Ushauri wa Papa anasema ingekuwa vizuri walimu wa kiyahudi na maparoko wakafanya kazi kwa pamoja katika miji ya kiyahudi Ushauri wa Papa anasema ingekuwa vizuri walimu wa kiyahudi na maparoko wakafanya kazi kwa pamoja katika miji ya kiyahudi 

Papa anamtaja Kard.Bea kuwa alikuwa chachu ya umoja kati ya wakristo na wayahudi

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 28 Februari 2019 amekutana na washiriki wa mkutano uliondaliwa kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 tangu kifo cha Kardinali Augustin Bea.Baba Mtakatifu amesisitizia juu ya umuhimu wa mazungumzo ya kiekumene na kidinina kumtaja Kardinali Bea kwamba alikuwa ni chachu ya umoja kati ya wakristo na wayahudi

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 28 Februari 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa Mkutano uliondaliwa kwa fursa ya kumbukumbu ya miaka 50 tangu kifo cha Kardinali Augustin Bea. Kardinali Augustin Bea alikuwa ni Askofu Mkuu Katoliki na mwanashirika wa Yesu (Mjesuiti) na mwanabiblia wa Ujerumani aliyechaguliwa kuwa Kardinali na Papa Yohane XXIII, mwanzilishi wa uekumene na mazungumzo ya wayahudi na wakristo katika Kanisa katoliki.  Alizaliwa tarehe 28 Mei 1881, nchini Ujerumani, akapata daraja la upadre tarehe 25 Agosti 1912 na kumaliza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana kunako 1914. Tangu 1924 alikuwa ni Profesa wa Maandiko matakatifu ,1930 hadi 1049 alikuwa ni Gombera wa Taasisi ya Kipapa ya Kibiblia na katika miaka hiyo alikuwa ni mkurugenzi wa Gazeti la Biblia. Alichagulia kuwa Kardinali tarehe 14 Desemba 1959 na Papa Yohane XXIII.  Na kifo chake kilitokea kunako tarehe 16 Novemba 1968. Padre Augustin Bea aliwahi kuwa muungamishi wa Papa Pio XII, tangu mwaka  1945 hadi kifo cha Papa huyo kilichotekea  mwaka 1958.

Katika hotuba ya Baba Mtakatifu kwa  wajumbe hao wa mkutano  huo anawashukuru kufika kwao na shukrani kwa Kardinali Kurt Koch kwa maneno yake ya utangulizi wa mkutano huo. Kituo chao katika kushirikiana na Baraza la Kipapa la kuhamasisha umoja wa Kikristo, Taasisi ya kipapa ya Biblia na Kituo cha mafunzo ya kikristo katika Chuo Kikuu vcha Kiyahudi huko Yerusalemm, wanaadhimisha miaka hii kwa njia ya kufanya mikutano mingi katika  ngazi ya juu, wakati wakifanya kumbukumbu ya miaka 50 tangu kifo cha  Kardinali Augustin Bea. Kwa kufanya hivyo wanayo fursa ya kuangalia kwa upya sura hii na kutafakari juu ya hati muhimu za Mtaguso wa II wa Vatican. Na uhusiano na Huyahudi, umoja wa kikristo, uhuru wa dhamiri na dini ni baadhi ya mada msingi ambazo zinapiga kengele leo hii Baba Mtakatifu Francisko amethibitisha.

Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake anasema, Kardinali Bea siyo wa kukumbuka tu kwa kile ambacho alitenda, lakini pia ni pamoja na jinsi gani alikuwa anatenda. Kwa maana hiyo anabaki kuwa mfano wa kuigwa kwa njia ya mazungumzo ya kiekumena na kidini na ndiyo maana ya kufanya mazungumzo ndani ya familia na uyahudi (Tume kwa ajili ya mahusiano ya kidini na uyahudi, Kwa sababu zawadi na wito wa Mungu, 20). Nahum Goldmann, Rais wa Chama cha Wayahudi Duniani alimfafania Kardinali  Bea kwa kutumiamaelezo matatu ambayo ni kuelewa, wingi wa wema wa binadamu na ujasiri (Staatsmann ohne Staat. Autobiographie, 1970, 378). Hizi ni mantiki msingi kwa ajili ya kufanya mchakato wa mapatano ya watu. Hawali ya yote uelewa wa wengine, kwa upande wa Kardinali Bea alikuwa anazingatia upendo na heshima kuwa ni viu  msingi wa mazungumzo. Alikuwa akisema kuwa heshima inatatufundisha hata haki ya kupendekeza ukweli. (A. BEA, Mkutanoi wa wakristo, 1962, 72). Baba Mtakatifu anasema ni kweli kwamba hakuna ukweli nje ya upendo na upendo unainamia nafasi ya kwanza kama uwezo wa kupokea, kukumbatia na kuichukulia kwake.

