Cerca

Vatican News
Papa Francisko ametembelea Kanisa kuu la Mtakatifu Yosefu, Abu Dhabi na kuwashukuru waamini kwa ushuhuda wa imani yao kwa Kristo na Kanisa lake. Papa Francisko ametembelea Kanisa kuu la Mtakatifu Yosefu, Abu Dhabi na kuwashukuru waamini kwa ushuhuda wa imani yao kwa Kristo na Kanisa lake.  (© Vatican Media)

Papa Francisko atembelea Kanisa kuu la S. Joseph, Abu Dhabi!

Kanisani hapo amelakiwa na waamini zaidi ya 300 waliokuwa na furaha kubwa kukutana na kuzungumza na Khalifa wa Mtakatifu Petro. Baba Mtakatifu amesema, inafurahisha na kutia moyo kutembelea na kusali katika Makanisa machanga duniani. Ametumia fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza waamini kwa ushuhuda wa tunu msingi za Kiinjili huko Uarabuni.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne, tarehe 5 Februari 2019, kabla ya kuhitimisha hija yake ya kitume huko Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu, alipata nafasi ya kukutana na kuagana na wafanyakazi wanaotekeleza utume wao katika Jumba la Mushrif. Wafanyakazi, wakleri, ndugu na jamaa zao walikuwa wameambatana na Askofu mkuu Francisco Montecillo Padilla, Balozi wa Vatican kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu, Kuwait, Guba ya Uajemi, Bahrain, Qatar na Yemen. Katika tukio hili hadhimu, Askofu Paul Hinder amehudhuria pia.

Baba Mtakatifu Francisko kabla ya kuanza kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu, alipata nafasi ya kutembelea na kusali kwa kitambo kidogo kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Yosefu huko Abu Dhabi. Kanisani hapo amelakiwa na waamini zaidi ya 300 waliokuwa na furaha kubwa kukutana na kuzungumza na Khalifa wa Mtakatifu Petro. Baba Mtakatifu amesema, inafurahisha na kutia moyo kutembelea na kusali katika Makanisa machanga duniani. Ametumia fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza waamini kwa ushuhuda wa tunu msingi za Kiinjili huko katika Umoja wa Falme za Kiarabu!

Papa: Matembezi Binafsi
05 February 2019, 14:52