Ufunguzi wa Wiki ya Kuombea Umoja wa Wakristo tarehe 18 Januari 2019 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Roma Ufunguzi wa Wiki ya Kuombea Umoja wa Wakristo tarehe 18 Januari 2019 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Roma 

Papa Francisko anawaalika wakristo wote kushirikishana mema itokayo kwa Mungu!

Katika ufunguzi wa Wiki ya kuombea Umoja wa Wakristo,tarehe 18 Januari 2019 Jioni, Baba Mtakatifu Francisko anasema kuwa kila mmoja anategemea huruma ya Mungu nakila mmoja abaalikwa kushirikishana na wengine mema yatokanayo na Mungu. Umoja wa Wakristo ni tunda la neema ya Mungu na sisi lazima tuwe tayari kupokea kwa moyo wa ukarimu

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Leo hii inaanza Wiki ya kuombea umoja wa wakristo, ambapo tumealikwa sisi sote kusali kwa Mungu atujalie zawadi kubwa hii. Umoja wa Wakristo ni tunda la neema ya Mungu na sisi lazima tuwe tayari kuopokea kwa moyo wa ukarimy na uwezekano. Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Maombi kwa ajili ya Umoja wa Kristo wakati wa amaadhimisho ya masifu ya jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Roma tarehe 18 Januari 2019. Baba Mtakatifu amethbitisha kuwa na furaha ya kuweza kusali pamoja na wawakilishi wa makanisa mengine yaliyopo mjini Roma na ambao amewasalimu kwa salam ya kindugu. Hata kuwasalimia wawakilishi wa kiekumene kutoka nchi ya Finland, wanafunzi wa kiekumene wa Chuo cha Bossey, wakiwa katika ziara yao mjini Roma ili kujifunza na kuwa na uwelewa wa kina juu ya Kanisa Katoliki na vijana wakirotodhox wa nchi za Mashariki ambao wanasoma kwa msaada wa Tume ya ushirikiano wa Utamaduni na Makanisa ya Kiorthodox yanayofanya shughuli zake katika Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Wakristo.

Musa anawafundisha waishi kwa uaminifu na haki mara watakapofika nchi ya ahadi

Katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati, kinafikiria  watu wa Israeli waliokuwa wamekimbilia katika uwanda wa Moab, kabla ya kuingia katika Nchi ya Mungu ya ahadi. Hapo Musa kama baba mwema na kongozi aliyechaguliwa na Bwana anarudia kusoma Sheria kwa watu, na anawafundisha na kuwakumbusha kuwa wanapaswa waishi kwa uaminifu na haki mara tu wanatakapokuwa wamewadia katika nchi ya ahadi. Somo ambao limesikika linatoa maelezo jinsi gani ya kuadhimisha sikukuu tatu msingi za mwaka Pesach (Pasaka), Shavuot (Pentekoste), Sukkot (Tabernakulo). Kila moja ya sikukuu hii inatoa wito kwa wanasraeli kuwa na shukrani kwa mema yote waliyopokea kutoka kwa Mungu. Maadhimisho ya sikukuu inawataka ushiriki  wa watu wote. Hakuna ambaye anabaguliwa: kwa maaana “utafurahi mbele ya Bwana Mungu wako, wewe na kijana na msichana wako , mtumwa na mjakazi wake, Mlawi ambaye anaishi katika miji yako, mgeni, yatima na mjane wote watakuwa katikati yako ( Kumb 16,11.

Katika kila siku kuu inahitajia kufanya hija mahali ambapo Bwana anataka kukaa kwa jina lake

Kila sikukuu inatahitaji kufanya hija katika mahali ambapo Bwana ameamua kukaa kwa jina lake ( Kum 16,2)  Pale mwisareli mwaminifu lazima ajiweke mbele ya Mungu. Licha ya wasreli kuwa watumwa huko Misri, bila kuwa na mali binafsi , lakini hakuna atakayewakilishwa mbele ya Bwana akiwa mikono mitupo ( Kum 16,16) na zawadi ya kila  mmoja itapimwa kwa baraka ya Bwana ambayo atakuwa amempatia. Wote kwa dhati watapokea shemu yao ya utajiri wa nchi na ambayo inatokana na wema wa Mungu. Hiyo isishangaze kufuatia na sura za kibiblia katika hatua za maadhimisho katika sikukuu za aina tatu msingi kwa kutamkia waamuzi. Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa sikukuu hizo zinatoa ushauri kwa watu kuwa na haki na kuwakumbusha juu ya usawa , msingi kati ya wajumbe wote na kwamba wote wanategemea na huruma ya Mungu na kuwaalika kila mmoja ashirikishane na wengine mema aliyopokea. Kutoka shukrani na kusifu  Bwana katika mwaka ni sawa na hatua ya kushukuru kwa sababu ya kumsaidia hasa aliye karibu, mdhaifu na mwenye kuhitaji

Watu wa Indonesia wametafakari mada inayoongoza Wiki ya Maombi, lakini pia hata dunia nzima inaishi katika hali hiyo