Mantiki ya pili ya wema na ubinadamu, ni kujua kuunda yaani kutengeneza urafiki, mahusiano yanayofungamana juu ya undugu na ambamo unatuunganisha kama  viumbe wa Mungu ambaye ni Baba na anataka tuwe ndugu. Uelewa wa kumkubali mwingine, ni wema unaogundua na kuunganisha mahusiano ya umoja; na yote hayo yalikuwa yanamsaidia. Na mantiki ya tatu ilikuwa ni tabia ya ujasiri ambao Padre Congar alikuwa akielezea kama uvumilivu wa kutosha (S. SCHMIDT, Augustin Bea, The Cardinal of Unity, 1992, 538). Kardinali Bea alikuwa anasema: mtaguso hautakuwa na mahali pa kufikia iwapo hauna mahali pa kuanzia” (Mkutano wa wakristo 22). Baba Mtakatifu Francisko amependa kusisitizia juu ya matunda ya safari ya pamoja iliyofikia kwa njia ya  mazungumzo kati ya wayahudi na wakatoliki baada ya Kardinali Bea na shule yake. Katika mchakato wa Kituo chao ni hatua msingi kwani Vatican iliomba Chuo Kikuu cha Gregoriana, kusimamia mafunzo na kilikabidhiwa mpango muhimu sana wa mafunzo ya kiyahudi katika Kanisa Katoliki (hati ya pamoja ya mafunzo ya kiyahudi, 14 Novemba 2002)

Kadhalika Baba mtakatifu wakati akiwatakia matashi mema kwa kazi yao amependa kuwapongeza wanafunzi ambao wamenza mafunzo hayo ya kiyahudi ambayo siyo rahisi na kusoma somo hili katika dunia na utamaduni  ambao ni tajiri lakini mgumu. Anawatia moyo waendelee mbele. Anawashukuru maprofesa  ambao kwa ukamrimu wao wanajikita kwa muda wao na taaluma yao. Kwa namna ya pekee pongezi kwa maprofesa wa somo la Kiyahudi katika Chuo Kikuu cha Yerusalemu na wengine wote wanahijihusisha na kituo hicho. Wanao wanafundisha katika mazingira ambayo katika uwepo wao wanawalikilisha tayari mapya ya ujumbe wenyewe. Kwa hakika ni kwa jinsi gani ya kuanzisha mazungumzo ya dhati bila kuwa na utambuzi wa ndani? Mazungumozo yanapaswa yapelekwe mbele kwa sauti mbili na ushuhuda wa maprofesa wa kiyahudi na katoliki ambao wanafundisha pamoja ndiyo muhimu zaidi ya mazungumzo!

Na sasa kwa jinsi gani ya kuendelea na safari? Baba Mtakatifu Francisko anauliza swali hili na kujibu kuwa  hadi sasa mazungumzo ya kiyahudi na kikriso mara nyingi yamefanyika kwa mantiki ya aragaha zaidi ya wataalam. Kutafakari kwa kina na uelewa maalum ni msingi lakini haitoshi. Kandoni mwa njia hiyo inahitajika kuchukua njia nyingine, iliyo kubwa na ambayo ni ya kuendeleza matunda kwa  sababu mazungumzo yasibaki yanaonekana kwa walio wachache, bali yageuke kuwa ni fursa ya matunda kwa wengi. Urafiki na mazungumzo kati ya wahayahudi na wakristo kwa dhait yanatakiwa kutazama upeo na kuvuka mipaka yake ya jumuiya ya kisayansi. Ingekuwa vizuri kwa mfano katika mji wa Wayahudi, walimu wa kiyahudi na maparoko kufanya kazi pamoja na jumuiya zao, katika kutoa huduma ya binadamu anayeteska na kuhamasisha njia za amani,na mazungumzo kwa wote. Ndiyo matashi mema ya Baba Mtakatifu kwa jitihada hizi za  kazi yao ya utafiti na mahusiano binafsi kati ya wakristo na wayahudi ili yaweza kutoa matunda katika  ardhi yenye rotuba na kusimika mizizi yake ya muungano wa kina. Kwa ajili ya kumbukumbu ya sura na kazi ya Kardinali Bea iwe ni chachu katika jitihada zao za utafiti wa umoja kati ya wakristo na kuhamasisha kwa dhati upyaisho wa urafiki na ndugu wayahudi.

28 February 2019, 14:23