Tafuta

Katekesi ya Baba Mtakatifu tarehe 2 Januari 2019 Katekesi ya Baba Mtakatifu tarehe 2 Januari 2019 

Papa:Aliye pembezoni ndiye mjenzi wa Ufalme wa Mungu!

Katika Katekesi ya kwanza ya mwaka kwenye ukumbi wa Paulo VI, tarehe 2 Januari 2019, tafakari yake ni mwendelezo wa Sala ya Baba Yetu. Ili kuelezea mapinduzi ya Injili Papa amejita katika hotuba ya Yesu akiwa mlimani. Ametoa onyo juu ya unafiki wakati wa sala na kwamba mkristo wa kweli ni yule anayejitambua kuwa ni mwana wa Mungu

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ndugu kaka na dada habari za asubuhi na pia heri na mwaka mpya! Tuendelea na katekesi kuhusu Baba Yetu, inayo angazwa na fumbo la Noeli ambayo tumeadhimisha muda kitambo. Ndiyo mwanzo wa tafakari ya katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 2 Januari 2019, kwa waamini na mahujaji wote katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, ikiwa ndiyo katekesi yake ya kwanza kwa mwaka ambao umeanza lakini ni katika mwendelezo wa katekesi zilizopita kuhusu sala ya Baba Yetu.

Hotuba ya mlimani

Injili ya Matayo inaonesha somo la Baba Yetu katika kipindi kigumu, na ni katika kiini cha hotuba yake mlimani (taz Mt 6,9-13). Katika sehemu hiyo Yesu alipanda mlimani karibu na ziwa na kukaa akiwa amezungukwa na wafuasi wake kina baadaye, wakafika umati mkubwa usiojulikana majina yao. Mkutano kubwa sana wa watu hawa ndiyo uliopokea kwa mara ya kwanza sala ya “Baba Yetu”. Eneo hilo kwa maana nyingine ni lenye maana kubwa, kwa sababu katika mafundisho hayo marefu na ambayo yamepewa jina la hotuba ya mlimani (taz, Mt 5,1-7, 27), Yesu anasisitiza mantiki msingi ya ujumbe wake. Hotuba hiyo ni kama upinde uliopambwa katika sikukuu yaani wa Heri. Yesu anaupamba kwa furaha katika utaratibu wa watu wa wakati wake, lakini hata wa wakati wetu ambao walikuwa hawafikiriwi.

Heri masikini, wapole na wenye huruma

Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari anasema, heri maskini, wapole, wenye huruma, wanyenyekevu wa moyo… hayo ndiyo mapinduzi ya Injili. Mahali ambapo kuna Injili yapo mapinduzi. Injili haileti usumbufu, bali inatusukuma. Ni ya kimapinduzi. Watu wote wenye uwezo wa kupenda, wahudumu wa amani hadi kufikia wakati huo walikuwa wamewekwa pembezoni mwa historia, kinyume chake ni wajenzi wa Ufalme wa Mungu. Hiyo ni kama Yesu anataka kusema kuwa, endelea mbele ninyi mnaochukua mioyoni mwenu fumbo ambalo limeonesha ukuu wake katika upendo na msamaha!

Ruhusa hiyo inapindua thamani ya historia

Ruhusa hiyo ambayo inapindua thamani ya historia inachanua upya wa Injili. Sheria haipaswi kuondolewa, lakini kuna ulazima wa kuitafsiri kwa upya na ambayo inafikisha maana yake ya asili. Iwapo mtu ana roho nzuri, na yupo tayari katika upendo, ndiye anatambua kuwa kila neno la Mungu, lazima lifanyike mwili hadi kufikia matokeo yake ya mwisho. Upendo hauna mipaka. Unaweza kupenda mke wake, rafiki, hadi kufikia kumpenda adui kwa mantiki ya upyaisho. Yesu anasema: “lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki”. (Mt 5,44-45).

