Tafuta

Vatican News
Kwa ujasiri tujifungulie katika mwanga wa upole na unyenyekevu wa Yesu na kama Mamajusi tutaweza kuhisi furaha kubwa na ambayo hatuwezi kamwe kuhifadhi kwa ajili yetu Kwa ujasiri tujifungulie katika mwanga wa upole na unyenyekevu wa Yesu na kama Mamajusi tutaweza kuhisi furaha kubwa na ambayo hatuwezi kamwe kuhifadhi kwa ajili yetu   (ANSA)

Papa:Kama Mamajusi tufungue mioyo katika mwanga ambao ni Yesu!

Tafakari ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican tarehe 6 Januari 2018, wakati Mama Kanisa anaadhimisha sikukuu ya Epifania, Papa anasema kuwa hata sisi kama Mamajusi tuache tuangazwe na mwanga wa Kristo ambao unatoka Bethlehemu. Tusiruhusu hofu zetu za kufunga mioyo na tuwe na ujasiri

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Leo ni sikukuu ya Epifania ya Bwana na ni sikukuu ya maonesho ya Yesu anayewakilishwa na mwanga. Katika masomo ya kinabii mwanga huo ni ahadi na kwa dhati  Isaya anaelekeza Yerusalem kwa meneno haya: “Inuka na jufunike na mwanga, kwa sababu mwanga utachomoza kwa ajili yako, utukufu wa Bwana  utaonekana kwako” (Is 60,1). Mwaliko wa nabii unashangaza kwa sababu unajitokeza katika kipindi maalumu hasa siku moja kabla ya watu kurudishwa  makwao na  katika matukio mengi ambayo watu hao walikuwa wamefanya uzoefu.

Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa sala ya Malaika kwa Bwana kwa mahujaji na waamini wote waliokusanyika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro, wakati Mama Kanisa anadhimisha Sikukuu ya Epifania yaani tokeo la Bwana tarehe 6 Januari 2019. Akiendelea na tafakari hiyo anathibitisha kuwa, leo huo ni mwaliko unaotolewa kwetu sisi tunaoadhimisha Noeli ya Yesu na kututia moyo ili tuweza kuacha na kujengelea mwanga wa Bethlehemu. Hata sisi sote tunaalikwa kutotazama ishara za kijujuu tu matokeo mbalimbali, badala yake ni  kuanza safari katika mchakato wa mapya ya maisha safari yetu kama watu waamini.

Yesu ni mwanga na alizawaliwa katika mji wa Daudi

Mwanga ambao Nabii alikuwa ametangaza na katika Injili unawalikilishwa na pia  kukutana. Yesu alizaliwa huko Bethlehemu katika mji wa Daudi na alikuja kuleta wokovu kwa walio karibu na mbali. Mwinjili Matayo anaoneshaaina hiz tofauti za kukutana na Kristo katika kujikitaka kwenye hali ya uwepi wake. Kwanza Herode na waandishi wa Yerusalemu walikuwa na moyo mgumu na kukataa kumwona mtoto. Watu wa aina hiyo Baba Mtakatifu Francisko anasema, wanawakilisha wale wote hata katika nyakati zetu, watu wenye kuwa na hofu ya kuja  kwa Bwana na wanafungia mioyo yao ndugu kaka na dada wenye kuhitaji msaada. Herode anaogopa kupoteza madaraka na wakati huo ho hafikiri hata wema wa kweli wa watu, badala yake ni ubinafsi tu. Waandishi na viongozi wa watu wanaogopa kwa sababu hawajuhi kutazama upeo zaidi  badala yake ni kuwa na uhakika wao binafsi na ndiyo maana hawawezi kupokea mapya ambayo ni Yesu.

Zawadi  za Mamajusi

Tofauti ya uzoefu wa Mamajusi ( taz (Mt 2,1-12)ni kwamba  hawa walikuja kutoka mashariki ya mbali, wakiwakilisha watu wote walio mbali na imani ya utamaduni wa kiyahudi : Licha ya hayo waliacha waongozwe na nyota na kukabiliana na safari ndefu na hatari  hatari ya kutofika na kujua ukweli wa Masisha. Walikuwa wamejifungulia mapya na kwa maana hiyo walioneshwa yaliyo makuu na mshangao mpya wa historia. Mungu alijifanya mtu. Mamajusi walimshudia Yesu na kumtolea zawadi muhimu ya dhahabu, uvumba na manemane. Hiyo ni kutokana na kwamba anayemtafuta Bwana si kwamba anavumlivu wa safari ndefu, bali hata kuwa na ukarimu wa moyo na hivyo hatimaye Mamajusi walirudi katika nchi yao ( Mt 2,12) wakiwa wamejazwa ndani ya moyoni mwao fumbo la yule Mfalme mnyenyekevu na maskini; Baba Mtakatifu anaongeza kusema kuwa, tunaweza kufikiria kuwa  hawa walipata kusimulia uzoefu walioupata wa wokovu unaotoka kwa Mungu kwa njia ya Kristo ya kwamba ni kwa ajili ya wote wawe  wa karibu na mbali. Na ni wokovu ambao siyo rahisi kuumiliki na mtoto, badala yake yeye ni zawadi kwa watu wote.

Walipitia njie nyingine

Injili inasema walipita njia nyingine, Baba Mtakatifu  anafafanua kuwa kila mmoja wanaume na mwanamke anayekutana na Yesu anabadili njia na kurudi katika maisha tofauti, anajipyaisha katika njia nyingine na ndiyo maana walirudi katika nchi yao. Hata sisi tuache tuangazwe na mwanga wa Kristo ambao unatoka Bethlehemu. Tusiruhusu hofu zetu za kufunga mioyo, bali kuwa na ujasiri wa kujifungulia mwanga wa upole na unyenyekevu. Kwa njia hiyo kama Mamajusi tutaweza kuhisi furaha kubwa ( taz Mt 2,10), ambayo hatuwezi kamwe kuhifadhi kwa ajili yetu. Na Bikira Maria awe ndiye msaada wetu katika safari ya kuona nyota ambaye inatufikisha kwa Yesu.

06 January 2019, 13:30