Tafuta

Papa Francisko Papa Francisko 

Papa:haiwezekani kukabidhi maisha katika mantiki ya kiufundi

Papa amekutana na wawakilishi wa Baraza la Kipapa la Maisha wakiwa wanafungua Mkutano wa Mwaka unaongozwa na Mada ya Kanuni maadili kuhusu matumizi ya Roboti:Watu,mashine na Afya.Onyo ni kwamba haki za kibinadamu ziwe ndiyo ardhi katika utafiti wa maadili duniani

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 25 Februari 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Maisha na kumshukuru Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, Rais wa Baraza la Kipapa la Maisha kwa maneno ya hotuba yake. Mkutano huo umewadia wakati wa kusheherekea Jubilei ya kwanza ya Baraza la Kipapa la Maisha kwa miaka 25 tangu kuundwa kwake. Baba Mtakatifu anakumbusha kuwa katika fursa ya siku hiyo alimtumia Rais wa Baraza la Kapapa la Maisha  mwezi uliopita  barua iliyokuwa na mada ya  Humana Communitas. Baba Mtakatifu anaonesha maana ya kile ambacho kilimfanya aandike ujumbe huo kwamba, hawali ya yote ilikuwa ni kuwashukuru Marais wote ambao wamejikita kuongoza kwa pamoja Baraza la Maisha na wajumbe wote kwa huduma ya kazi na jitihada zao kwa ukarimu katika kulinda na kuhamasisha maisha ya binadamu katika shughuli ya miaka 25. Baba Mtakatifu anathitisha kwa jinsi gani kuna haja ya kuwa na utambuzi wa Dunia inayoendelea kujibamiza. Kiungo cha uhusiano wa familia na jamii utafikiri kinaharibika  na kuwa na tabia ya kujiingiza ndani mwake na matakwa yake binafsi na kuona matokeo yake  katika masuala na wakati wake endelevu ( Barua Humana communitas 2). https://www.vaticannews.va/sw/pope/news/2019-01/papa-kanisa-litoa-nguvu-ya-ubinadamu-wa-maisha.html

Dunia inajiwakilisha katika kipeo hicho kikubwa hasa cha binadamu anapokuwa na uwezo wa kusayansi na kiufundi kwa kuweza kuwa na ustawi endelevu  kwa mujibu wa mpaji ya  Mungu lakini badala yake, tunatazama migogoro isiyo elezeka na kukua kwa ukosefu wa usawa. Kipindi cha mwanga wa maendeleo na udhaifu ambao unasababishwa na sayansi na ufundi, vimesabababisha matokeo yasiyo tarajiwa. Kwa upande mwingine kwa hakika, maendeleo ya teknolojia imetuwezesha kutatua matatizo hadi miaka michache iliyopita  na tunashukuru kwa watafiti ambao  walitoa matokeo hayo; na kwa upande mwingine Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, kumetokea matatizo na hatari ambazo wakati mwingine ni vigumu zaidi ya zile za mwanzo. Uwezekano  huo una hatarisha na kuweka  giza kwa yule anaye fanya na kwa ajili ya yule anayefanyiwa 

Mfumo wa kiteknolojia ambao unajikita katika mantiki hai ya  kujitosheleza haitoi jibu la kina kwa maswali ambayo binadamu anajiuliza; iwapo kwa upande mwingine haiwezekani kufanya lolote labda kwa rasilimali zake, kwa upande mwingine  inajiwekea mantiki kwa yule anayetumia . Na wakati huo  hu ufundi ni tabia ya ubinadamu.  Na hivyo haiwezi kueleweka  kama vile ni nguvu ambayo haijulikani  au mtindo, bali ni uzalishaji wa kazi yake kwa njia ya kutazama dharura ya kuishi kwa ajili yake na wengine. Kwa maana hiyo ni mtindo maalum wa kibinadamu wa kuishi katika dunia. Hata hivyo leo hii mapinduzi ya uwezo wa kiufundi yanazalisha hatari, baba Mtakatifu amesema na kwamba, badala ya kutoa maisha ya kibinadamu kama zana ya kuboreha kwa tiba, inakuwa hatari ya kubadilisha maisha katika mantiki yak ile ambacho kinaondoa maamuzi ya thamani. Mabadiliko hayo yanatokana na mashine na si vizingiti vya kujiongoza peke yake bali kuelezea namna ya kungoza mtu. Sababu ya kibiadamu inabadilika kuwa ya kujuu juu na siyo kufikiria hadhi ya kuwa binadamu.

