Tafuta

Katekesi ya Papa 13 Februari 2019 Katekesi ya Papa 13 Februari 2019 

Papa:Yesu anawataka wafuasi wake wasiwe wanafiki!

Katika tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa katekesi yake tarehe 13 Februari 2019 kwenye Ukumbi wa Papa Paulo VI mjini Vatican kwa waamini na mahujaji kutoka pande zote za dunia amesisitizia juu ya sala ya kimya na wazi kwa Mungu kwa kufuata mfano wa mafundisho ya Yesu na ili kuepuka unafiki wakati wa sala

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tuendelee na hatua ya mchakato wa kujifunza daima vema kusali kama Yesu alivyo tufundisha. Tunapaswa kusali kama, Yeye alivyo tufundisha kufanya. Yeye alisema: wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujaza. Yesu anawataka mitume wake wasiwe wanafiki kwana anasema: Tena msalipo, msiwe kama wanafikikwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia,ili waonekane na watu. Yesu hataki unafiki.Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa katekesi yake tarehe 13 Februari 2019 kwenye Ukumbi wa Papa Paulo VI mjini Vatican kwa waamini na mahujaji kutoka pande zote za dunia. Mada ya katekesi iliyoongoza siku ni  Baba wa watu wote, kama mwendelezo wa sala ya Baba Yetu, ma baada ya kusoma Injili ya Luka 10,21-22.

Sala ya kweli ni ile ya sirini na katika dhamiri

Sala ya kweli ni ile inayotimizwa sirini ndani ya dhamiri na moyo usiotabirika na ambao unaonekana na Mungu tu peke yake. Yaani Mimi na Mungu. Kwa Mungu huwezi kujificha, kwa maana dhamiri iko wazi na huwezi kabisa kujificha. Sala ina mzizi wake,na mzizi wa mazungumzo ya Mungu, kuna mazungumzo ya kimya kama vile kukutanisha mitazamo ya macho kati ya watu wawili wapendano. Binadamu na Mungu wanakutanisha mitazamo kwa njia ya sala. Kutazama Mungu na kuachwa utazama naye ndiyo maana ya kusali. Baba Mtakatifu ametoa mfano kwamba kuna wengine wanasema, wakati wa kusali hawana maneno… lakini kuacha utazamwe na Mungu ndiyo maana ya sala nzuri! anathibitisha Baba Mtakatifu. Pamoja na mfuasi kuamini anasali kwa dhati lakini katika siri ya dhamiri, mkristo ahachi dunia nje ya mlango wa chumba chake, bali anaingia na dunia hiyo katika moyo wa mtu na hali zote, matatizo na mbamo mengi ambaye yanapelekwa katika sala.

Je ni kitu gani kinakosekana wakati wa kusali sala ya Baba Yetu?

Kuna mambo mengi ya kutafakari katika sala ya Baba Yetu japokuwa ni vigumu kujibu swali kuhusu tafakari hiyo kwa maana inakosekana neno moja. Baba Mtakatifu amesema kwamba wengi wanafikiri ni kitu gani kinakosa katika sala ya baba Yetu. Ameuliza swali: Je ni kitu gani kinakosekana? Ni neno moja ambalo katika nyakati zetu labda wote hawalitilii maanani.  Je ni Neno gani ambalo tunasali kila siku katika Sala ya Baba Yetu? Yesu anatufundisha kusali midomoni mwetu hawali ya yote kutumia WEWE kwa sababu sala ya kikristo ni mazungumzo kwamba: Jina Lako litukuzwa, Ufalme wako ufikie na  utakalo nalifanyike. Anaongeza kusema Baba Mtakatifu: Siyo jina langu, ufalme wangu, utashi wangu, hapana kwa maana siyo sala hiyo, Sala inapitia sisi sote. Sehemu yote ya pili ya Baba yetu inajikita katika kwenye kutumia nafasi ya wingi: Utupe leo mkate wa kila siku, utusamehe makosa yetu, usituache katika majaribu, utuokoe maovuni. Hadi kufikia maombi msingi ya binadamu kama yale ya kuomba  chakula kwa ajili ya kutuliza njaa,yote ni maombi yanayotumia nafasi ya wing. Katika sala ya kikristo hakuna anayeomba mkate kwa ajili yake kwamba: nipe mkate leo hii, hapana, bali utupatie mkate. Kwa maana hiyo tunaomba kwa ajili ya wote na kwa ajili ya masikini duniani. Lakinimara nyingi neno hili linakosekana leo hii, Baba Mtakatifu amebainisha.Na tunapaswa kusali kwa njia ya kutumia WEWE SISI. Ndiyo fundisho jema alilofundisha Yesu, Baba Mtakatifu amekazia kutosahau!. Lakini hiyo ni kwa sababu gani? Baba Mtakatifu anajibu kwamba ni kwa sababu hakuna nafasi ya ubinafsi katika mazungumzo na Mungu. Hakuna nafasi ya matatizo binafsi ambayo siyo sala ya jumuiya ya kaka na dada. Sisi sote  ni jumuia nzima inayosali kwa pamoja .

