Tafuta

Tume ya Kipapa ya Ecclesia imeunganishwa katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa chini ya Usimamizi wa Rais wake Kardinali Luis Ladaria Ferrer Tume ya Kipapa ya Ecclesia imeunganishwa katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa chini ya Usimamizi wa Rais wake Kardinali Luis Ladaria Ferrer 

Tume ya Ecclesia Dei imenganishwa katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu

Baba Mtakatrifu Francisko amefuta Tume ya Kipapa ya Ecclesia Dei iliyokuwa imeunda mara baada ya uasi wa Wafebvriani. Zoezi la tume hiyo sasa limeunganishwa katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa Barua ya Kitume katika mfumo wa “Motu proprio”, Baba Mtakatifu Francisko tarehe 19 Januari 2019 amefuta Tume ya Kipapa ya Ecclesia Dei, iliyokuwa imeundwa kunako tarehe 2 Julai 1988 na Mtakatifu Yohane Paulo II kwa shughuli ya kishirikiana na Maaskofu na Mabaraza ya Kipapa Vatican, ili kurahisisha umoja kamili wa kanisa la mapadre, waseminari na watawa wa kike na kiume mbao walikuwa wanataka kubaki wameungana na Mfuasi wa mtume Patro katika Kanisa kwa kuendelea kutunza utamaduni wa kitasaufi na kiliturujia kutokana na kwamba zilikuwa ni jumuiya za kindugu zilizokuwa zimeanzishwa na Askofu Mkuu Marcel Lefebvre.

Uamuzi wake Baba Mtakatifu

Uamuzi wa Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa umefikia hatua hiyo mara baada ya kufanya tafakari pana na iliyofuata baadhi ya michakato ya hatua nyeti. Mkutano wa tarehe 16 Novemba 2017, wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa walikuwa wamemwomba moja kwa moja moja kuendeleza mazungumzo kati ya Vatican na Jumuiya ya Mapadre wa Mtaktifu Pio X. Kwa kuwa masuala yalikuwa yanahusu mafundisho, Baba Mtakatifu aliridhia maombi yao, yaliyo yalitotolea kunako tarehe 24 Novemba mwaka huo na mapendekezo hayo yakapata kupokelewa kwa ukarimu wakati wa mkutano wa mwaka mwezi Januari mwaka huu. Aidha amesema ni zaidi ya miaka therathini Yume ya Kipapa ya Ecclesia Dei, ( Kanisa la Mungu ) iliyokuwa imeundwa na Motu Proprio "Ecclesia Dei adflicta", ya tarehe 2 Julai 1988 imeweza kutoa suluhisho la ukweli na kusimamia kwa kazi nzuri ya ushirikiano na Maaskofu na Mabaraza ya Kipapa ya Vatican, katika kurahisisha kwa dhati umoja wa Kanisa la mapadre waseminari, jumuiya binafsi za watawa wa kike na kiume, walianzishwa na Monsinyo Marcel Lefebvre, ambao walikuwa na shauku ya kuendelea kubaki wameungana na mfuasi Mkuu wa Petro katika Kanisa Katoliki, kwa kuhifadhi utamaduni wa kitasaufi na kiliturujia. Kwa namna hiyo wao waliendelea shughuli na mamlaka katika usimamizi kwa jina la Vatican kwa kujiita chama au vyama hadi ilipofikia kinyume na ilivyokuwa.

Motu Proprio ya tarehe 7 Julai 2007

Baadaye kwa nguvu za Motu Proprio ya Summorum Potificum ya Papa ya tarehe 7 Julai 2007, Tume ya Kipapa iliweza kuweka madaraka yake ya Vatican juu ya taasisi na Jumuiya za kidini ambazo zilikuwa zimekubali  mfumo wa kawaida wa utamaduni wa Roma na ambazo zimepokea utamaduni wa awali wa maisha ya kitawa na kutunzwa kwa usimamizi na juu ya lengo lilikuwa limekubaliwa. Baada ya miaka miwili, mtangulizi wake Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kwa Motu Proprio ya Eclessiae unitatem (Kanisa lililoungana) ya tarehe 2 Julai 2009, iliweze kuunda kwa upya mfumo wa Tume ya Kipapa na ili hatimaye kuweza kuuunda kwa upya kutokana na kusimamishwa kwa maaskofu wanne waliokuwa wamepewa daraja la uaskofu bila idhini ya Papa. Na zaidi Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba, kwa kuzingatia kuwa baada ya tendo hilo la neema na masuala ambayo yametazamwa na Tume ya Kipapa ya Mafundisho Tanzu ya Kanisa, ikiwa ni ya asili msingi wa mafundisho ya Kanisa na tume ambayo ni kiungo kikuu zaidi kinachounganisha na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, kwa kuhifadhi hata vyanzo msingi vilivyo pyaishwa muundo.

