Tafuta

Vatican News
Misa ya Baba Mtakatifu huko Sacrofano Roma Ijumaa tarehe 15 Februari 2019 Misa ya Baba Mtakatifu huko Sacrofano Roma Ijumaa tarehe 15 Februari 2019  (Vatican Media)

Papa:Tushinde hofu dhidi ya wageni ili tukombolewe na Bwana!

Kushinda hofu na kuwakaribisha wengine,wenye njaa,kiu,wageni,wagonjwa na wafungwa ni neema ambayo inapelekea utume.Ni tunda la kujiaminisha moja kwa moja kwa Bwana na ambaye kwetu sisi ni wokovu pekee wa kweli

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Utajiri wa masomo yaliyochaguliwa katika maadhimisho haya ya ekaristi takatifu yanaweza kusemwa kwa ufupi neno moja: msiogope. Somo kutoka Kitabu cha Kutoka limeonesha waisraeli wakipitia Bahari ya shamu kwa hofu kubwa  kutokana na majeshi ya Farao kuwafuata na linawakaribia. Na wengi walikuwa wanafikiri ni bora wangebaki Misri na kuendelea kuishi kama watumwa kuliko kufa katika jangwa. Lakini Musa anawambia watu wasiwe na hofu kwa sababu Bwana yuko nao. Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo (Kut 14,13). Safari ndefu ya na ya lazima kupitia jangawani ili kufikia nchi ya ahadi  inaanza na majaribu makubwa. Isareli inaalikwa kutazama zaidi ya upeo masumbuko ya wakati  huo na kushinda hofu  kwa kuwa na matumaini makubwa kwa matendo ya wokovu na fumbo la Bwana. Ndiyo mwanzo wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 15 Februari 2019 jioni masaa ya Ulaya wakati wa kuadhimisha misa takatifu kwa washiriki wa Mkutano katika  Jumuiya ya Domus huko Sacrofano, Roma.

Hiyo ni  misa ya  ufunguzi rasmi wa Mkutano unaojikita kutazama hali halisi ya sasa kwa kuongoza na mada ya  mapokezi huru dhidi ya hofu. Ni mkutano ulioandaliwa na Chama cha Migrantes, Caritas ya Italia na Kituo cha Astalli katika Mkutano wa  siku mbili kuanzia tarehe 15 -17 Februari 2019. Ziara hii ilikuwa na  tabia ya kifaragha kwa washiriki hao tu.

Mitume wanabaki na wameshangaa na kupiga kelele

Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri yake anasema  katika sura za Injili ya Matayo (14,22 -33) mitume walibaki wakifadhaika na wakapiga yowe kwa hofu. Baada ya kumwaona Mwalimu aliyekuwa akitembe juu ya maji,wakifikiri ni kivuli. Katika mtumbi ulikuwa unalea kwa nguvu kutokana na upepo na hawakuwa na uwezo wa kumtambua Yesu, lakini mara  moja yeye aliwahakikishia:Jipeni moyo ni mimi; msiogope. Petro kwa mchanganyo wa mawazo akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. Na Yesu akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. Mara Yesu akanyosha mkono wake,akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? (Mt 14-27- 31).

Kwa sababu ya hofu ya watu nguvu ya dikteta uongezeka

Kufutia na matukio haya ya kibiblia, Bababa Mtakatifu Francisko anathibitisha kwamba, hata leo hii Bwana anazungumza nasi na kutuomba kujiachia kwake ili aweze kutukomboa na hofu zetu. Kuwa huru na woga ndiyo mada uliyochaguliwa kuongoza mkutano wao yaani Huru dhidi ya hofu. Hofu ni asili ya utumwa anabainisha Baba Mtakatifu na kwamba, Waisraeli waliendelea kuwa watumwa kwa sababu ya hofu. Vile vile ni asili ya kila udikteta, kwa sababu watu ya hofu ya watu, nguvu ya madikteta uongezeka. Mbele ya ukatili na ubaya wa  nyakati zetu, hata sisi kama watu wa Israeli tunashawishika kuacha ndoto za kuwa na uhuru, Baba Mtakatifu Francisko anabainisha na kwamba tunazidi kukandamizwa na woga mbele ya hali ambayo utafikiri hakuna hata njia ya kupitia. Vile vile haitoshi maneno ya mtu anayeongoza au nabii anayetoa uhakika, iwapo hatuhisi uwepo wa Mungu na hatuna uwezo wa kujikabidhi moja kwa moja katika wema wake. Kwa namna hiyo tunajifungia sisi binadamu katika udhaifu wa uhakika wa kibinadamu, katika mzunguko wa watu ambao wanawapenda, katika mambo yetu ya kila siku. Lakini mwisho wa nikukataa safari ya kuelekea katika Nchi ya ahadi kwa kutamani kurudi  utumwani huko Misri.

