Tafuta

Vatican News
Tarehe 31 Desemba 2018, Papa ameadhimisha masifu ya jioni katika Mkesha wa Sikukuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu Tarehe 31 Desemba 2018, Papa ameadhimisha masifu ya jioni katika Mkesha wa Sikukuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu  (ANSA)

Papa:Hata leo hii kuna mitindo isiyostahili ya utumwa!

Tarehe 31 Desemba 2018 saa 11 jioni massa ya Ulaya Baba Mtakatifu Francisko ameadhimisha masifu ya kwenye mkesha wa sikukuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu na kutakafari hali halisi ya sasa ya utumwa hata katika mji wa Roma. Baada ya masifu alitembelea maeneo ya huduma kwa watu wasio kuwa na makazi, hata kituo cha afya na baadaye katika pango na kusali

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 31 Desemba 2018 saa 11 massa ya Ulaya Baba Mtakatifu Francisko ameadhimisha masifu ya jioni kwenye mkesha wa sikukuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu. Katika mahubiri ya Baba Mtakatifu mara baada ya Somo kutoka Kitabu cha Mtakatifu Paulo (taz Gal 4,4-5), anasema kuwa katika mwisho wa mwaka Neno la Mungu linatusindikiza kwa maneno mawili ya Mtakatifu Paulo ya dhadi na nguvu. ambayo ni ufupisho wa Kitabu cha Agano jipya inayotoa maana ya kipindi kigumu na daima katika kila  hatua ya mwaka.

Neno linalojikeza kwa nguvu ni utimlifu wa nyakati, lakini huo ni upendo unaotoa ukamilifu wa kila kitu na Yesu anajikita katika upendo ambao Mungu anamwilisha kila binadamu; yeye anazaliwa ili kumwokoa na kumtoa katika hali ya utumwa na kumrudishia uhuru na hadhi yake. Baba wa mbingu alizaliwa na mwanamke ili sisi tuweze kupokea utimilifu wa ubinadamu wetu. Kuinama chini kwake umetuwezesha sisi kuinuliwa juu, kwa ajili ya  udogo wake, sisi tumekuwa na ukuu. Katika udhaifu wake ndiyo imekuwa nguvu yetu; Kwa kujifanya mtumishi, sisi tumekuwa na uhuru Baba Mtakatifu amethibitisha.

Uchungu wa sasa wa mtindo wa utumwa

Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari yake anaendelea kuonesha utambuzi alio nao wa hali halisi ya mwaka huu unaoisha na  uchungu ambao umetanda leo hii katika hali nyingi za utumwa na zisizo stahili hasa zinazowakumba wanaume na wanawake hata katika mji wa Roma. Kufuatia na hali hiyo Baba Mtakatifu amefikiria watu wasio kuwa makazi. Ni zaidi ya watu elfu kumi na kwamba, wakati wa kipindi cha baridi hali ni ngumu zaidi. Hawa wote ni wana wa Mungu, lakini katika mitindo mbalimbali ya utumwa na wakati mwingine ni nzito ambayo imewafikisha kuishi katika hali isiyo na hadhi.

Hata Yesu alizaliwa katika hali kama ile baba Mtakatifu anabainisha na  kuongeza kusema, lakini si kwa bahati mbaya au ajali, kwa maana alipenda iwe hivyo mwenyewe na ili  anaoneshe ushiriki wa upendo wa Mungu kwa ajili ya wadogo na maskini na ili kuweza kupanda mbegu duniani ya ufalme wa Mungu wa haki, makao na amani, mahali ambamo hakuna yoyote awe mtumwa, bali wote wawe ndugu na wana wa Mungu mmoja.  Hii ni hali halisi ambayo Mama Kanisa haitaki kuwa na mtazamo wake kwa urahisi tu Baba Mtakatifu anaongeza, kwani  Kanisa linataka kukaa ndani na kuwa na ukaribu wa watu hawa na hali hii kama Bikira Maria alivyokaribisha na kukumbatia Mwana wa Mungu.

Utimilifu wa nyakati

Mtakatifu Francisko katika tafakari yake pia ameweza kujikita kutazama juu ya utimilifu wa nyakati na kusema, “Yesu ambaye siku chache tumeadhimisha kuzaliwa kwake, ni nyota iliyo ngani. Kwa hakika kwa sasa haionekani na aina maana, lakini kwa muda karibia kwa miaka therathini, Yesu alifungua nguvu ambayo ilikuwa haijawahi kusikika na ambayo ipo na itadumu katika historia yote. Nguvu hiyo inaitwa upendo. Upendo unatoa ukamilifu wa kila kitu hata katika nyakati, Yesu amejikita katika upendo wote wa Mungu na wa kuwa binadamu.

Yesu anavunja vunja minyororo ya dhambi

Utume wa Mwana wa Mungu ni ule wa kumkomboa mwanadamu na kumrudishia uhuru wake. Utumwa ambao Mtakatifu Paulo anasisitiza katika somo ni ule wa kufuata amri na ambayo inamwelimisha mtu, japokuwa haimwondolei uhuru wa hali yake ya kidhambi, kinyume chake anasema inamfunga na kumzuia kufikia uhuru wa kuwa mwana. Mungu Baba alimtuma Mwana wake mzaliwa wa kwanza ili aweze kuondoa katika moyo wa mtu utumwa wa kizamani wa dhambi na kumrudishia hadhi yake. Katika moyo wa binadamu kwa dhati, kama anavyofundisha Yesu katika Injili ( Mk 7,21-23) ndimo yanatoka mawazo yote mabaya ambayo yanaharibu maisha na uhusiano mwema.

Baba Mtakatifu amepitia katika kituo cha afya na kusimama katika pango

Kabla ya kuanza wimbo wa shukrani Te deum kwa mwaka unaoisha wa kawaida, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, wameweka Ekaristi Takatifu na kuabudu. Na mara baada ya maadhimisho ya liturujia ya masifu na shukrani (Te deum), Baba Mtakatifu Francisko akiwa amesindikizwa na Kardinali Konradi Krajewski Msimamizi wa sadaka ya Papa Vatican, wamekenda katika maeneo ya watu wasio kuwa na makazi kutazama bafu na vyoo, saloon na kituo cha afya kilichofunguliwa hivi karibuni katika nguzo ya Bernin mjini Vatican.  Na baada ya kuwasalimia watu waliokuwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu amesimama mbele ya Pango iliyotengenezwa kwa mchanga na kusali kidogo kabla ya kurudi katika makao yake katika nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican.

01 January 2019, 09:58