Tafuta

Ujumbe wa Kwaresima:Kuvunjwa kwa muungano na Mungu ulisababisha kudhoofisha hata uhusiano na maelewano ya kuwa binadamu na mazingira ambamo tunaishi Ujumbe wa Kwaresima:Kuvunjwa kwa muungano na Mungu ulisababisha kudhoofisha hata uhusiano na maelewano ya kuwa binadamu na mazingira ambamo tunaishi 

Ujumbe wa Papa wa Kwaresima:Maana kwa matumaini sisi tumekombolewa!

Katika fursa ya maandalizi ya kipindi cha Kwaresima 2019 Baba Mtakatifu ametoa ujumbe kuwa tusiache kipindi hiki mwafaka kipite hivi hivi! Tuombe Mungu atusaidie kujikita kwenye matendo ya dhati katika safari ya kweli ya uongofu.Tuache ubinafsi,mtazamo juu yetu binafsi kwa kutazamia Pasaka ya Yesu na tuwe karibu na ndugu wenye matatizo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kila mwaka Mungu anatoa fursa kwa waamini wake kwa njia ya mama Kanisa kujiandaa kwa furaha, kutakasika katika roho ili kuweza kuadhimisha Pasaka kwa sababu ya kuchota kutoka katika fumbo la wokovu ule  ukamilifu wa maisha mapya katika Kristo, (kutoka katika sala ya kweresima) kwa mtindo huo tunaweza kutembea, Pasaka baada ya Pasaka kuelekea katika utimililifu wa wokovu ambao tayari tumeupokea kwa neema ya fumbo la Pasaka katika Kristo. “Maana kwa matumaini sisi tumekombolewa” (Rm 8,24). Fumbo hili ambalo tayari linafanya kazi ndani mwetu, katika maisha hapa duniani ni mchakato unaoendelea na ambao unaunganisha hata historia na kila kiumbe. Mtakatifu Paulo alifikia kusema:“Viumbe vyote vinangojea kwa hamu Mungu awadhihirishe watoto wake”(Rm 8,19). Ni katika mantiki hiyo ninapenda kuchota katika kitovu hicho cha tafakari ambayo iweze kutusikindikiza katika safari ya uongofu katika kipindi cha kwaresima. Ndiyo mwanzo wa ujumbe wa  Baba Mtakatifu Francisko  wa kwaresima kwa  2019 kwa waamini wote ili kuweza kujiandaa vema katika  mchakato wa safari ya uongofu. Ujumbe wake unaongozwa mada  Maana kwa matumaini sisi tumekombolewa, mada inayotoka katika  Somo la  Mtakatifu Paulo kwa Warumi (Rm 8,19). Ni ujumbe ambao uliandikwa tarehe 4 Oktoba 2018 katika Sikukuu ya Mtakatifu Francis wa Assisi.

Wokovu wa uumbaji:Maadhimisho ya Siku Kuu tatu za Pasaka ya mateso kifo na ufufuko wa Kristo

Baba Mtakatifu anasema kuwa,maadhimisho ya Siku Kuu Tatu za Pasaka, mateso kifo na ufufuko wa Kristo, unahitimishwa na mwaka wa kiliturujia ambao unatualika kila mara kuishi katika  mchakato wa maandalizi, kwa kuwa na  utambuzi wa kujifananisha na Kristo (Rm,8,29) kwamba ni zawadi isiyokadirika ya huruma ya Mungu. Iwapo binadamu anaishi kama mtoto wa Mungu na anaishi kama mtu aliyekombolewa na kuacha aongozwe na Roho Mtakatifu (Rm 8,14) anatambua na kuweka matendo ya sheria ya Mungu, kuanzia na ile iliyoandikwa katika moyo wake na katika asili, yeye anafanya wema, hata ya uumbaji katika kushirikishana na wokovu wake. Kwa maana hiyo kazi ya uumbanji anasema Mtakatifu Paulo ina shauku ya kina ambayo inajionesha kama wana wa Mungu, yaani wale ambao wanafaidika katika neema ya fumbo la Pasaka ya Yesu na wanaishi kwa utimilifu wa matunda ambayo yanatakiwa yafikie ukomavu wao wa  wokovu wa mwili wa binadamu mwenyewe. Iwapo upendo wa Kristo unabadili maisha ya watakatifu, katika roho,moyo na mwili. Mambo haya yanatoa sifa kwa Mungu na kwa sala, kutafakari kwa kujihusisha katika hilo hata kiumbe kama inavyo jionesha kiajabu kwenye wimbo wa sifa ya ndugu jua wa Mtakatifu Francis wa Assisi (Rej Enc. Laudato Si, 87). Lakini kwa namna hiyo maelewano yatokanayo na wokovu ni bado na daima yako hatarini kutokana na  nguvu hasi ya dhambi na kifo.

