Tafuta

Vatican News
Papa Francisko anaswashukuru kwa shughuli ya vikosi vya ulinzi na usalama mjini Vatican ambayo inajulikana na uwezo kitaaluma, hekima ya kukabiliana na hali tofauti hata zile ngumu Papa Francisko anaswashukuru kwa shughuli ya vikosi vya ulinzi na usalama mjini Vatican ambayo inajulikana na uwezo kitaaluma, hekima ya kukabiliana na hali tofauti hata zile ngumu  (Vatican Media)

Ombi la Papa kwa vikosi vya usalama ni kulinda hata mizizi ya utamaduni!

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 17 Januari 2019, amekutana na vikosi vya Polisi na viongozi wengine wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama mjini Vatican. Kati ya sifa na maombi kwao ni ile ya ulinzi wa mizizi ya utamaduni, ambayo inaashiria kung’oka.kuna utambuzi kwamba bila kuwa na mizizi siyo rahisi kukua na mti unatoa maua kutokana na mizizi iliyopo ndani ya ardhi

Sr. Angrela Rwezaula -Vatican

Tarehe 17 Januari 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na vikosi vya Polisi na viongozi wengine wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama mjini Vatican. Wakati wa hotuba yake amewashukuru kwa fursa hiyo ambayo ni ya utamaduni na kwamba inampatia fursa ya kuweza kutoa shukrani zake kwao katika  huduma yao  wanayoitoa katika Makao Makuu ya Kitume na mjini Vatican. Kwa namna ya pekee ameshukuru hotuba ya Mkuu wa Polisi aliyosoma kwa niaba ya wote na kumpa heri nyingi Rais Felice Colombani na Mkuu mwingine  Luigi Carnevale wakiwa wote wawili kwa siku chache zilizopita wamepewa madaraka ya uongozi. Kadhalika kwa wote amewatakia matashi mema ya dhati ya mwaka mpya ili uwe na utajiri wa thamani ya kibinadamu na kikristo kwa kuwezesha kuleta matunda mema ya kuishi.

Siku kuu ya Noeli na Epifania zilizoadhimishwa hivi karibuni, Baba Mtakatifu amesema zimetuwezesha kutafakari kwa mara nyingine tena juu ya kuzaliwa kwa Bwana na kuonesha kwake Kristo katika dunia hii. Kuja kwake kati yetu kunaonesha ule ukaribu wa Mungu kwa ajili ya binadamu na upendo usio kifani kwa ajili yetu. Uwepo wake unatoa maana ya maisha yate na kutoa chachu ya matumaini, kusaidia kuinua mtazamo zaidi ya upeo wa matatizo na magumu ya kila siku. Na wakati huo huo, unatusukuma katika upendo wa kuweza kuishi katika uhusiano kwa mtindo wa kindugu na huruma hasa kwa watu ambao wanateseka kwa magonjwa na walio baguliwa pembezoni.

Mtindo wao wa ukaribu wa watu kwa mfano ndiyo hata kazi yao na ambayo wao wanao uwezekano wa kushuhudia kila siku. Na kwa ajili ya wito wao, hawa ni watu maalum wa ukaribu, Baba Mtakatifu  anaendelea  kuwashukuru kwa shughuli hiyo yenye thamani ya kulinda na kuweka utaratibu wa umma, mahujaji, watalii ambao wanatoka kila kona ya dunia ili kufika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, na wanarahisisha matembezi yao. Kwa ujumla shughuli yao anasema inajulikana na uwezo  wao kitaaluma, hekima ya kukabiliana na hali tofauti hata zile ngumu; na kwa hizo Baba Mtakatifu anawapongeza kwa dhati. Aidha anapenda kupongeza uwezo wao wa kiufundi na ukarimu. Anawashuru waendelee kuchuchumalia kutafuta ubora wa mtindo wa shughuli yao kwa kujibidisha kuwapokea wote kwa uvumilivu na uelewa, hata kipindi ambacho wanahisii kweli uchovu au mzigo mzito wa hali isiyopendeza.

Huduma yao ya kila siku ni uso angavu wa kila siku na usiku katika Uwanja wa Mtakatifu Petro na maneo yote ya Vatican, Baba Mtakatifua amefafanua kuwa wao wanakaa katika maeneo yao, pamoja na hali ya hewa yaani iwe nzuri au isiyo nzuri. Akifikiria utayari wao na roho ya sadaka anapatwa mashangao pia simanzi na hata amethbitisha kwamba  kidogo aibu,kwani akifikiria mara nyingi watu ambao wanajiita wakristo wakati mwingine hawatoi mifano mizuri mbele yao. Hawezi pia kusahau hata ushirikiano mwafaka wakati wa ziara zake katika Maparokia na kwenda katika Jumuiya nyingine za Roma au kama vile fursa nyingine za ghafla anazozifanya katika sehemu mbalimbali za Italia. Kwa hayo yote Baba Mtakatifu anawapongeza na kuwa na utambuzi mkuu!

Baba Mtakatifu amegusia juu ya Hotuba ya Mkuu wa Polisi alivyozungumza juu ya maana ya uwajibikaji na kwamba ipo hatari ya kuupoteza katika jamii hii. Wao kama walinzi wa Uwanja wa Mtakatifu Petro, walinzi wa ziara zake, walinzi wa mambo mengi, kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anawaomba wafanye jambo moja hasa la kujibidisha katika jitihada za ulinzi wa mizizi ya utamaduni wa mji, wa taifa na utumaduni. Ustaarabu huu upo hatari ya kung’oka mizizi yake anasema Baba Mtakatifu na kuwa, upo utambuzi kwamba bila kuwa na mizizi siyo rahisi kukua, na mti unatoa maua kutokana na rutuba na mizizi iliyopo ndani ya ardhi (Rej F.L. Bernardez, Para recobrar). Baba Mtakatifu anawasihii wajibidishwa kwa hali na mali katika kulinda mizizi kwa sababu, ni mizizi inayotoa utambulisho. Utambulisho wao ni ule wa leo hii, lakini pia unatokana na mizizi iliyopita  na utaendelezwa kwa watoto wao na wajikuu, lakini daima unatokana na mizizi. Baba Mtakatifu anashukuru iwapo watafanya hivyo!

Ameitiisha kwa kuwakabidhi katika maombezi ya Bikira Maria Mtakatifu. Yeye aweze kuwa karibu nao katika kazi na kusaidia familia zao na ambapo amewatumia ujumbe maalum hasa wa kusali kwa ajili yake. Amewatakia heri ya Mwaka Mpya na kuwabariki kwa Baraka Takatifu ya kitume.

17 January 2019, 16:10