Tafuta

Vatican News
Sikukuu ya Epifania ya Bwana tarehe 6 Januari 2019 Sikukuu ya Epifania ya Bwana tarehe 6 Januari 2019  (Vatican Media)

Misa ya Papa Epifania:Mungu anajionesha mahali pa unyenyekevu!

Katika hitimisho la mahubiri ya Baba Mtakatifu wakati wa Misa ya Sikukuu ya Epifania iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro tarehe 6 Januari 2019 anasema katika kipindi hiki cha Noeli inayo karibia mwisho wake, tusipoteze fursa kwa ajili ya kutoa zawadi kwa Mfalme wetu, aliyekuja kwa ajili wote na si katika jukwaa la tamasha na sikukuu za kidunia

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Neno Epifania linaonesha  tokeo la Bwana ambapo Mtakatifu Paulo katika somo la pili ( Ef 3,6) anasema kuwa, anajionesha kwa watu,kwa kuwakilishwa leo hii na Mamajusi. Anajifunua kwa namna hii nzuri ya uhalisia wa Mungu aliyekuja kwetu. Kila taifa, lugha na watu ambao amewapokea na kuwapenda. Na ishara hiyo ni mwanga ambao unafika mahali popote na kuangaza. Ndiyo mwanzo wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko, katika Sikukuu ya Epifania au tokeo la Bwana, wakati wa Misa Takatifu aliyoongoza katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, tarehe 6 Januari 2019.

Bado ni mshangao kwa jinsi Bwana alivyojionesha

Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri anafafanua kuwa iwapo Mungu wetu alijionesha kwa watu wote, lakini bado inabaki mshangoa kwa jinsi anavyojionesha. Katika Injili iyosomwa inaonesha kuingia na kutoka kwa kuzungukia Jumba la Mfalme Herode, wakati huo huo Yesu akitambulishwa kama Mfalme na Mamajusi waliouliza: “Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi( ( Mt 2,2)”. Watampata lakini siyo mahali walikuwa wanafikiria . Yeye hakuwa katika Jumba la Kifalme huko Yerusalem, lakini katika makazi ya kinyenyekevu huko Bethelehemu. Mfano huo ni sawa na uleambao ulikuwa unajionesha katika siku ya Noeli, wakati Injili inaelezea juu ya tangazo rasmi liliotolewa na Kaisari Augusto, kuwataka watu wote nchini kote wahesabiwe  wakati Kurenio alipokuwa mkuu wa mkoa wa Siria( Mt 2,2). Lakini hakuna watawala wa nguvu wa wakati ule walipata kutambua kuwa Mfalme wa historia alikuwa anazaliwa katika nyakati. Na hata baadaye Yesu alipokuwa na miaka therethini, alijionesha wazi kwa umma, akitambulishwa na mtangulizi wake Yohane Mbatizaji, ambapo Injili inatoa fursa ya kuwakilisha kwa mantiki hiyo, akiorodhesha watawala wa wakati huo, ambao walikuwa ni wa kidunia na kitasaufi, kama vile Tiberia Kaisari,Ponsio Pirato,Herode, Filipo,Lusana, Anas na Kayafa walikuwa ni makuhani wakuu.  Wakati huo ndipo neno la Mungu lilimjia Yohane kule jangwani. Kwa namna hiyo, hakuna mmoja wa wakuu hao bali ni mtu mmoja aliyekuwa amekwenda jangwani. Na ndipo hapo mshangao. Mungu hajipandishi katika mantiki ya dunia hii kwa ajili ya kijionesha Baba Mtakatifu amesisitiza!

