Tafuta

Tushike mkono Maria, kwani kukaa nawe tutaweza kushinda vimbunga vikali vya kihistoria na Mama wengi uwashika mikono watoto wao Tushike mkono Maria, kwani kukaa nawe tutaweza kushinda vimbunga vikali vya kihistoria na Mama wengi uwashika mikono watoto wao 

Papa:Tushike mkono Maria,kukaa nawe tutashinda vimbunga vikali!

Tushike mkono ili kugundua mahusiano ambayo yanaunganisha. Tukusanyike pamoja chini ya vazi lako na upendo wa kweli, mahali pa kurudisha familia ya kibinadamu. Ndiyo mbiu iliyosikika katika mahubiri ya Papa Francisko tarehe 1 Januari 2019 katika Sikukuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu. Mama siyo uchaguzi bali tumpokee katika maisha, Malkia wa amani

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Wote waliosikia hayo walishangaa juu ya habari walizoambiwa na wachungaji( Lk 2,18). Kushangaa ndiyo jambo tunaloalikwa leo hii katika hitimisho la siku ya Nane ya Noeli, tukiwa katika mtazamo bado kuhusu Mtoto aliyezaliwa kwa ajili yetu masikini wa kila kitu, lakini aliyejaa upendo. Mshangao ni tabia ya kuanza nayo  katika mwaka kwa sababu maisha ni zawadi ambayo inatupatia uwezekano wa kuanza daima. Ndiyo mwanzo wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Misa Takatifu ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu, tarehe 1 Januari 2019, sambaba na maadhimisho ya Siku ya Amani duniani.

Mshangao mbele ya Mungu ambaye ni mtoto

Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri anasema leo hii pia ni siku ambayo inashangaza mbele ya Mama wa Mungu. Mungu ni mtoto Yesu katika mikono ya mwanamke, anamnyonyesha Muumba wake. Sanamu iliyoko mbele yao inaonesha Mama na Mtoto ambao wameungana kwa namna ya kufanana na kuwa kitu kimoja. Ni fumbo la leo hii linalojikita katika  mshangao usio kuwa na mwisho. Mungu alijunganisha na ubinadamu daima, Mungu ni mtu daima na ndiyo habari njema ya mwanzo wa mwaka. Mungu siyo bwana aliye mbali, anayeishi pekee yake  huko mbinguni, bali ni upendo uliojifanya mtu na kuzaliwa kama sisi na mama ili awe ndugu wa kila mtu. Yeye yupo juu ya magoti ya mama yake, na hata mama yetu na tangia hapo anainama juu ya ubinadamu kwa ukarimu mpya. Sisi tunatambua vema upendo wa Mungu lakini ni upendo wa baba na mama, kama ule wa mama ambaye hachoki kamwe kuamini watoto na wala kuwaacha kamwe. Mungu pamoja  nasi hatuachi pamoja na kutegemeana na makosa yetu,  dhambi zetu na kwa jinsi gani tunagawanya dunia na tunataka iwe. Mungu anaamini ubinadamu na hata  mahali ambapo mambo yanakwenda kombo kabla yake yeye anamtanguliza mama yake.

Katika mwanzo wa mwaka tumwombe Mama Maria

Mwanzo wa mwaka tumwombe Yeye neema ya kuwa na mshangao mbele ya Mungu wa maajabu. Tupyaishe mshangao wa asili ya tangu ilipozaliwa imani yetu. Mama wa Mungu atusaidie, Mama wa Mungu aliyeumbwa na Bwana, anatuzaa  hata sisi kwa Bwana. Ni mama anayezaa wana wake kwa mshangao wa imani. Maisha bila mshangao yanakuwa ni meusi na ya mazoea tu; kwa manana hiyo ni  imani, Baba Mtakatifu anathibitisha. Hata Kanisa linahitaji kupyaishwa mshangao wa kuwa makao ya Mungu aliye hai; Mchumba wa Bwana, Mama anayezaa watoto wake. Bila kufanya hivyo ipo hatari ya kufanana na kanisa la makumbusho yaliyopita. Mama Bikira Maria kinyume chake anapeleka Kanisa katika hali ya kinyumbani, ya nyumba ambayo anaishi Mungu na mapya mengi. Tupokee fumbo la Mama wa Mungu kama wakazi wa Efeso wakati wa mtaguso. Kama wao walivyotamka na kusema, Mama Mtakatifu wa Mungu. Kwake yeye tuache tutazamwe naye , tuache tukumbatiwe naye, tuache tuchukuliwe kwa mikono yake, Baba Mtakatifu amesisitiza!

