Tafuta

Barua ya Papa Francisko kwa Rais wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha katika maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanza kwake Barua ya Papa Francisko kwa Rais wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha katika maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanza kwake 

Papa:Kanisa ni kuimarisha nguvu ya ubinadamu katika maisha!

Tarehe 15 Januari 2019 Ofisi ya Vyombo vya habari mjini Vatican imewakilisha Barua ya Baba Mtakatifu Francisko aliyomwandikia Rais wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya Maisha katika fursa ya kuadhimisha mwaka wa 25 tangu kuanzishwa kwake

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Leo hii suala msingi la kuheshimu maisha ya mtu yamekiukwa kwa namna mbaya sana,  mfano wa utoaji wa bimba na kuondolea mbali wagonjwa masuala ambayo ni mabaya sana yanayofanya kudumbukia katika utamaduni wa kifo. Ni lazima kuchuchumalia mantiki mpya ya kimaadili ulimwenguni, yenye kuwa na  umakini wa mada ya kazi ya uumbaji na maisha ya binadamu. Ubinadamu huo usichanganywe na aina yoyote ya kiitikadi na wala utashi wa nguvu, badala  uwe wa kindugu na mshikamano ili kuweza kuendelea na shughuli ya ulinzi wa maisha ya binadamu. Ndiyo msimamo mkuu ulitolewa na Baba Mtakatifu Francisko katika Barua yake aliyomtumia Rais wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya maisha, Askofu Mkuu Vincenzo Paglia  katika fursa ya kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo.

Jumuiya nzima ya kibinadamu

Tafakari ya Baba Mtakatifu inaanzia na jumuiya ya kibinadamu, kwa maana anasema,  inahitaji kukua kwa utambuzi wa pamoja juu ya uumbaji na upendo wa Mungu. Katika nyakati zetu, Baba Mtakatifu anandika, Kanisa linaitwa kutoa nguvu mpya ya ubinadamu wa maisha ambayo inataka kuvunja shauku hii ya Mungu kwa ajili ya kiumbe chake. Juhudi mpya ni za kufuata, kuhamasisha na kulinda maisha ya kila kiumbe inayochukua hatua hiyo ya upendo upeo wa Mungu. Ni uzuri na uvutio wa Injili ambayo haiwezi kupunguzwa kamwe upendo wa jirani na kuuweka katika mantiki za kiuchumi na kisiasa  hata katika baadhi ya mkazo wa mafundisho au maadili ambayo yanafuata aina fulani ya kiitikadi.

Historia ya Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya maisha iliundwa tarehe 11 Februari 1994

Ni upendo mkubwa ambao uliweza kufikia hatua ya kuanzisha Taasisi ya Maisha tangu miaka 25 iliyopita ambapo ni kunako tarehe 11 Februari 1994 kwa utashi wa Mtakatifu Yohane Paulo II kwa kufuata ushauri wa Mtumishi wa Mungu na mwanasayansi, Jérôme Lejeune ambaye aliweza kuamini mabadiliko na kujikita katika matendo katika kambi  ya madawa na alikubali kusaidia wajibu  wake kwa muundo kama huo. Taasisi wa maana hiyo iliweza kuendeleza tafiti na mafunzo ili kuweza kuonesha kuwa sayansi na teknolojia vikiwekwa katika huduma ya binadamu na haki zake msingi vinachangia wema fungamani wa binadamu na kuendeleza mipango ya Mungu ya wokovu. Baba Mtakatifu anakumbusha hayo akitaja hata Motu Propiro ya Vitae mysterium iliyounda Taasisi hiyo kwa dhati.

Hata hivyo baada  ya kushughulikia Katiba mpya iliyotolewa tarehe 18 Oktoba 2016, imeweza kupyaisha mwamko wa shughuli hizo kwa lengo la kufanya  iwe wazi juu ya mada makini zaidi kwa mantiki ya sasa, ambayo kutokana na kukua kwa njia za ubunifu na teknolojia ya sayansi na utandawazi mwingi, kwa upande mwingine, kati ya tamaduni, dini, uelewa tofauti na kwa upande mwingine  kati ya ukuu wa familia ya kibinadamu na nyumba yetu ya pamoja, ambayo binadamu anaishi. Baba Mtakatifu Francisko kuhusiana na hilo pia alikumbusha wakati wa hotuba yake katika Mkutano Mkuu wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya maisha, tarehe 5 Oktoba 2017 kwamba, kuigwa kwa mwenendo wa dhati wa hadhi ya binadamu unatazama kinadharia na kimatendo katika sayansi na kiteknolojia  ili kuwekwa pamoja hata kwa ugumu wake kwenye mahusiano ya maisha na wakati huo huo kuna maana na thamani yake.

