Tafuta

Vatican News

Papa:Ni wajibu wetu kujua hadhi ya kila mtu na kuokoa maisha!

Baba Mtakatifu Francisko ametoa ujumbe wake kwa njia ya video kwa wajumbe na waandaaji wa Mkutano wa 7 wa dunia kuhusu hukumu ya kifo unaofanyika mjini Bruxelles akiwaomba wazuie kuktaisha maisha ya wengine na badala yake watoa fursa ya kufanya toba kwa wahalifu

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 27 Februari 2019, Baba Mtakatifu Francisko ametoa ujumbe wake kwa njia ya video kwa wajumbe  na waandaaji wa Mkutano wa  7 wa dunia kuhusu hukumu ya kifo unaofanyika mjini Bruxelles. Baba Mtakatifu anasema, maisha ya binadamu ni zawadi tuliyoipokea. Ni muhimu na msingi. Ni kisima cha zawadi nyingine na haki nyingnine zote ambazo ni lazima kulindwa. Na zaidi kwa waamini wanatambua kuwa binadamu ameumbwa kwa mfano na sura ya Mungu. Lakini iwe kwa waamini na wasio waamini, kila maisha ni mema na hadhi yake lazima ilindwe bila kuwekewa vizingiti.

Hukumu ya kifo ni ukiukwaji mkubwa wa hali ya kila maisha ya mtu

Akiendelea na ujumbe wake anasema hukumu ya kifo ni ukiukwaji mkubwa wa haki ya maisha ya kila mtu. Na kama kweli jamii na jumuiya ya binadamu wanakabiliana mara nyingi na uhalifu mkubwa ambao unahatarisha wema wa pamoja na usalama wa kila mtu, lakini ni sawa na kweli kwamba leo hii kuna vyombo vingine ambavyo vinalipiza hasara iliyotendwa na ambayo ni mfumo wa gereza ambao unakuwa daima mwafaka wa kulinda jamii dhidi ya ubaya mbao unaweza kusabaishwa kwa  baadhi ya watu. Kwa upande mwingine kuna kuzingatia hata kumpatia fursa mwenye makosa ya kuweza kutubu na ambaye haiwezekani kumwacha peke yake. Na ndiyo sababu ya nchi nyingi kuendelea kuahidi juu ya kujali  maisha na siyo juu ya hukumu ya kifo au kufika kuondoa kabisa sheria hiyo ya hukumu  kama mantiki chanya anasisitiza Baba Mtakatifu.

Kanisa daima ni mlinzi wa maisha 

Baba Mtakatifu anasema Kanisa daima limekuwa ni mlinzi wa maisha katika maono dhidi ya hukumu ya kifo amaye imekomaa. Kwa sababu hiyo,Baba Mtakatifu  amependelea kusasisha hata  Katekisimu ya Kanisa Katoliki. Hiyo kwa sababu anasema kwa kipindi kirefu, hukumu ya kifo ilifikiriwa kama jibu linalofaa kwa wahalifu  ili kulinda wema wa pamoja. Japokuwa na kufanya tendo hilo hadi ya  hadhi ya mtu haipotei hata kama huyo ametenda uhalifu mbaya sana. Hakuna ambaye anaweza kuwawa au kukosa fursa ya kukumbatiwa kwa upya na jumuiya ambayo ameijeruhi na kufanya iteseke. Lengo la kuondoa hukumu ya kifo duniani kote, inawakilisha ujasiri wa kuthibitisha misingi ya hadhi ya binadamu na uhakika kuwa binadamu anaweza kukabiliana na uhalifu zaidi ya kukataa ubaya, kwa kumtafuta uwezekano mwingne aliyehukumiwa kipindi cha kufanya malipizi kwa mabaya aliyotenda ili afikiria kwa upya hali yake na kuwa na uwezo wa kubadili maisha yake na ikiwezana na daima.

Matashi mema duniani ili hukumu ya kifo iweze kufutwa kabisa

Baba Mtakatifu anahitimisha akiwatakia mema na kuwasindikiza katika sala, kuwatia moua katika kazi yao na zaidi wakuu wa nchi na wadau wanaohusika katika nchi zao ili watumize hatua muhimu kuelekea kufuta kabisa hukumu ya kifo. Baba Mtakatifu anaongeza: Ni wajibu wetu kujua hadhi ya kila mtu na kufanya kazi kwa namna ya kuweza kuona kwamba hawaangamizi maisha mengine badala yake wanayakomboa kwa sababu ya wema wa jamii na hali zake.

27 February 2019, 17:10