Tafuta

Vatican News
Nia za Baba Mtakatifu Francisko kwa Mwezi Desemba 2018: Kutangaza na kushuhudia imani! Nia za Baba Mtakatifu Francisko kwa Mwezi Desemba 2018: Kutangaza na kushuhudia imani!  (ANSA)

Nia za Baba Mtakatifu kwa mwezi Desemba: Ushuhuda

Baba Mtakatifu anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kusali kwa ajili ya kuwaombea wahudumu na watangazaji wa imani, ili waweze kutafuta lugha muafaka katika majadiliano na tamaduni mamboleo; majadiliano yanayojikita katika sakafu ya nyoyo za watu, lakini zaidi ya yote, wawe ni wasikivu makini!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika nia zake za jumla kwa Mwezi Desemba 2018 ni kwa ajili ya kuombea huduma ya kutangaza na kushuhudia imani kwa Kristo Yesu. Baba Mtakatifu katika ujumbe wake kwa njia ya video anasema, ikiwa unataka kushirikisha imani kwa njia ya maneno, unapaswa kusikiliza sana na tena kwa makini. Waamini wanaalikwa na kuhimizwa na Baba Mtakatifu kujitahidi kuiga mtindo wa maisha ya Kristo Yesu aliyejitahidi kusoma alama za nyakati, ili kuwahudumia na kuwaonjesha upendo na huruma ya Mungu, watu waliokuwa mbele yake!

Baba Mtakatifu anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kusali kwa ajili ya kuwaombea wahudumu na watangazaji wa imani, ili waweze kutafuta lugha muafaka katika majadiliano na tamaduni mamboleo; majadiliano yanayojikita katika sakafu ya nyoyo za watu, lakini zaidi ya yote, wawe ni wasikivu makini! Ujumbe huu wa Baba Mtakatifu kwa njia ya video unasambazwa sehemu mbali mbali za dunia kwa njia ya mtandao wa utume wa sala duniani. Ujumbe huu unaweza kupatikana kwa anuani ifuatayo: (www.thepopevideo.org).

Papa: Nia Desemba 2018
07 December 2018, 07:50