Nguvu haribifu ya dhambi:kuna mantiki ya kutaka kuwa na kila kitu na kwa haraka

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea kutafakati dhambi  anasema, kwa dhati tunaishi kama vile siyo watoto wa Mungu, mara nyingi tunakuwa na tabia  haribifu kwa jirani hata kwa viumbe wengine, lakini hata sisi wenyewe, kwa kudai zaidi au kiasi cha kuzidi kufanya matumizi ya upendo wetu binafsi.  Ukosefu wa kadiri unachukua nafasi na kutuingiza katika mtindo wa maisha ambayo yanakiuka vizingiti ambavyo katika maisha ya kibinadamu na asili vinataka kuheshimiwa, kwa kufuata shauku ambazo haziwezi kuthibitiwa na ambazo zinafafanuliwa katika kitabu cha Hekima kuwa ni waovu hasa wale ambao hawaoni Mungu kama mfano katika matendo yao, na wala kuwa na matumaini ya wakati endelevu ( Rej Hek 2,1-11). Iwapo hatuna matumaini ya kuelekea katika Pasaka, kuelekea katika upeo wa ufufuko ni wazi kwamba tunaingiliwa na mantiki ya kutaka kuwa na kila kitu na kwa haraka, kuwa nacho cha zaidi na kuishia kulazimisha.

Baba Mtakatifu anaongeza kusema kuwa, sababu ya kila ubaya tunaitambua kuwa ni dhambi ambayo tangu kuonea kwake katikati ya watu iliondoa muungano na Mungu na wengine na uumbaji ambamo sisi sote tumeunganika awali ya yote kwa njia ya mwili wetu. Kuvunjwa kwa muungano na Mungu ulisababisha kudhoofisha hata uhusiano na maelewano ya kuwa binadamu na mazingira ambamo tunaitwa kuishi na ambamo katika bustani ilibadilishwa kuwa jangwa ( Yer 3,17-18). Hii ina maana ya ile dhambi ambayo inapelekea mtu kujifanya muungu wa uumbaji na kuhisi kama mkuu kabisa na kuitumia, si kwa ajili ya matakwa ya muumba, bali kwa ajili ya matakwa yake binafsi na kwa madhara ya  viumbe na wengine. Inapotokea kuacha sheria ya Mungu sheria ya upendo inashia kuthibitisha sheri ya nguvu dhidi ya wadhaifu, Baba Mtakatifu anathibitisha! Dhambi ambayo inaishi ndani ya moyo wa mtu (Mk 7,20-23) na inajionesha kwa jinsi gani  uchoyo wa kurarua ustawi, kutojali ustawi wa wengine na mara nyingi hata watu wake na kupelekea unyonyaji katika kazi ya uumbaji, watu na mazingira, kwa mujibu wa tamaa mbaya isiyotosheka na ambayo inadai kila shauku ya haki na wakati mwisho wake ataishia kuharibika hata kwa yule anayemiliki.