Baba Mtakatifu  Francisko akiendelea na tafakari yake anasema, wakristo wa Indonesia wakitafakari juu ya mada iliyochaguliwa kuongoza Wiki ya Maombi  wametoa uamuzi wa kujikita katika maneno ya Kitabu cha Kumbumbu ya Torati kuhusu haki na kufuata haki hiyo tu ( Kumb 16,20) Kwa njia yao wasiwasi ni hai ambao wanaona kila wakati kungezeka kukua kwa uchumu katika nchi ni mdogo lakini kutokana na kufuaa mantiki za kisasa, za kuacha walio wengi katika umasikini na utajiri kwa walio wachache tu. Hii inasababisha na myumbo wa maelewano katika jamii ambamo watu wengi wa makabila rangi, lugha na dini wanaishi kwa pamoja na kushirikishana maana ya wajibu wa pamoja. Baba Mtakatifu akifafanua zaidi juu ya hali hasi ya Indonesia, amebainisha kuwa, hali halisi hiyo lakini inaikumba hata dunia nzima. Iwapo jamii haina tena msingi wa mshikamano na wema wa pamoja, kwa maana ya kuona kashfa za watu wanaoishi na umasikini wa kukithiri karibu na majumba makuu na marefu ya kifahari, au hoteli makubwa  na vituo vikubwa vya kibiashara, ambayo ni ishara ya utajiri wa kutisha! Tumejisahau hekima ya sheria ya Musa ambapo kwa mujibu wake inasisitiza kuwa utajiri usio shirikishwa jamii inagawa jamii hiyo.

Mtakatifu akiwaandikia warumi, anagusia mantiki hiyo kwa jumuiya za kikristo

Mtakatifu Paulo akiwaandikia warumi, anajaribu kutoa mantiki sawa na hiyo  katika jumuiya ya kikristo. Wenye nguvu lazima wahangaikie wadhaifu. Siyo mkristo anayejipendelea mwenyewe binafsi (Rm 15,1). Kwa kufuata mfano wa Kristo, Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, lazima kujitahidi kuwainua wale walio wadhaifu. Mshikamano na uwajibikaji wa pamoja ndiyo lazima uwe sheria ambayo ni nguzo ya familia ya kikristo. Kama watu wa Mungu hata sisi daima tupo kilele cha ncha ili kuingia katika Ufalme alioahidi Bwana. Lakini kwakuwa tumegawanyika, kuna ulazima kwanza wa kukumbuka mwaliko juu ya haki ambao umetolewa na Mungu. Hata kati ya wakristo, Baba Mtakatifu anabainisha , kuna hatari ya kuonekana mantiki inayojulikana kwa waisraeli wa wakati ule wa zamani, lakini hata kama  watu wengi ambao wameendelea hata sasa, ambao katika nia yao ya kukusanya na kurundika utajiri wanawasahau wadhaifu na wenye kuhitaji. Ni rahisi sana kusahau usawa ambao ni msingi na upo kati yetu, kwa maana unatokana na asili ya kuwa wote tu watumwa wa dhambi na ambao Bwana alitukomboa kwa njia ya ubatizo na kutuita watoto wake.

Iwapo tunadharau wengine na neema tuliyopewa inageuka kisima cha kiburi, je tunawezaje kuingia mbinguni?

Baba Mtakatifu Francisko anabainisha kuwa ni rahisi kufikiria kuwa neema ya kitasaufi tuliyopewa ni miliki yetu,na kwamba  jambo ambalo hilo tunastahili. Kuna uwezekano pia kwamba zawadi tulizopokea kutoka kwa Mungu zinatufanya tuwe kipofu cha zawadi walizopewa hata wakristo wengine. Hii ni dhambi kubwa Baba Mtakatifu amesisitiza, hasa ya kupunguza au kudharau zawadi ambazo Bwana amewajalia ndugu wengine, kwa kuwaona kuwa wao ni wenye kuwa na bahati mbaya kwa Mungu. Iwapo sote tunamwilishwa sawa na mawazo na kuruhusu kuwa neema hiyo tuliyoipokea inageuka kuwa kisima cha kiburi, ukosefu wa usawa na migawanyiko: Je ni kwa njia zipi tunaweza sasa kuingia katika Mbingu ya ahadi?

Wakristo waliopyaishwa na kutajirishwa na ushirikishano wa  zawadi watakuwa na uwezo wa kutembea hatua thabiti kuelekea umoja

Utamaduni ambao unaonesha Mbingu ni utamaduni ambao unataka haki, ni sikukuu ambayo inawaunganisha wote, katika sikukuu ambayo inaonesha wazi zawadi tulizopokea zipo na zinashirikishwa. Kwa kutimiza hatua za mwanzo kuelekea nchi ya ahadi na ambayo ndiyo umoja wetu,awali ya yote lazima kujitambua kwa unyenyekevu kwamba  baraka ambayo tumeipokea  siyo ya haki yetu , bali ni kwa ajili ya zawadi yetu na ambayo tumepewa ili kuweza kushirikishana na wengine. Na kwa upande mwingine, Baba Mtakatifu anasema, lazima kutambua thamani ya neema waliyopewa hata jumuiya nyingine za kikristo. Na matokeo yake yatakuwa ni shauku ya kushiriki katika zawadi nyingine. Wakristo waliopyaishwa na kutajirishwa na ushirikishano wa zawadi watakuwa ni watu wenye uwezo wa kutembea hatua kwa hatua thabiti na imani katika njia inayopelekea umoja.

 

18 January 2019, 19:00