Kishawishi za kuzungusha mwanga hata katika majumba ya watawala

Kwa kusikiliza orodha ya watu hao wakuu, Baba Mtakatifu anafafaua kuwa , inawezekana kukujia kishawishi cha kutaka kuzungusha mwanga juu yao. Na unaweza kufikiria,kuwa ingekuwa vema iwapo nyota ya Yesu ingeweza kutua hata Roma katika kilima cha Palatino mahali ambaoo Mfalme Augusto alikuwa anaishi na kutawala dunia; ufalme wote ungegeuka mara moja kuwa wa kikristo. Na zaidi iwapo mwanga ungeweza kuangaza jumba kuu la Herode, waliokuwa ndani mwake  wangeweza kufanya yaliyo mema badala ya mabaya. Lakini mwanga wa Mungu hauendi kwa wale ambao wanaangazwa na mwanga wao binafsi, Mungu anapendekeza , halazimishi; anaangaza, lakini hafumbishi. Kadhalika Baba Mtakatifu amebainisha kuwa, daima  kuna kishawishi kikubwa cha kuchanganya mwanga wa Mungu na ule wa dunia. Ni mara ngapi tumefuata taa za ulaghai wa utawala na nguvu, kwa kufikiria ni katika kutoa huduma ya Injili! Lakini tumezungusha mwanga katika upande wenye makosa, kwa sababu Mungu hakuwa mahali hapo. Mwanga wake mzuri unaangaza kwa upendo mnyenyekevu. Ni mara ngapi kama Kanisa tumejaribu kuangazwa na mwanga binafsi! Lakini sisi siyo jua la ubinadamu. Sisi ni mwezi ambao pamoja na vivuli vyake, vinaangaza mwanga wa kweli wa Bwana. Kanisa ni fumbo la mwezi ( “Mysterium lunae). Na Bwana ambaye ni mwanga wa dunia ( Yh 9,5). Ni yeye  na siyo sisi!

Mwanga wa Mungu unaangaza kwa yule anaye upokea. Nabii Isaya katika Somo la Kwanza  (60,2) Baba Mtakatifu anasisitiza anatukumbusha kuwa, mwanga wa mungu hauzuii giza na ukungu mzito kufunika ardhi nzima, lakini unaangaza kwa yule aliye tayari kuupokea. Kwa maana hiyo naabii anatoa mwaliko unaomhusu kila mmoja: “iinuka na uangazwe  maana mwanga unachomoza kwa ajili yako” ( 60,1). Baba Mtakatifu anabainisha kuwa inahitaji kuamka na kuondokana na kukaa, ili ujikite katika safari. Bila kufanya hivyo unabaki umesimama kama wale waandishi na wasulihishi wa Herode, ambao pamoja na kuwa na ufahamu vizuri mahali alipozaliwa Masiha, hawakuondoka.

Ni lazima kujivika mwanga wa Mungu ili Yesu awe nguo ya kila siku

Ni lazima kujivika mwanga ambao ni  Mungu kila siku ili Yesu aweze kuwa nguo ya kila siku. Lakini kwa kufavaa nguo ya Mungu ambayo ni rahisi kama mwanga, lazima hawali ya yote kuacha kujivika nguvo za kushangilia. Matokeo yake ni kufanya kama Herode ambaye badala ya kupenda mwanga wa Mungu alipendelea mwanga wa dunia hii wa utawala na kujulikana. Mamajusi kinyume chake, waliweza kukamilisha unabii, waliamka ili waweze kujivika mwanga. Wao wenye waliona nyota angani, lakini siyo waandishi wa Herode na wala mtu yoyote huko Yerusalemu. Ili kumpata Yesu, kuna ulazima wa kubadili njia tofauti, kuna haja ya kuchukua njia mbadala, njia yake ya upendo mnyenyekevu. Kuna haja ya kuhifadhi. Kwa hakika Injili ya siku inahitimisha ikisema kuwa, Mamajusi walimwona na Yesu na wakati wa kurudi kwao walipitia njia nyingine(Mt 2,12). Kupitia njia nyingne  na  tofauti na ile ya Herode. Baba Mtakatifu anasema, ni kutafuta njia  mbadala katika dunia kama ile ambayo ilipitiwa na wale awote ambao katika Noeli wako na Yesu. Maria na Yosefu na wachungaji. Hawa ni kama Mamajusi ambao waliacha makazi yao na kujiweka katika hija, katika njia za Mungu. Hiyo ni kutokananna kwamba, ni yule tu anaye acha mashiko ya ulimwengu huu na kujikita katika njia ya kutafuta fumbo la Mungu.

