masuala ya watoto. Kwa mawazo hayo anawashukuru na kuwatakia mema katika huduma ya pamoja na kumwaomba Bwana awabariki katika jitihada zao kwa ajili ya dunia yenye haki na matashi ustawi wa wote. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya  Web:  https://www.worldgovernmentsummit.org/

11 February 2019, 15:11