Baba Mtakatifu akihutubia washiriki wa Mkutano wa  IFAD tarehe 14 Februari 2019 Baba Mtakatifu akihutubia washiriki wa Mkutano wa IFAD tarehe 14 Februari 2019 

Papa anasema inawezakana kuwa wasanii wa uzalishaji katika maendeleo vijijini!

Baba Mtakatifu ametoa wito kwa wenye kuwa na majukumu ya kimataifa, mashirika yasiyo kiselikali,wadau wanaochangia katika sekta ya umma na binafsi ili kuendeleza mikondo ya lazima ya matendo ya dhati kwa kiwango kinachostahili kusaidia kanda za vijiji duniani na hatimaye wote waweze kuwa wasaniii wazuri wa uzalishaji kwa ajili ya maendeleo

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Nimekubali mwaliko wako Bwana Rais ambao umenielekeza kwa niaba ya Shirika la ufadhili wa maendeleo ya kilimo IFAD katika sherehe hizi za ufunguzi wa Mkutano wa 42 wa  mashirika yasiyo ya kiserikali. Ndiyo mwanzo wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 14 Februari 2019, kwenye ufunguzi wa Mkutano wa IFAD uliofanyika katika makao ya FAO mjini Roma. Akiendelea hotuba yake anasema, kufika kwake katika  makao hayo unatokana na mahitaji ya ndugu wengi ambao wanateseka duniani. Anapenda asiwaone nyuso zao nyekundu kwa maana hatimaye kilio chao kimesikilizwa, mahangaiko yao yamefikiriwa. Wao wanaishi katika hali mbaya, rasilimali zao zimekaushwa, mito imechafuliwa, ardhi imenyauka, hawana tena maji ya kutosha kwa ajili yao, hata kwa ajili ya kilimo; majengo ya vituo vya afya yanakosekana na nyumba zao ni za kutia wasiwasi na kuanguka.

Mbele yetu kuna jamii yenye uwezo wa kuendelea katika wema

Hali halisi hizi Baba Mtakatifu asisitiza  zinaonekana katika kipindi na kwa upande mwingine jamii zetu zimeweza kupata matokeo makubwa katika mantiki ya ufahamu. Hii ina maana kwamba mbele yetu kuna jamii yenye uwezo wa kuendelea kutoa mapendekezo ya wema; na itashinda hata kwa mapambano dhidi ya njaa na umasikini wa kukithiri. Kuwa na uamuzi wa dhati katika kupambana ndiyo msingi ili kuweza kusikiliza kwa dhati kilio na kusema hapatakuwapo na njaa kwa wakati ujao, bali ilikuwa ni wakati uliopita. Lakini ili kufikia  hatua hiyo ni lazima kuwapo msaada wa jumuiya ya kimataifa , jumuiya mahali ya raia  na wote ambao wanamiliki rasilimali. Wahusika wa wasivamiwe kwa kupitiwa  mmoja baada ya  mwingine badala yake wachukue wajibu wa kupata suluhisho la dhati na halisi Baba Mtakatifu ameonya.

Uwajibu wa Vatican na mashirika yanayojikita katika maendeleo ya watu

Baba Mtakatifu anasema, Vatican imekuwa daima ikiwatia moyo juhudi zilizofanywa na Shirika la kimataia kwa ajili ya kukabiliana na umasikini. Kwani hatuwezi kusahau hata Mtakatifu Paulo VI kunako mwaka 1964 alitoa wito mkubwa duniani  mjini Bombay India, pia kwa kupendekeza kwa upya katika matukio tofauti ya  kuweza kuunda mfuko ambao unawezesha binadamu kumwamasisha andokane na  mambo yote yanayomletea umasikini (Hotuba katika Mkutano wa dunia wa vyakula 9 hata yeye  hawajasita kamwe kuhamaisha kunzishwa kwa mambo hayo na moja ya hatua hiyo inayoonekana ni IFAD yenyewe. Mkutano wa 42 wa IFAD unaoendelea katika mantiki hii na mbele yake unayo kazi ya ya kushangaza na ngumu katika kuunda uwezekano wa haraka, il kuondoa kila aina ya wasiwasi na kuwaweka kila watu katika hali zao wakabiliana na mahitaji ambayo yanawasumbua. Jumuiya ya Kitaifa ambayo inaendeleza ajenda ya maendeleo endelevu ifikapo 2030 inapaswa kutimiza hatua za kufuata na za kweli katika malengo 17 waliyojiwekea. Katika pendekezo hilo, Baba Mtakatifu Francisko anasema, msaada wa IFAD unaonesha hatua ya kuweza kufuatilia kwenye malengo mawili ya kwanza ya ajenda, ikiwa ni kusitisha umasikini na mapambano dhidi ya njaa, na pia kuhamaisha uzalishaji.