Inabidi kufanya hata sisi ili kukamilisha unabii

Baba Mtakatifu anasema haitoshi kujua Yesu amezaliwa wapi, kama waandishi iwapo huwezi kwenda huko. Haitoshi kujua kwamba Yesu amezaliwa, kama Herode iwapo hukutani naye. Iwapo mahali pake napageuka kuwa mahali petu, wakati wake, unageuka kuwa wakati wetu, utu wake unageuka kuwa wa kwetu, ndipo kweli unabii utakamilishwa ndani mwetu. Kwa kufanya hivyo ndipo Yesu anazaliwa ndani mwetu na kugeuka kuwa Mungu hai kwa ajili yangu. Leo hii tunaalikwa kuiga mfano wa Mamajusi, Baba Mtakatifu anasisitiza, kwa maana wao hawafanyi majadiliano, badala yake wanatembea; hawabaki kuwa watazamaji, bali wanaingi katika nyumba ya Yesu; hawajiweki katikati, bali wanainama na kumsujudia Yeye; ambaye ndiye kitovu; hawatazami mipango yao binafsi, bali wanajikita haraka  katika njia nyingine.  Na katika ishara zao kuna uhusiano nyeti wa Bwana yaani ufunguzi wa kina wa mahusiano na Yeye na ambao unawajumuisha kabisa ndani mwake na Yeye. Kwake yeye tutumie lugha ye upendo, lugha yenyewe ambayo Yesu akiwa bado mchanga alikuwa anazungumza. Kwa hakika Mamajusi walikwenda kwa Bwana si kwa ajili ya kupokea, bali kutoa. Tujiulize: je katika sikukuu ya Noeli tulimpelekea zawadi Yesu, kwa ajili ya sikukuu yake au tulibadilishana zawadi kati yetu tu?

Kama hatujatoa zawadi kwa Bwana, wakati ni huu hatujachelewa

Iwapo tulikwenda kwa Bwana na mikono mitupu, basi hatujachelewa hata leo hii. Baba Mtakatifu ameshauri. Injili kwa dhati inataka kusema kuwa kila orodha ndogo ya zawadi zilizotolewa kwa siku ile yaani dhahabu, uvumba na manemane. Dhahabu inatambuliwa kuwa kitu cha thamani, kinachokumbusha kuwa Mungu anapaswa kupewa nafasi ya kwanza. Na kuabudiwa; Lakini kwa kufanya hivyo lazima hujinyime wewe binafsi nafasi ya kwanza na kujiamini kuwa ni  mwenye kuhitaji na usiye jitosheleza. Na uvumba ni ishara ya uhusiano na Bwana kwa sala kama moshi wa ubani uelekea kwa Mungu (zab 141,2). Lakini ili ubani upate kunukia lazima uchomwe na ndiyo katika sala, lazima kuchoma kidogo muda, kutumia muda wako kwa Bwana. Ni kusali kwa dhati na siyo kwa maneno. Kwa mapendekezo ya matendo ndipo tunaona manemane ambayo ni mafuta yalitumiwa kumpaka kwa upendo mwili wa Yesu mara baada ya kutolewa msalabani (Yh 19,29).

Bwana anafurahi kuona kuwa tunatunza miili ya wale wenye kujaribiwa na mateso, mwili wake zaidi kwa wadhaifu na ambao wameachwa nyuma, wale ambao wanaweza kupokea tu bila kuwa na cha kurudisha. Ni thamani kubwa katika macho ya Mungu  kutoa huduma  kwa ajili ya wale ambao hawawezi kurudisha chochote  bali wanasubiri kupokea tu! Katika kipindi hiki cha Noeli inayoaribia mwisho wake, tusipoteze hiyo fursa kwa ajili ya kutoa zawadi kwa Mfalme wetu, aliyekuja kwa ajili wote na si katika jukwaa la tamasha na sikukuu za dunia hii, bali kwa mwanga wa umasikini wa Bethlehemu. Na kwa kufanya hivyo mwanga wake utaangaza juu yetu.

06 January 2019, 11:34