Baba Mtakatifu wakati wa kubariki waamini mara baada ya katekesi yake kuhusu sala ya Baba Yetu Baba Mtakatifu wakati wa kubariki waamini mara baada ya katekesi yake kuhusu sala ya Baba Yetu 

Papa anahimiza tuige mfano wa Watakatifu Syril na Methodius katika uinjilishaji!

Katika salam zake Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Tafakari ya Katekesi amewakumbusha kuwa tarehe 14 Februari ni siku kuu ya Watakatifu Syril na Methodius wainjilishaji wa Ulaya ya Mashariki na wasimamizi wa Ulaya.Kwa kuiga mfano wao,watusaidia wote kila mazingira kugeuka maisha,wafuasi na wamisionari wa uongofu wa mbali na karibu

Na Sr. Angela Rwezaula - Vartican

Baba Mtakatifu katika salam zake za mwisho mara baada ya tafakari ya Katekesi tarehe 13 Februari 2019 katika ukumbi wa Papa Paulo VI mjini Vatican, amewashukuru watu wa asilia ambao wamemletea zawadi ya stola iliyotengenezwa na wanawake asilia wa utumaduni mkubwa kutoka kabila la Wichi, barani Amerika ya Kusini, hata kuwasalimia watu wengine ambao walikuwapo katika makundi wakionekana wanapeperusha bendera za Panama wiki chache baada ya siku ya vijana duniani!

Aidha amewasalia mahujaji kwa lugha ya kiarabu kutoka Siria,Lebanon na nchi zote za Mashariki akikumbusha kuwa, leo hii  bado kuna ndugu na kaka na dada  duniani wanaoteseka na wako mbali wanahitaji tufanye kazi kwa ajili yao na mambao tunawakumbuka katika sala.

Vile vile amewasalimia waandishi wa habari wa Askanews ambao wanapitia kipindi kigumu cha matatizo na ambapo pia amekumbush mahijaji na waamini wote  kuwa tarehe 14 Februari, ni Siku Kuu ya Mtakatifu Syril na Methodius wainjilishaji wa watu wa Slovakia na wasimamizi wa Ulaya. Kwa kuiga mfano wao, watusaidia watu wote kila mazingira kugeuka maisha, wafuasi na wamisionari wa uongofu wa mbali na ule wa karibu. Upendo wao kwa Bwana utupatie nguvu ili kustahimili kila sadaka, na ili Injili iweze kuwa sheria msingi wa maisha yetu.

 

13 February 2019, 14:52