Tafuta

Vatican News
Tuinge mfano wa Maria, Yosefu na wachungaji, lakini pia Mamajusi ambao walijkita katika hija ya  kumtafuta  Masiha na wakamwona Tuinge mfano wa Maria, Yosefu na wachungaji, lakini pia Mamajusi ambao walijkita katika hija ya kumtafuta Masiha na wakamwona  (Vatican Media )

Wito wa Papa kwa viongozi wa Ulaya waoneshe ukarimu na mshikamano!

Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko ametoa wito kwa viongozi wote wa Ulaya kuonesha ukarimu na mshikamano ili kuwapokea wahamiaji ambao kwa siku kadhaa wako bado ndani ya Meli wakitafuta Forodha ya kutua penye usalama. Kadhalika amewatakia matashi mema ya sikukuu ya Noeli kwa wakristo wa Kiorthodox wa nchi za Mashariki

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa siku nyingi hivi watu arobaini wameokolewa katika Bahari ya Mediterania na wako bado katika Meli mbili za Shirika lisilo la kiserikali wakitafuta mahali penye forodha ya kutua na yenye  usalama. Kutokana na hilo ninatoa kwa mara nyingine  tena wito kwa viongozi wa Ulaya ili waonesha kwa dhati ukarimu mbele tatizo la watu hawa. Ndiyo wito wa Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Saala ya Malaika wa Bwana, akiwaomba viongozi wote wa Ulaya kuonesha ukarimu na mshikamano wa kuwapokea wahamiaji ambao kwa siku nyingi wamekataliwa kupokelewa katika nchi za Ulaya.

Noeli ya kwa baadhi ya wakristo wa Kiorthodox

Baba Mtakatifu amewatakia matashi mema kwa baadhi ya makanisa ya mashariki katoliki na kiorothodox ambao wanafuata kalenda ya Juliani na wataadhimisha Noeli Takatifu tarehe 7 Januari 2019, ni matashi mema ya kindugu kwa ishara ya muungano kati ya wakristo wote wanaomtambua Yesu kama Bwana na Mwokozi. Kwa wote anawatakia Heri ya Noeli.

Sikukuu ya Epifania Sambamba na Siku ya kimisionari kwa watoto na vijana ( Utoto mtakatifu)

Sikukuu ya Epifania pia inakwenda sambamba na  siku ya Kimisionari kwa watoto na vijana ( Utoto Mtakatifu) ambapo mwaka huu inawaalika vijana wote wamisionari kuwa wanariadha wa Yesu ili kushuhudia Injili katika familia, shuleni na mahali popote pale wanapokuwa. Kwa mwaana hiyo, Baba Mtakatifu Francisko amewatumia salam binafsi kwa mahujaji, familia parokia, vyama vya kitume kutoka Italia na sehemu mbalimbali za nchi.

Amwasalimia hata kwa namna ya pekee kikundi cha kihistoria cha bandi ambayo inahamasisha thamani ya sikukuu ya Epifania na ambayo kwa mwaka huu imewakilishwa na eneo la Mkoa wa Abruzzo nchini Italia. Amekumbuka Tamasha la msafara wa Mamajusi unaoendelea katika miji mingi ya Poland kwa ushiriki wa familia nyingi na vyama ya kitume. Amewasalimia pua  bendi ya muziki iliyokuwako katika uwanja kwa furaha katika sikukuu ya Epifania na kwa wote amewatakia sikukuu njema na kama kawaida wasisahau kusali kwa ajili yake.

06 January 2019, 13:37