Kuzuia utamaduni wa utofauti

Katika Barua iliyotumwa kwa  Askofu Mkuu Paglia, Baba Mtakatifu anaonesha wazi kwamba katika kipindi hiki utafikiri kinazidi kupanuka  zaidi kati ya upendeleo wa kuwa na ustawi binafsi, furaha ya ubinadamu wa kushirikishana hadi kufikia kufikiri kwamba kati ya jumuiya binafsi ya kibinadamu na sasa upo mchakato wa kweli wa mafarakano. Anaonesha hayo kama alivyokuwa amekwisha elezea zaidi katika mwanga wa Laudato Si, mahali ambapo anasema: “kuna hali ya dharura, mahali ambapo kuna haja ya  uhusiano wetu na historia ya dunia na watu. Ukosefu wa uelewa kwa suala la umoja wa familia ya wanadamu na wakati wake endelevu, mamlaka ya nguvu za kidunia, mgawanyiko na vita na inazidi kuongezeka duniani kote. Ni zaidi ya utamaduni mmoja, kwa namna  hiyo ni kuzuia utamaduni wa jumuiya ya kutojali, au kuhusishwa suala la kupendelea  fedha.

Kinyume cha maendeleo

Katika hali hizo, Baba Mtakatifu anaonesha, kwamba wakati rasilimali za kiuchumi na teknolojia zinazopatikana zingewezesha kutunza huduma ya kutosha ya nyumba yetu ya  familia ya kibinadamu na kumbe ni kutokana na  rasilimali hizi ambazo zinaleta migawanyiko yetu zaidi na ukali na ambayo ndiyo jinamizi kubwa na kwa namna hiyo watu wanahisi upungufu wa kiroho. Kwa maana ya kusema ni kuweka maisha pembeni mwa  dunia au jamii  kwa upendo huo na kuwa na tabia ya kudhoofisha kwa kina hali hiyo, kwa kujitafutia njia potofu na kipofu cha kufurahia vitu tu.Baba Mtakatifu anahimiza kwamba, tunapaswa kutambua kwamba wanaume na wanawake wa nyakati zetu  mara nyingi wameharibiwa na kwamba sisi  sote ni kama tumejikunja sisi binafsi  katika mfumo wa fedha na itikadi za matumizi ya hovyo katika kuchagua mahitaji yetu na kuendesha ndoto zetu, bila kujali uzuri wa maisha ya kushirikishana pamoja na uwezekano wa kuishi katika nyumba ya pamoja.

Tusichanganye ubinadamu na itikadi za utashi wa nguvu

Kadhalika anasema Baba Mtakatifu kuwa mtu mkristo anaalikwa kusikiliza kilio cha mateso ya watu. Mtazamo mpya wa maadili ya ulimwengu wenye kuwa makini na kuzingatia  mada za uumbaji na maisha ya  binadamu, ndilo  lengo ambalo tunapaswa kuzingatia kwa ngazi ya kiutamaduni. Hatuwezi kuendelea katika njia yenye makosa iliyofuatwa kwa miongo tangu kuundwa kwa ubinadamu, na wala kuchanganyikiwa na aina yoyote  ya itikadi katika matashi ya nguvu. Lazima tupinge aina hizi za kiitikadi zinazojitokeza na kupata hata msaada wa soko na teknolojia kwa ajili ya ubinadamu. Utofauti katika maisha ya mwanadamu ni mzuri kabisa na ambao anastahili kufuatwa kimaadili, kwa ajili ya thamani ya kuhudumia viumbe vyote. Kashfa iliyopo kiukweli ni kwamba, ubinadamu hunapingana wenyewe, badala ya kuwa na msukumo kutokana na tendo la upendo wa Mungu.

Baba Mtakatifu Francisko anatoa ushauri wa  Kanisa kama mstari wa mbele wa kutafuta uzuri huo  ambao unaigwa na kuwa sehemu yake kwa kupyaisha na shauku kubwa. “Tunatambua kuwa tumekutana na matatizo ya kujifungulia katika upeo wa kibinadamu hata katika umbu la Kanisa”. Ni lazima tujiulize sana kama tumefanya vya kutosha kutoa mchango wetu maalum kama Wakristo kwa maono ya mwanadamu anayeweza kuunga mkono umoja wa familia ya watu katika mazingira ya kisasa na ya kiutamaduni. Au hata kama tumepotea kuona hali halisi msingi badala yake tumeweka mbele matarajio yetu binafsi ya kiroho juu ya utawala wa jiji la kidunia, kujifungia yenyewe na mali zake, kwa kuhudumia jumuiya mahalia  iliyoofunguka  katika ukarimu wa kiinjili kwa masikini na wenye kuwa na mahangaiko.

Ubinadamu uwe wa kindugu na mshikamano

Kwa upande wa Baba Mtakatifu anasema sasa ni  wakati wa kufufua maono mapya ya udugu kibinadamu na mshikamano wa  ubinadamu na mtu binafsi na watu. Imani na shughuli za kindugu kwa kiumbe mwanadamu inapatikana  kwa sababu ya kutambua kuwa maisha ni kama mapambano yasiyo na mwisho na jambo jingine ni kutambua familia ya kibinadamu kama ishara ya nguvu ya Mungu Baba. Njia zote za Kanisa kwa dhati zinapelekea ubinadamu kama alivyokuwa ameonesha wazi hata Mtakatifu Yohane Paulo II na Mtakatifu Paulo VI.  

BARUA YA PAPA
15 January 2019, 16:06