Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amekutana na wawakilishi wa Apostoliki Diaconia wa kanisa la Kiorthodox Ugiriki Papa Francisko amekutana na wawakilishi wa Apostoliki Diaconia wa kanisa la Kiorthodox Ugiriki  (Vatican Media)

Papa:Wafuasi wa Kristo wasiwe wafungwa wa utofauti

Katika ukumbi wa mapapa,Baba Mtakatifu Francisko amekutana na uwakilishi wa“Apostolikì Diakonia” wa Kanisa la Ugiriki na ambapo anapongeza matunda ya ushirikiano na mazungumzo kati ya wakatoliki na waorthodox.Amehimiza kuwa mituemwa Kristo wasiwe ni wafunguwa wa utofauti

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 25 Februari 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wawakilishi wa Apostoliki Diakonia, na kuwapokea kwa shangwe na kuwashukuru kwa ziara yao, kwa namna ya pekee Askofu wa Agathanghelos. Na kuwaomba mara moja watakaporudi Atene wamfikishie salam zake Mkuu wa Kanisa la Ugiriki Ieronymos II, ambaye tarehe 16 Februari ameadhimisha miaka 11 tangu kuchaguliwa kwake katika Kanisa hilo. Baba Mtakatifu anasali kwa Baba ambaye ni mwenye kushusha kila zawadi nzuri na kila zawadi kamilifu (Yk 1,17) amjalie afya, utulivu na furaha ya kiroho. Anamwombea hata kwa maombezi ya Mtume Paulo ambaye alitangaza Injili Ugiriki na kutimiza ushuhuda wake hadi kufiadini Roma, awajalie neema watu wapendwa wa Ugiriki.

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake amethibtisha kuwa ushirikiano kati ya Apostoliki Diakonia na Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuhamasisha umoj owa wakristo kwa zaidi ya miaka 15 unajionesha mwanga na pongezi ya mipango ya utamaduni na mafunzo. Ni mfano mzuri na ambao umeleta matunda ambayo wakatoliki na waorthodox wanafanya kazi pamoja. Katika mchakato wa safari ya aliyeanzisha na ambaye ameweezsha kuendeleza msingi wa vijana wanafunzi katika Makanisa, ameweza kufanya uzoefu na kuona ni kwa njia gani pamekuwapo na umoja  zaidi ya matarajio kwa miaka.

Baba Mtakatifu anasema kuwa, kufanya kazi kwa pamoja inasaidia kujigundua kwa upya udugu. Vijana wanatufundisha tusikae kama wafungwa wa utofauti, badala yeke ni kuwa na utashi wa kutembea pamoja tukifuata iòi kushinda matatizo yanayozuia ukamilifu wa muungano. Na hii inatazama upande wetu kuendelea kutembe pamoja  na kufanya kazi kwa pamoja ili kuweza kujigundua kwa upya undugu. Hatua kwa hatua, katika kile tufanyacho,  tunaweza kuona,kwa msaada wa Mungu na uwepo wa upendo wake ambao unatuunganisha katika umoja daima kwa nguvu zaidi. Baba Mtakatitifu ameongeza kusema kwamba anaomba pamoja nao kuombaili kutambua hili: siyo kila mmoja atembea njia yake, kwa kufuata hatma yake binafsi, utafikiri mwingine hana historia  iliyowekwa pembeni mwake bali nikutambua kama  wote ni ndugu ambao kwa msaada wa Mungu alifanya kukutana na ambaye tunatembea kwa pamoja kuelekea kwa Bwana mmoja na tukichukuliana mizigo mmoja na mwingine, tukifurahia mmoja na mwingine. Anashukuru chombo hiki Apotoliki Diaconia kwa hatua kubwa waliyokamilisha katika mchakato wa safari na anawahakikishia ushirikiano wa na msaada wa Kanisa Katoliki ili waweze kuendelea na mchakato huo wa safari.

 Utume wa uchungaji wa familia ni muhimu na wa kina katika kambi ya ushirikiano kati ya Waorthodox na wakatoliki, katika kambi ambayo anasema inahitaji kupapaliwa kwa shauku na dharura. Katika kambi hiyo ina tabia ya mabadiliko mengi ya haraka katika jamii, na ambayo inakubwa na ongezeko la udhaifu wa undani. Familia za kikristo, japokuwa wapo katika mantiki ya kijiografa na utamaduni tofauti lakini kuna uchochezi wa changamoto ninyi zinazofanana. Na sisi  Baba Mtakatifu anathibitisha tunaalikwa kukaa karibu na kusaidia familia ili wajigundue zawadi ya undugu na uzuri wa kulinda upendo ambao unapyaishwa kila siku katika kushirikiana na uvumilivu, uwazi na kwa nguvu ya upole wasala. Tunaalikwa kukaa karibu mahali ambapo maisha ya familia hayakamiliki kwa mujibu wa ukamilifu wa wazo la kiinjili na haukamilishwi katika amani na furaha (Rej Esort. ap. postsin. Amoris laetitia, 5).

Kwa pamoja Baba Mtakatrifu anasema katika kuheshimu kila mmoja utamaduni wa kitasaufi, tunaweza kushirikiana katika kuhamasisha kila mantiki kitaifa na kimataifa, shughuli na mapendekezo ambayo yanatazama familia na thamani ya familia. Amehitimisha kwa kuwashukuru tena kufika kwao katika ziara hiyo na Bwana watulize na baraka zake, lakini wasisahau kusali kwa ajili yake.

Apostoliki Diakonia ni chombo mbacho kwa upande wa Sinodi Takatifu ya Kanisa Kiorthodox huko Ugiriki kinajikita katika khamasisha shughuli za kichungaji, utamaduni na uariri katika lugha ya Kigiriki. Kwa kuborehs uhusiano na Kanisa la Kiorthodox huko Ugiriki uliodumisha baada ya ziara ya Mtakatitu Yohane Paulo II huko Atene kunako 2001, imewezekakana kufanikisha baadhi ya mipango ya ushirikiano kati ya Vatican na Chombo cha Utume wa Ushemasi “Apostoliki Diakonia” la Kanisa la Ugiriki kwa ngazi ya utamaduni.

25 February 2019, 11:51