Haiwezekani kukabidhi maisha katika mantiki ya kiufundi: Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba ni kwa bahati mbaya majanga hayo yanajionesha katika sayari na nyumba  yetu uwazi wa vyombo vya kiufundi. Kwa maana hiyo, maadili ya kutumia Roboti duniani ni jambo moja muhimu la kuzingatia. Ni suala ambalo linaeleza kuwa na utambuzi wa kina na kwa  namna ya mantiki ya mazingira kijamii na juu ya afya na juu ya maisha.  Hili ni suala ambalo linakwenda pamoja  na kufanana sana na ekolojia fungamani ambayo inajieleza na kuhamasishwa na Laudato Si. Na zaidi, katika ulimwengu wa sasa, Baba Mtakatifu anaongeza kusema imekumbwa na mwingiliano kati ya  tamaduni tofauti, na inapaswa kupeleka mchango maalumu kwa waamini katika utafiti wa mantiki ya kazi ya kushirikishana kiulimwengu na ambayo iwe ndiyo kiongozi wa pamoja kwa ajili ya uchaguzi wa yule anayepswa kuwajibika na maamuzo na kuchukua uwajibikaji katika mpango wa kitaifa na kimataifa.

Haki za binadamu ziwe ndiyo ardhi katika utafiti wa kisayansi wa maadili duniani: Hii ina maana ya kujihusisha katika mazungumzo ambayo yanatazama haki za binadamu na kuweka mwanga ulio wazi na uwajibu wake katika utafiti. Ni suala la kujihusisha katika uwanja wa utafiti wa pamoja wa maadili duniani kwa namna kupata na kujiuliza tamaduni ambazo zinapaswa zichote urithi wa sheria ya kawaida na ambayo  ni asili.  Katika barua ya Humana Communits, Baba Mtakatifu anakumbusha juu ya mada ya teknolojia iliyopo na inayowezekana.  Kuna uwezekano wa kuingilia ukuu wa dhana hai na kawaida ya ukuu wa udogo ambao unapaswa kushirikishana katika mafunzo daima. Hadhi ya  kila binadamu, lazima ipewe kipaumbele cha tafakari na kila aina ya matendo ya kweli. Ni lazima kutambua vema nini maana ya mantiki hiyo, ya kiakili na kidhamiri, hisia, sababu ya upendo na matendo ya kimaadili na kujitosheleza. Vyombo kama  mashine na ambavyo vinasaidia uwezo wa kibinadamu kwa dhati vina ukosefu wa ubora wa ubinadamu.

Ni lazima kuzingatia maelekezo na sheria yake, katika utafiti wenyewe ili kuelekea uundaji sawa kati  ya kuwa binadamu na zaidi katika toleo la sasa za roboti. Mambo hayo kwa hakika Baba Mtakatifu Francisko anasema yanajichanganya katika dunia yetu na kujibadili kwa kina katika maisha yetu. Iwapo tutatambua kutoa dhamani ya  matukio haya, nguvu maalumu ya mambo haya mapya yanawezekana  kuanzsisha mantiki moya kwa kila mt una binadamu fungamani. Mjadala kati ya wataalam wenyewe inaonesha tayari matatizo makubwa ya kuongoza mwenedendo wake katika kufanya kazi kwa kiasi kikubwa kutoa data kamili. Kama vile inavyotoa  maswali mengi ya kujiuliza juu ya  maadili ya kiteknolojia na  juu ya viumbe na kufanya kazi ya ubongo, kwa kila kesi na kujaribu kueleza kila kitu. Akili ya binadamu katika mfumo wake na sehemu zote za kiakili na kimwli lazima kuzingatia dharura ya matukio ya uzoefu na dhamiri. Matukio ya binadamu yanaelekeza na matokeo ya ufafanisho wa kuhesabu kila kiungo. Na wakati huo huo mantiki hiyo inachukuliwa kwa kina kwa mujibu ambao kila kitu ni cha hali ya juu katika kila sehemu (cfr Esort. ap. Evangelii gaudium, 234-237).

Kuanzia tatehe 25 -27 Februari mjini Vatican katika ukumbi mpya wa Sinodi, unafanyika Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Maisha. Mkutano huo unaongozwa na Mada ya Kanuni maadili kuhusu matumizi ya Roboti:Watu,mashine na Afya. Tukio hili liliwakilishwa kwa vyombo vya habari tarehe 15 Januari 2019. Hata hivyo katika Mkutano huo mkuu tarehe 25 na 26 mkutano umefunguliwa hata kwa umma. Tarehe 25 Mchana mkutano unatazamia kujikita juu ya tofauti za utafiti. Sehemu ya pili tarehe 26 Februari asubuhi, watajikita  kutazama jamii na elimu ya binadamu na kwa jinsi gani  roboti ilivyoabidili utambuzi na uelewa katika dunia, mahusianio na uelewa wa kuishi kijamii. Sehemu ya tatu mchana tarehe 26 mkutano mkuu utajikita kuangalia matumizi ya kimaadili katika sekta ya afya. Kazi ya Mkutano wa mwaka  2019 inaunganisha pamoja utakaofayika mwaka  2020 kuhusu akili bandia Mantiki hizi mbili za roboti na akili bandia zinatofautiana, lakini wakati huo huo zinaunganika pamoja kwa sababu zinashirikishana mantiki, maendeleo ya kiteknolojia na matumizi ya maadili.

25 February 2019, 13:06