Cerca

Vatican News
Papa amekutana na wawakilishi 38 kutoka makabila 31 tofauti ya watu  asilia wa Amerika ya Kusini,Asia,Afrika na maeneo ya pasifiki katika mkutano wa IFAD,mjini Roma Papa amekutana na wawakilishi 38 kutoka makabila 31 tofauti ya watu asilia wa Amerika ya Kusini,Asia,Afrika na maeneo ya pasifiki katika mkutano wa IFAD,mjini Roma  (ANSA)

Papa anakazia umuhimu wa utunzaji wa mazingira katika sayari hii

Hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko katika Mkutano wa IV wa Muungano wa Jukwaa za watu asilia duniani,uliotishwa na IFAD tarehe 14 Februari 2019.Katika hotuba yake anaonesha umuhimu wa kuongeza nguvukatika mikono ili kuwakimbilia leo hii wanaohitaji msaada na kufungua milango ya kesho kwa ajili ya kizazi kitakacho fuata baada yetu

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Baba Mtakatifu Francisko akianza hotuba yake katika Mkutano wa IV wa Muungano wa Jukwaa za watu asilia, dunainia uliotishwa na IFAD tarehe 14 Februari 2019 amshukuru Bi Myrna Cunningham kwa maneno yake na kuwasalimia washiriki wote Mkutano huo wa Baraza la Ifad kwa kuongozwa na mada ya kuhamasisha fahamu na ubunifu wa watu asilia katika kuunda umoja wa kuweza kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo endelevu.

Uwepo wao hapo Baba Mtakatifu amethibitisha ni kuonesha kuwa masuala ya mazingira ni muhimu sana na kuwaalika kuwa upya wawe  na umakini wa mtazamo wa sayari yetu ambayo imejaruhiwa katika kanda nyingi kwa sababu ya tamaa ya kibinadamu na migogoro ya silaha ambayo inasababisha mambe mengi mabaya mengi,kama ulivyo hata majanga ya asili ambayo yanawaacha bila upeo kwa sababu ya madhara yake. Kwa kusisitiza, Baba Mtakatifu anasema haiwezekani kuendelea kudharau majanga hayo kwa kutoa jibu la sintofahamu na ukosefu wa mshikamano, au kusubiri tena vipimo vya kuweza kukabiliana kwa namna ya ya dhati. Kinyume chake inahitaji nguvu hai ya kindungu ambayo itaongeza nguvu mikono yetu ili kuweza kuwakimbilia leo hii wanaohitaji msaada na kufungua milango ya kesho kwa ajili ya kizazi kitakacho fuata baada yetu.

Mungu aliumba ardhi kwa ajili ya faida ya wote, ili iweze kuwa nafasi ya kupokeana, na  hakuna yoyote aweze kuhisi amebaguliwa,pia wote waweze kupata nyumba. Sayari yetu ni tajiri ya rasilimali nyingi za asili. Na watu asilia kwa utajiri wao wa lugha, utamaduni, mila, fahamu na mitindo ya mababu, iweze kuwa kengele ya dharura kwa watu na kuonesha uwazi kwamba mali asilia siyo mali yakumilikiwa binafsi na  binadamu bali ni kwa ajili ya wale ambao wamepewa kuitunza na kama wito wa kuilinda  ili isipoteze uoto wake na maji yaweze kuendelea kuwa safi na salama, hewa nzuri na misitu ya kupendeza na ardhi yenye rutuba.

Baba Mtakatifu amerudia kuwashukuru shirika la IFAD kwa maana wanaendelea kujikita kutambua sauti ya kilio, kwa kuheshimu mazingira ambayo wao wanalinda. Aidha anasema uzoefu wa IFAD na ufundi wake kama vile hata zana wanazosiweka ni moja ya tunu msingi katika huduma ya kuendeleza mchakato wa safari ya kuwa na utambuzi ambao unapelekea katika  maendeleo ya kiteknolojia na kiuchumi  (Laudato si’ n. 194). Anwatia moyo wa kuendelea mbele akiomba Mungu ili asichoke kuwasindikiza kwa baraka jumuiya zao na zile za IFAD ,wafanye kazi vema na kuwalinda wale wote wanaoishi vijijini pia maskini wa sayari.

14 February 2019, 15:00