Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu akishuhudia wasanii kutoka Quba mara baada ya Katekesi yake tarehe 2 Januari 2018 katika Ukumbi wa Paulo VI Baba Mtakatifu akishuhudia wasanii kutoka Quba mara baada ya Katekesi yake tarehe 2 Januari 2018 katika Ukumbi wa Paulo VI 

Papa:Uzuri unainua mioyo daima na kutufanya tuwe wema kwa Mungu!

Mara baada ya tafakari ya katekesi, Baba Mtakatifu Francisko amewasalimia mahujaji wote na zaidi kuwapongeza wasanii wa michezo kutoka Quba ambao wamecheza mbele yake. Papa anasema uzuri unainua mioyo na kutufanya tuwe wema na hata kutufikisha kwa Mungu. Amewaalika waamini wote katika maadhimishao ya sikukuu ya Epifania ya Bwana Jumapili ijayo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mara baada ya tafakari ya katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 2 Januari 2019, amewasalimia waamini wote na mahujaji kutoka pande zote za dunia. Bila kuwasahu kwa namna ya pekee vijana, wazee, wagonjwa na manandoa wapya: Amewasifu kwa wingi wao, hasa kuwa wajasiri wa kufunga ndoa.

Kadhalika amewasalimia na kuwashurukuru wasanii wa michezo kutoka nchini Quba. Akifafanua juu ya mchezo amesema: mchezo wao leo,unaoenesha uzuri wa ajabu na ambao unahitaji juhudi kubwa ili kufikia kuonesha kile walichokiona mbele yao. Inahitajika mazoezi mengi, kwa maana hiyo amewatia moyo waendelee mbele namna hiyo katika dunia. Aidha amefafanua juu ya neno uzuri kwamba, uzuri daima unainua moyo, uzuri unatufanya tuwe wema na uzuri unapelekea kufikia wema hadi kutufikisha hata kwa Mungu.

Dominika ijayo Baba Mtakatifu Francisko amesema tunaadhimisha Sikukuu ya Epifania ya Bwana na kwa maana hiyo, kama Mamajusi tuige mfano hata sisi kuwa na mtazamo wetu juu mbinguni. Ni kwa kufanya hivyo tu, tutaweza kuona nyota ambayo inatualika kutembea katika njia ya wema amethibitisha. Na hatimanye amewatakia wote heri ya mwaka mpya.

 

 

 

 

 

02 January 2019, 16:02