Hakuna litakalo wezekana bila kuwa na maendeleo vijijini

Hakuna lolote litakalo wezekana iwapo hapatakuwapo na maendeleo vijijini, Baba Mtakatifu amebainisha na kwamba, ni maendeleo ambayo yamezungumzwa kwa kipindi kirefu, lakini hata leo hii haya jatimizwa.  Badala yeke ni kuona matokeo ambayo siyo mema kwa upande wa zaidi ya milioni 820 ya watu ambao wanateseka na chakula, utapia mlo duniani na whao wota wanaishi katika maeneo ya vijiji,na ambao wanajikita katika uzalishaji na wakati huo ni wakulima. Na zaidi wimbi la uhamiaji kutoka vijiji kwenda  mijini ni suala la dunia nzima ambalo haliwezi kudharauliwa anasema Baba Mtakatifu! Maendeleo ya maeneo mahalia kwa dhati yana thamani  kubwa japokuwa hayafanyi kazi kwa lengo linalokusudiwa. Hii ina maana ya kila mmoja, kila jumuiya inaweza kabisa kwa uwezo wake na kwa namna yake kwa kuishi maisha ya kibinadamu yenya hadhi na kuitwa jina kwa njia ya ushirikiano. Kwa maaana hiyo Baba Mtakatifu anatoa wito kwa wote wenye majukumu ya kimataifa na mashirika yasiyo kuwa ya kisekiliaka kama vile kwa wote wadau  wanaojikita kuchangia katika sekta ya umma na binafsi,ili kuendeleza mikondo ya lazima katika kujikita kwenye matendo  kwa kiwango kinachostahili katika kanda za vijiji duniani ili wote waweze kuwa wasanii na wahusika wa uzalishaji kwa ajili ya maendeleo.

Ubunifu na teknolojia vijijini iendane na utamaduni

Hatimaye Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari kwao inayotazama mada inayoongoza mkutano huo wa IFAD ambayo ni ubunifu na kuanzishwa kwa ujasiliamali katika dunia ya vijiji. Inabidi kuchuchumalia ubunifu, juu ya uwezo wa wajasiliamali na wadau wote wa sekta mahalia na upatikanaji wa mchakato wa uzalishaji kwa sababu ya kuweza kupata mabadiliko ya  vijiji, na hatimaye kuweza  kusitisha utapiamlo na kuendeleza kwa namna ya ubunifu wa mantiki ya kilimo.  Katika mantiki hiyo ni lazima kuhamasisha sayansi na dhamiri na kuweka teknolokoa ya kweli katika huduma kwa masikini. Mengineyo, teknolojia mpya haiwezi kutofungamana na utamaduni mahalia, kuwa na utambuzi wa tamaduni, lakini pia ni kufungamanisha na kutana kwa njia ya mkakati wa  pamoja. Anawatia moyo wote washiki wa Mkutano huo  na wale ambao wanajikita katika Shirika hili la IFAD kwa kazi yao na  wasiwasi wao ambao uweze kweli kuleta manufaa kwa wale ambao wamebaguliwa , ni waathirika wa sintofahamu na ubinafsi na kwamba inawezakana kuona kuona mapambano ya dhati yanafanyika ya kusitisha njiia na kuwa na haki na ustawi kwa wote.

14 February 2019, 12:44