Tuache tutazamwe na Mama Maria hata kipindi cha mahitaji

Tuache tutazamwe, hasa hasa wakati wa kipindi cha mahitaji na iwapo tunajikuta tumegugwa na mafundo magumu ya maisha kwa hakika tutazame Mama. Na hiyo ni nzuri hawali ya yote kuacha kutazamwa na Mama. Iwapo tunamtazama,yeye haoni wadhambi, bali anawaona watoto. Wanasema kuwa macho ni kioo cha roho; macho ya aliyejaa neema yanaangaza uzuri wa Mungu na kutafakari juu yetu mbingu. Yesu alisema kuwa macho ni taa ya mwili (taz Mt 6, 22): Macho ya mama yanatambua kuangaza kila aina ya giza na kuwasha kila sehemu matumaini. Mtazamo wake juu yetu unatwambia:“ wapendwa, kuweni jasiri, ni mimi mama yenu”.

Mtazamo wa kimama unaotoa imani unasaidia kukua katika imani. Imani ni mahusiano na Mungu anayejikita ndani ya mtu kabisa na ili aweze kulindwa anahitaji Mama wa Mungu. Mtazamo wa umama unatufanya kujiona waaamini wapendwa wa Mungu na kupendana sisi kwa sisi, zaidi ya vizingiti na mwelekeo wa kila mmoja. Mama Maria anatusimika mizizi katika Kanisa, mahali ambamo umoja unahesabika zaidi ya utofauti,na anatushauri kusaidiana mmoja na mwingine.Kuwa na  ukarimu leo hii watu wengi wataka kuufuta katika kamusi. Mtazamo wa Maria unatukumbusha kuwa ili tuweza kuwa na imani ni muhimu kuwa na huruma ambayo inafukuzia mbali ubaridi. Iwapo katika imani kuna nafasi ya Mama wa Mungu, huwezi kupoteza  kiini ambacho ni Bwana kwa sababu Maria hajielekeze kwake binasfi, bali anaelekeza kwa Yesu na ndugu kwa sababu Maria ni mama

Mtazamo wa Mama Maria ni kama mtazamo wa kila mama

Mtazamo wa Mama ni matazamo wa kila mama. Katika dunia ambayo inatazama wakati ujao bila mtazamo wa umama,na bila kutambua kutazama watu kama wana dunia ni kipofu hata kama itaongeza faida. Kutakuwa na uwepo matapato, lakini hayatakuwapo kwa wote Baba Mtakatifu amesisitiza. Tutaishi katika nyumba sawa, lakini si kama ndugu. Familia ya kibinadamu inahesabu juu ya msaada wa mama. Dunia ambayo upendo wa umelegea au kujikita katika hisia tu, inaweza kuwa tajiri ya mambo lakini dunia haitakuwa  na wakati ujao ulio mwema. Mama wa Mungu anatufundisha mtazamo wake juu ya maisha na mtazamo wake juu yetu na umaskini wetu. "Tunakulilia tikilalamika bondeni kwenye machozi, utuangalia kwa macho yako yenye huruma".

Tuache tukumbatiwe na Mama

Baba Mtakatifu Francisko anafafanua kuwa, baada ya mtazamo, ndipo unaingia mchezo katika moyo mahali ambapo Injili leo hii inasema alikuwa anayaweka na kuyatafakari  mambo hayo yote moyoni mwake  ( Lk 2,19). Mama Maria alikuwa na mambo yote ndani ya moyo wake , alikuwa anakumbatia kila kitu, matukio mema na yale yaliyo kinyume. Yote aliyatafakari, kwa maana alikuwa anayapeleka kwa Mungu. Na ndiyo tazama siri yake. Wakati huo huo maisha ya kila mmoja wetu yako roho mwake, anatamani kukumbatia hali zetu na kuzifikisha kwa Mungu, na ndiyo maana tuache tukumbatiwe na Mama anathibitisha!