Katika sala ya mkristo anapeleka matatizo ya watu

Katika sala mkristo anapeleka matatizo ya watu wote wanaoishi karibu naye na wakati wa usiku, anamsimulia Mungu machungu yote ambayo amekutana nayo kwa siku. Yote anayaweka mbele yake, sura zote za marafiki na hata wale wenye kuleta vizingiti mbele yake: katika sala zake hawaoni kama maadui. Iwapo mtu hatambui mtu aliye karibu yake hasa  watu wanaoteseka na wala kuwa na huruma ya machozi ya masikini, ina maana ymoyo wake uko mbali ni moyo mkavu na zaidi ni kama jiwe. Katika kesi kama hiyo ni vema kumwomba Bwana aguse Roho ili moyo uweze kuwa na huruma: Bwana niumbie moyo wangu uwe na huruma, amekazia Baba Mtakatifu. Mungu nisaidie moyo wangu uwe mwepesi ili niweze kutambua, kubeba matatizo ya wote namachungu ya wengine. Kristo hakupita kandoni mwa taabu za dunia hii, kila mara aliphisi upweke, uchungu wa mwili au roho alikuwa akihisi uchungu wa kweli kama wa umbu la mama. Hali hiyo ya kuhisi huruma kuu ndiyo neno na ufunguo wa Injili kwa mkristo na ndiyo ulimsukuma Msamaria mwema kumsaidia mtu aliyejeruhiwa na majambazi na kuwachwa kandoni mwa baraba na alikuwa kinyume na wengine waliokuwa na moyo mgumu.Tunaweza kujiuliza maswali je ninapo sali ninajifungulia katika mateso ya wengine. Je ninaposali ninakuwa na utulivu?

Wapo watu wasio mtafuta Mungu lakini Yesu anataka tusali kwa ajili yao

Wapo watu ambao ambao hawamtafuti Mungu lakini, Yesu anataka tusali hata kwa ajili yao kwa maana Mungu pia anawatafuta watu hawa wote. Yesu hakuja kwa ajili ya wenye afya, bali walio wagonjwa na wenye dhambi (Lk 5,31)  yaani kwa wote hata kwa wale wanaofikiri ni wenye afya,lakini kwa hakika hapana. Iwapo tutafanya jitihada za haki hatuwezi kuhisi kuwa bora zaidi ya wengine. Baba anapenda wote na hivyo tujifunze kutoka kwa Mungu ambaye daima ni mwema kwa wote na kinyume chake sisi tunashindwa kuwa wema na wengine au kuwa wema kwa yule ambaye tunampenda tu.Baba Mtakatifu amemahitimisha kaka na dada, watakatifu na wadhambi, wote ni ndugu tunaopendwa na Baba Mmoja. Na jioni ya maisha yetu tutahukumiwa juu ya upendo, hasa ni  kwa jinsi gani tulipenda. Siyo upendo wa kihisia, bali ni upendo upeo na wa dhati kwa mujibu wa sheria ya kiinjili, isemavyo : Amin,nawaambia,kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo,mlinitendea mimi.

 

 

13 February 2019, 14:36