Cerca

Vatican News
Chama cha Kipapa cha  Kanisa hitaji kuanzisha sala kwa ajili ya watoto wa Siria Chama cha Kipapa cha Kanisa hitaji kuanzisha sala kwa ajili ya watoto wa Siria 

Papa:tusali kwa ajili ya watoto wa Siria wanaoteseka kwa vita!

Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana Baba Mtakatifu Francisko amewasha mshumaa kwa kuonesha mshikamano wake kwa ajili ya watoto wa Siria ambao hadi sasa karibia miaka nane wanateseka na vita

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Majilio ni kipindi cha matumaini. Muda huu ninataka kuonesha matumaini ya amani kwa ajili ya watoto wa Siria, nchi pendevu Siria  ambayo inasumbuka na vita  vinavyodumu sasa karibu miaka nane. Kwa njia hiyo ninaungana na Chama cha Kipapa cha Kanisa Hitaji kuwasha mshumaa, na hiyo ni pamoja na watoto wengi ambao watafanya hivyo, watoto wa Siria na waamini wengi duniani ambao wanawasha mishumaa yao. (kuwasha mshumaa) Hayo ndiyo maelezo ya Baba Mtakatifu Francisko, aliyo anza nayo mara baada ya tafakari ya Neno la Mungu na sala ya Malaika wa Bwana, kwa mahujaji wote na waamini waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro. Baba Mtakatifu anaonesha mshikamano huo kwa watoto wa Siria ambao hadi sasa karibia miaka nane wanateseka na vita.

Mwanga wa matumaini uondoe giza la vita

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na maelezo kuhusu kuwasha mshumaa amesema “ mwanga wa matumaini na mianga mingi ya matumaini itambae na kuangazia giza nene la vita! Tusali na kuwasaidia wakristo ili wabaki nchini Siria na nchi za Mashariki kama mashuhuda wa huruma,  wa msamaha na mapatanao. Mwanga wa matumaini uwafikie hata wale wote wanaosumbuka katika siku hizi ya migogoro na mivutano mbalimbali katika pande za dunia, zilizo karibu na mbali. Maombi ya  Kanisa yaweze kuwasaidia ili wahisi ule ukaribu wa Mungu mwaminifu na kugusa kila dhamiri katika jitihada za kweli na kukuza amani. Na Bwana Mungu  wetu awasamehe wote wanao fanya vita; wale wote wanatengeneza silaha za kutuharibu, awaongoe moyo yao. Baba Mtakatifu anaongeza kusema  “ tusali kwa ajili ya nchi pendeka ya Siria . (“Salam Maria”…)

Salam mbalimbali kwa mahujaji waliofika

Kadhalika Baba Mtakatifu Fransiko amewasalimia watu wa Roma, mahujaji wote, ambao siku hizi wapo  Roma, kwa namna ya pekee waliotoka huko Linden, Marekani, Valencia na Pamplona: vilevile wanafunzi na maprofesa wa Tassisi ya Claret kutoka Madrid, Uispania. Pia salam kwa wote akiwatakia safari njema ya Majilio, lakini pia wasisahau kusali kwa ajili yake. 

        

03 December 2018, 10:37