Katika maisha yaliyogawanyika leo hii, mahali ambapo ipo hatari ya kupoteza mwongozo ni muhimu  uwepo wa mkono wa Mama. Kuna kupotea na pia upweke mwingi njiani. Duniani inaruhusu na utafikiri daima hakuna muungano. Tunahitaji kuwa na imani kwa Mama. Katika maandishi matakatifu yeye anakumbatia hali nyingi za dhati na yupo mahali ambako kuhahitaji msaada. Alikimbia kwenda kwa binadmu ya Elizabeth, alikwenda katika arusi ya Kana, anawatia moyo mitume katika karamu… Maria ni wakiri wa upekwe na migawanyo. Yeye ni mama wa faraja, anayetuliza. Yeye anakaa na yule aliye mpweke…Yeye anatambua kuwa faraja ya maneno haitoshi, inahitaji uwepo wa karibu; na yeye yupo kama mama. Baba Mtakatifu anasisitiza, tumruhusu akumbatie maisha! Katika sala ya Salam Malkia, tunamwita maisha yetu na utafikiri ni kuzidisha kiasi, kwa sababu Maisha ni Kristo ( Yh 14,6), lakini Maria ndivyo alivyo ungana na Yeye na kuwa karibu na sisi na  hakuna kitu kilicho bora zaidi ya kuweka maisha yetu katika mikono yake na kumtambua kuwa ni maisha, mpole, mpendelevu na matumaini yetu.

Tuache mama Maria atushike mkono wake

Tuache mama Maria atushike mkono wake, Baba Mtakatifu anasema. Mama wengi uwashika mikono watoto wao na kuwapeleka mbele kwa upendo katika maisha. Je ni watoto wangapi leo hii wanatembe peke yao na wanapoteza mwelekeo, kwa maana wanajiamini ni wenye nguvu lakini wanapotea, wako huru lakini wakati huo wanakuwa watumwa. Ni wangapi wamesahau upendo wa umama na wanaishi wamekasirika na kuwa na utofauti wa kila kitu! Ni wangapi kwa bahati mbaya wanatabia mbaya na kionesha chuki na ukatili wa kila kitu! Kujionesha ukatili wakati mwingine hadi kufikia hatua ya kutumia nguvu. Lakini hiyo yote ni udhaifu. Tunahitaji kujifunza kutoka kwa wamama ambao kwa ushujaa wao wanatoa nguvu zao na kuwa na huruma, hekima na upole.

Mungu hakuumba mama yake tofauti na wengine

Mungu hakuumba mama tofauti na wengine na ndiyo maana kuna sababu ya kubwa ya kuhitaji hata sisi Mama. Yesu mwenyewe alitupatia mama yake na si kwa fursa fulani, bali ni wakati ule akiwa katika msalaba, maana aliwaambia  mitume na kila mfuasi kuwa : “ Tazama mama yako! ( Yh 19, 27) . Kuwa na Mama siyo suala la uchaguzi, Yeye anapaswa kupokelewe katika maisha: ni Malkia wa amani ambaye anashinda mabaya na kutupeleka katika njia ya wema, anatupeleka hadi katika umoja kati ya watoto wote na kutuelimisha juu ya kuwa na huruma. Tushike mkono Maria, Kwa maana kukaa nawe Maria tutaweza kushinda vimbunga vikali vya kihistoria. Tushike mkono ili kugundua mahusiano ambayo yanaunganisha. Tukusanye pamoja chini ya vazi lako kwa upole na upendo wa kweli, mahali ambapo panarudisha familia ya kibinadamu. Tunaukimbilia ulinzi wako Mama mzazi Mtakatifu wa Mungu. Baba Mtakatifu amehitimisha akiwaomba waamini wote kurudia sala ya tunaukimbilia ulinzi wako …

 

01 January 2019, 11:30