Nguvu inayookoa kwa njia ya maungamo na msamaha

Kwa maana hiyo kazi ya uumbaji  Baba Mtakatifu Francisko anasema ina ulazima wa kuwa na wito ambao unajionesha kwa wana wa Mungu na wale ambao wamekuwa “viumbe wapya”Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita hali mpya imefika (2 Cor 5,17). Kwa hakika pamoja na maonesho hayo hata kazi ya uumbaji inaweza kufanya Pasaka: kujifungulia mbingu mpya na nchi mpya (rej Uf 21,1). Na katika safari ya kuelekea Pasaka inatakiwa kukarabatiwa uso wetu na mioyo ya kikristo kwa njia ya toba, uongofu na msamaha, ili kuweza kuishi utajiri wote wa neema ya fumbo la pasaka.

Mambo muhimu katika safari ya kwaresima ni kufunga,sala na sadaka

Ni muhimu kuwa na uvumilivu na ndiyo hata matarajio  ya  kazi ya uumbaji ambayo yatakuta ukamilifu iwapo kuwakuwa na maonesho ya wana wa Mungu, yaani waamini  wakristo  watakapoingia kwa maamuzi katika uchungu huo ambao ndiyo uongofu. Kazi yote ya  uumbaji inaalikwa pamoja na sisi kutoka katika utumwa wa uharibifu ili kushiriki uhuru mtukufu wa watoto wa Mungu ( Rm 8,21). Kwaresima ni ishara ya sakramenti ya uongofu huu. Na hiyo inawaalika wakristo kutafakari na kwa dhati fumbo la Pasaka katika maisha yao binafsi, familia na kijamii kwa namna ya pekee kwa njia ya kufunga, sala na kutoa sadaka.

Kufunga:maana yake ni kujifunza kubadili mienendo yetu dhidi ya wengine na viumbe. Kutoka katika kishawishi ambacho kinapendelea kurarua kila kitu ili kujishibisha urafi wetu, na badala yake kuwa na  uwezo wa kuteseka kwa ajili ya upendo na ambao unaweza kutuliza utupu wa moyo wetu. Kusali ili kujua namna ya kujikana na miungu na umimi ili  kuthibitisha mahitaji ya Bwana na huruma yake. Kutoa sadaka ili kuweza kuepuka kuishi upendeleo wetu katika kukusanya kila kitu kwa ajili yetu binafsi, kuwa na udanganyifu wa kuwa na uhakika wa ujao na ambao haupo mikononi mwetu. Kufanya hivyo ili kuweza kupata furaha ya mpango wa Mungu ambao ameuweka katika uumbaji na katika mioyoni mwetu, ni ile njia ya kupenda kama Yeye, ndugu zetu, ulimwengu na ili kuweza kupata upendo wa kweli na wa furaha.

Kwaresima ya Mwana wa Mungu ilikuwa ni kuingia katika jangwa la uumbaji ili kufanya urudie  kuwa bustani

Baba Mtakatifu Francisko anasema kwaresima ya Mwana wa Mungu ilikuwa ni kuingia katika jangwa ya uumbaj ili kufanya irudie kuwa bustani ya muungano na Mungu kama ilivyokuwapo kabla ya dhambi ya asili (rej Mk 1,12-13: Is 51,3). Kwaresima yetu iwe ya kutembea katika safari hiyo kwa kupeleka matumaini ya Kristo hata kwa viumbe ambavyo vitakombolewa kutoka katika utumwa wa uharibifu ili kushiriki uhuru mtukufu wa watoto wa Mungu ( rej Rm 8,21). Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu anatoa angalisho kuwa:tusiache kipindi hiki mwafaka kipite hivi hivi! Tuombe Mungu atusaidie kujikita kwenye matendo ya dhati katika safari ya kweli ya uongofu. Tuache ubinafsi,yaani mtazamo juu yetu binafsi na kutazamia Pasaka ya Yesu; tuwe karibu na ndugu, kaka na dada wenye matatizo, kushirikishana nao mali zetu kiroho na kimwili. Kwa kufanya hivyo tutaweza kupokea kwa dhati maisha na ushindi wa Kristo dhidi ya dhambi na dhidi ya kifo na tutaweza kuipatia hata kazi ya uumbaji nguvu yake ya kubadilisha.

KWARESIMA 2019

 

26 February 2019, 12:05