Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amewakumbusha waamini juu ya Sikukuu ya mkingiwa dhambi ya asili tarehe 8 Desemba Papa Francisko amewakumbusha waamini juu ya Sikukuu ya mkingiwa dhambi ya asili tarehe 8 Desemba 

Papa:Sikukuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili

Tumkabidhi Mama! Yeye kama mfano wa imani na utii kwa Bwana, atusaidie kuandaa mioyo yetu ili kumpokea Mtoto Yesu katika Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Ni maneno ya Papa Francisko wakati wa akiwakumbusha waamini na mahujaji juu ya Sikukuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili, itakayofanyika tarehe 8 Desemba

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Jumamosi ijayo tutaadhimisha Sikukuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili. Tumkabidhi Mama! Yeye kama mfano wa imani na utii kwa Bwana, ili atusaidie kuandaa mioyo yetu  kumpokea Mtoto Yesu katika Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyowaeleza waamini na mahujaji wote waliofika katika katekesi ya tarehe 5 Desemba 2018 katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican. Kadhalika amewasalimia watu mbali mbali waliofikia kutoka pande za dunia, bila kuwasahau vijana, wazee, wagonjwa na wanandoa wapya.

05 December 2018, 15:36