Cerca

Vatican News
Tarehe 1 Januari ni Siku ya 52 ya Kuombea Amani Duniani kwa Mwaka 2019 Tarehe 1 Januari ni Siku ya 52 ya Kuombea Amani Duniani kwa Mwaka 2019   (Vatican Media)

Papa:Watu wote wawajibike kukuza amani katika jamii duniani!

Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana,Baba Mtakatifu amewatakia matashi mema ya Mwaka mpya 2019, kwa mahujaji na waamini wote na shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Italia kwa matashi mema aliyomtakia na amewapongeza watu wote wanaojikita katika harakati za kukuza amani duaniani

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Siku ya Noeli nilitoa ujumbe wa matashi mema ya kindugu kwa Roma na katika ulimwengu mzima. Na leo hii kwa mara nyingine ninarudia kuwatakia baraka na neema ya amani na matarajio mema. Tusali kila siku kwa ajili ya amani. Ndiyo mwanzo wa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 1 Januari 2019, aliyowambia mahujaji na waamini waliyokusanyika katika Kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini  kusali katika sala ya Malaika wa Bwana, wakati Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu, sambamba na maadhimisho ya Siku ya 52 ya Kuombea Amani Duniani kwa Mwaka 2019.

Shukrani za matashi mema ya Rais wa Jamhuri ya Italia

Baba Mtakatifu Francisko, anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Italia kwa matashi mema aliyomtakia wakati akihutubia taifa tarehe 31 Desemba usiku wa kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya. Bwana abariki daima huduma yake yenye thamani kwa watu wa Italia.

Pongezi kwa jumuiya, vyama na mashirika kwa ajili ya kukuza amani

Kadhalika Baba Mtakatifu Francisko anawatakia matashi mema ya sikukuu watu wa Roma, mahujaji wote walionganika katika Kiwanja cha Mtakatifu Petro kwa idadi kubwa! Na kwamba, utafikiri ilikuwa ni siku ya kutangaza watakatifu. Aidha kwa washiriki wa maandamano ya amani katika nchi zote yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidiom amewapongeza na kuonesha ukaribu wake wa jumuiya hiyo kwa sala na katika juhudi zao za amani duniani kote, vilevile amekumbuka jumuiya mbalimbali za Kanisa kwa namna ya pekee hata usiku wa tarehe 31 Desemba huko Matera nchini Italia Na kwa maombezi ya Bikira Maria, Bwana awape neema ya kuwa mafundi wa amani lakini amani inaanzia nyumbani, katika familia, mafundi wa amani kila siku katika mwaka mpya. Anawatakia kwa mara nyingine matashi mema na heri ya mwaka mpya, wakati huo huo wasisahau kusali kwa ajili yake.

01 January 2019, 13:54