Kukataa kukutana siyo ubinadamu

Aidha  Baba Mtakatifu anabainisha kwamba, kujikunja kwa namna ya ubinafsi ni ishara ya kushindwa, ya kukua kwa hofu zetu kwa watu wengine, ambao hawajulikani, waliobaguliwa  na ambapo ni wageni  ambao ndiyo wenye kupendelewa na Bwana kwa mujibu wa Injli ya Mtakatifu Matayo sura ya 25.  Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa  hayo yote yanaonekna kwa namna ya pekee leo hii mbele ya wahamiaji na wakimbizi ambao wanabisha hodi katika milango yetu wakitafuta ulinzi, usalama na wakati endelevu ulio bora. Ni kweli kabisa hofu ni sheria, kwa sababu pia kuna ukosefu wa maandalizi ya kukutana huko. Na katika hili pia Baba Mtakatifu amekumbusha alivyozungumzia hilo mwaka jana wakati wa fursa ya Siku ya wahamiaji na wakimbizi duniani kwamba: “siyo rahisi kuingia katika utumaduni wa mwingine, kuvaa utu wake tofauti na wetu, kutambua mawazo na uzoefu. Na ndiyo maana mara nyingi tunakataa kukutana na mwingine na kuweka vizingiti ili kujilinda! Kukataa kukutana siyo jambo la kibinadamu, Baba Mtakatifu amekazia!

Badala yake tunaalikwa kuishinda hofu na kujifungulia makutano. Kwa kufanya hivyo haitoshi kutafuta sababu na kuhesabu  na takwimu. Musa aliwambia watu mbele ya Bahari ya Shamu wakiwa na adui wa vita aliyekuwa nyuma ya mabega yao akiwafuata: Msiogope kwa sababu Bwana hawaachi watu wake bali anatenda kimaajabu katika historia ili kutimiza mpango wake wa wokovu. Musa alizungumza hivyo kwa sababu alikuwa anamwamini Mungu. Kukutana na mwingine pia ni kukutana na Kristo.Yeye mwenyewa alitueleza. Ni yeye anayebisha hodi katika milango yetu akiwa na njaa, kiu, mgeni, uchi, na mfungwa akiomba akutane na kusaidiwa. Na iwapo bado kuna wasi wasi, Baba Mtakatifu Francisko amethibitisha kwa maneno wazi ya Yesu:Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi(Mt 25,40).

Inaweza kueleweka maana hiyo ya kutiwa moyo na Mwalimu kwa wafuasi wake: Jipeni moyo ni mimi; msiogope. Mt 14,27). Baba Mtakatifu anaendelea ksema: Ni kweli ni yeye hata kama macho yetu yanashindwa kutambua katika nguo zilizochanika, miguu iliyo michafu, uso usiotambulika, mwili uliojeruhiwa, asiyekuwa na uwezo wa kuzungumza lugha yetu… Hata sisi kama Petro tunawza kuwa na kishawishi cha kumjaribu Yesu kwa kumwomba ishara. Labda baada ya hatua chache za wasiwasi juu yake na kubaki waathiriki kwa upya wa hofu, lakini Bwana hatuachi! Baba Mtakatifu anathibitisha. Hata kama sisi ni wanaume na wanawake wenye imani haba, Kristo anaendelea kunyosha mikono yake ili kutuokoa na kutufanya tukutane na Yeye katika mkutano ambao unatuokoa na kuturidishia furaha ya kuwa wafuasi wake.

Kama somo hili ni ufunguo wa historia basi ni kuanza upya kukaribisha na kupokea

Na kama huu ni ufunguo unaofaa wa somo la historia ya leo, Baba Mtakatifu anafafanua kuwa basi tunatakiwa kuanza kushukuru kwa yule anayetupatia  fursa ya mkutano huo, hata kwa wengine ambao wanabisha hodi katika milango yetu na kutoa uwezekano wa kushinda hofu zetu, ili kukutana, kukaribisha na kumsaidia Yesu kupitia mtu.Vile vile na ambaye amependa kwa nguvu zote kuacha akombolewe dhidi ya hofu, aliyefanya uzoefu wa furaha ya kukutana, leo hii anaalikwa kutangaza juu ya paa, kwa uwazi ili kuwasaidia wengine waweze kuwa tayari kujikita katika makutano na wokovu wake Yesu. Kwa kuhitimisha amethibitisha kwamba hii ni neema ambayo inapelekea katika utume, tunda la kujiaminisha moja kwa moja kwa Bwana na ambaye kwetu sisi ndiyo wokovi pekee wa kweli. Kwa maana hiyo kama mtu binafsi na kama jumuiya, wote tunaalikwa kufanya maombi ya watu waliokombolewa kwamba: Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. (Kut 15,2).

16 February 2019, 09:03