Tafuta

Vatican News
Tarehe 6 Machi 2019 ni mwanzo wa kwaresima ambao unafunguliwa kwa kupakwa majivu. Misa ya majivu kwa upande wa Papa itafanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Sabina Tarehe 6 Machi 2019 ni mwanzo wa kwaresima ambao unafunguliwa kwa kupakwa majivu. Misa ya majivu kwa upande wa Papa itafanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Sabina 

Kalenda ya maadhimisho ya Papa mwezi Machi na Aprili 2019

Kalenda ya maadhimisho ya Baba Mtakatifu Francisko kwa mwezi Machi na Aprili 2019 imetolewa na Monsinyo Guido Marini msimamizi mkuu wa maadhimisho ya Liturujia za Papa

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 26 Februari 2019 Monsinyo Guido Marini Msimamizi Mkuu wa maadhimisho ya Liturujia  za Papa  ametoa kalenda ya maadhimisho ya Baba Mtakatifu kwa mwezi wa Machi na Aprili 2019. Kalenda hiyo inaanza na siku ya  Jumatano, tarehe 6 Machi 2019 ambayo ni siku ya majivu. Baba Mtakatifu ataongoza maandamamo katika Kanisa la Mtakatifu Anselmi saa 10.30 za jioni masaa ya Ulaya na kuadhimisha Misa Takatifu, kupaka majivu na baraka katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Sabina saa 11.00 jioni.

Dominika ya kwanza ya Kwaresima tarehe 10 Machi 2019 ni mwanzo wa Mafungo ya Kipindi cha Kwaresimakwa Baba Mtakatifu na wahudumu wote wa Vatican huko Ariccia, nje kidogo ya mji wa Roma. Ijumaa tarehe 15 Machi 2019  ni siku ya kumaliza mafungo ya kiroho huko Ariccia. Ijumaa tarehe 29 Machi  2019, Baba Mtakatifu ataongoza maadhimisho ya kitubio katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican saa 11.00 jioni masaa ya Ulaya. Jumamosi na Jumapili tarehe 30-31 Machi 2019, Baba Mtakatifu Francisko atafanya ziara ya kitume nchini Morocco.

Mwezi Aprili 2019

Domenika tarehe 14 Aprili 2019 ni siku kuu ya Matawi na mateso ya Bwana ambapo ni matarajio ya maandamano na maadhimisho ya misa kuu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro majira ya saa 4.00, asubuhi masaa ya Ulaya. Alhamisi Kuu, tarehe 18 Aprili 2019, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican saa 9.30 asubuhi ni Misa Takatifu ya kubariki mafuta.

Ijumaa Kuu Takatifu  tarehe 19 Aprili 2019, ni maadhimisho ya mateso ya Bwana saa 11.00 Jioni masaa ya Ulaya  katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Na saa 3.15 usiku Baba Mtakatifu ataangoza Njia ya Msalaba katika magofu ya Koloseo mjini Roma. Jumamosi Kuu, tarehe 20 Aprili 2019, saa 2.30 usiku katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro ni kuanza mkesha wa Pasaka. Jumapili ya Pasaka tarehe 21 Aprili 2019, saa 4.00 asubuhi masaa ya Ulaya itakuwa ni maadhimisho ya Misa ya siku ya Pasaka katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Na saa 6.00 katikati ya Kanisa Kuu Mtakatifu Petro itatolewa Baraka ya “Urbi et Orbi”.

 

 

26 February 2019, 12:06