Mapendekezo ya Mkutano wa tarehe 23-25 Januari 2018 wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa

Kutokana  na sababu hizo na pia  ruhusu ya Mkutano wa  IV wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa uliofanyika  tarehe 15 Novemba 2017, na ambao ulitoa maombi ya kwamba kuwepo na mazungumzo kati ya Vatican na Jumuyia ya Mapadre wa Mtakatifu Pio X ili waweze kukubaliwa kuwa Shirika kwa kuwa masuala yaliyokuwa wamezungumzia yalikuwa na tabia ya mandisho, ambapo katika maombi hayo, Baba Mtakatifu aliridhia katika Mkutano na Rais wa Kipapa wa Mafundisho Tanzu ya Kanisa, tarehe 24 Julai; kadhahalika kutokana na mapendekezo yaliyopokelewa wakati wa Mkutano wa mwaka wa Baraza hilo, waliyofanya kuanzia tarehe 23 -26 Januari 2018, na baada ya kutafakari sana Baba Mtakatifu amefikia maamuzi yafuatayo:

Kwa kuzingatia leo hii kutulia kwa  hali zilizokuwa zimepelekea Mtakatifu Yohane Paulo II kuunda Tume ya Kipapa ya Ecclesia Dei;  Kwa kutazama kuwa Taasisi na Jumuia za Watawa zinaadhimisha mtindo wa kawaida na wameweza kuwa na msimamo wa idadi na maisha; kwa kuzingatia tendo la mwisho na masuala yote yaliyozingatiwa na Tume ya Kipapa ya Ecclesia Dei kuwa  ni masuala  ya kawaida ya mafundisho; kwa kupendelea kuwa lengo hili la mwisho linakuwa daima wazi, na  katika dhamiri ya jumuiya za Kanisa, Baba Mtakatifu anahitimisha kwa kuridhia na Barua yake ya Kitume ( ‘Motu proprio data’) kwamba anamua kufutwa kwa  Tume ya Kipapa ya Ecclesia Dei, iliyokuwa imeundwa kunako tarehe 2 Julai 1988 kwa Barua ya Motu Proprio Ecclesia Dei adflicta.

Shughuli za tume hiyo sasa zinaingia moja kwa moja katika Baraza la Kipapa la mafundisho tanzu ya Kanisa

Baba Mtakatifu Francisko aidha amethibithisha kuwa shughuli za Tume kwa maneno mengine, inakabidhiwa yote katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na ndani ya umbu hilo wataunda kitengo kinachojihisisha na mwendelezo wa shughuli za usimamizi, uhamasishaji na ulinzi ambao umeendeshwa na Tume ya Ecclesia  dei iliyofutwa. Vilevile Baba Mtakatifu amethibitisha kuwa, bajeti ya Tume ya kipapa ya Ecclesia dei inaingia katika mahesabu ya kawaida ya Baraza la Kipapa na Mafundisho Tanzu ya Kanisa.

Katika Barua ya kitume wa Yohane Paulo II 1988

Kwa kutazama kuanzishwa kwa tume hiyo tunaweza kukumbuka badhi ya maneno ya Barua ya Kitume ya “Ecclesia Dei” ya Mtakatifu Yohane Paulo II aliyo anadika mara baada ya hutoaji wa daraja la uaskofu bila idhini ya Papa kunako tarehe 30 Juni 1988 na Askofu Mkuu Marcel Lefebvre na ambaye alikataa baadhi ya usasisho wa maamuzi ya Mtaguso wa Vatican II. Tendo hilo Mtakatfu Yohane Paulo II alithibitisha kuwa unatoa mwanya kwa wote kufanya tafakari ya kina na ili kupyaisha shughuli za uaminifu kwa Kristo na Kanisa lake. Aidha anathibitisha Mtakatifu Yohane Paulo II, kuwa mzizi wa tendo hili ni uasi  kwa maana unakwenda kiunyume na utamaduni. Kutokamilika kwake kunatokana na kutokuzingatia  tabia za utamaduni ambao kama ulivyokabidhiwa na uwezo wa Mtaguso wa Vatican II, na  mahali ambapo unachota asili ya Mitume na kuendelezwa katika Kanisa chini ya usimamizi wa Roho Mtakatifu. Kwa dhati, inabidi kuwa na uelewa wa mambo hata maneno yanayotolewa yanakua iwapo yatoa tafakari na utafiti kwa waamini, ambao wanatafakari katika mioyo yao, iwe kwa akili ya kina na ambapo wanahisi mambo ya kiroho au kuhubiri wale ambao,ni wafusi wa maaskofu ambao wamepokea karama hakika ya ukweli.

19 January 2019, 14:47