Baba Mtakatifu Francisko anasema, hii ndiyo siri msingi wa kila kitu katika hotuba ya mlimani kwamba, “muwe wana wa Baba yenu aliye mbinguni”. Kwa mtazamo rahisi, sura hizi za Injili ya Matayo utafikiri ni hotuba za kimaadili pia utafikiri inahitaji elimu ya dharura na ambayo ni vigumu kuitimiliza, kinyume chake ni kugundua hawali ya yote kuwa ni hotuba ya kitaalimungu. Mkristo si yule anayejibidisha ili aweze kuwa mwema zaidi ya wengine. Mkristo anatambua kuwa ni mwenye dhambi kama wengine. Mkristo rahisi pia ni mtu anayetambua kusimama mbele ya Moto Mpya unaowaka wa maonesho ya Mungu, ambaye haleti jina lisiloweza kutamkwa, lakini ambaye anaomba watoto wake wamtaje jina lake Baba na kuachwa wapyaishwe na nguvu yake na kutafakari mwanga wa wema wake katika dunia hii yenye kiu ya wema na ambayo inahitaji habari njema.

Mafundisho ya sala ya Baba Yetu

Kwa mantiki hiyo Yesu anaanzia mafundisho ya sala ya Baba Yetu. Anafanya hivyo kwa kutofautisha makundi mawili ya wakati wake. Na hayo ni wanafiki, kwa maana anasema: “Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. (Mt 6,5). Baba Mtakatifu anasisitiza, kuna watu wenye uwezo wa kusali sala kama wapagani japokuwa wanafanya hivyo ili watu wawaone na kuwasifu. Ni mara ngapi tunaona kashfa ya watu ambao wanakwenda kanisani, na kushinda kutwa nzima pale au wanakwenda kila siki wakati huo huo wanaishi na chuki na wengine au wanazungumza vibaya watu wengine. Hiyo ndiyo kashfa! Ni bora usienda Kanisani! Uishi kama mtu wa mataifa, Baba Mtakatifu ameshauri, na kuongeza kusema, iwapo unakwenda kanisani, uishi kama mtoto, kama ndugu na utoe ushuhuda na siyo mpinzani wa ushuhuda! Sala ya Mkristo kinyume chake ina ushuhuda wa kuaminiwa ambao ndiyo dhamiri yake, mahali ambapo vinasukana na kuendelea na mazungumzo na Baba kwamba: “wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujaza. (Mt 6,6).

Kwa jinsi gani ya kusali

Yesu baadaye alionesha jinsi gani ya kusali kwamba, “Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi” (Mt 6,7). Kutokana na maneno hayo Baba Mtakatifu Francisko amesema labda aliwakatisha hata tamaa wale ambao walikuwa wamezoa kusali sala nyingi za kizamani, kwa maana wakati wa sala zao zilikuwa ni ndefu za kusifu hata maombi. Tufikiria wale wa Mlima karmelo mahali ambapo Nabii Elia alishindana na makuhani wa Baal. Wao walikuwa wakipiga kelele, wakicheza cheza na wakiomba mambo mengi ili Mungu wao aweze kuwasikiliza. Kinyume chake Elia alikuwa kimya na Bwana akajionesha kwa Elia, watu wa mataifa wanafikiria kuzungumza sana ndiyo kusali.

Kutokana na hiyp Baba Mtakatifu ametoa angalisho: “ninawaza wakristo wale ambao katika kusali wanaamini kuongea na Mungu kama kasuku” Hapana, katika kusali ni kwa njia ya sala ya moyo kutoka ndani. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. (Mt 6,8). Inawezekana tu ikawa sala ya kimya Baba Yetu ikatoka ndani ya roho kwa maana ni kujiweka chini ya mtazamo wa Mungu ambao unakupeleka katika upendo wake Baba na hiyo inatosha kusikilizwa. Baba Mtakatifu amehitimisha na kusema: ni vema kufikiria kuwa Mungu wetu hana haja ya sala kwa kupata mafao! Yeye hana haja ya kitu chochote, Mungu wetu katika sala anaomba kuwa makini, katika ufunguzi wa milango yote yote ya ufahamu na Yeye ili kujigundua daima kuwa sisi ni wanawake wapendwa. Na yeye anatupenda sana!

 

 

 

 

 

 

 

02 January 2019, 16:10