Adam alijibu Mungu hapana, na Maria asiye na dhambi, alijibu: Tazama mimi ni mjakazi wa Bwana. Papa Francisko anashauri kuiga mfano wa Mama Maria Adam alijibu Mungu hapana, na Maria asiye na dhambi, alijibu: Tazama mimi ni mjakazi wa Bwana. Papa Francisko anashauri kuiga mfano wa Mama Maria 

Papa:Mungu daima anamtafuta binadamu na Maria anatikia ndiyo!

Katika tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, tarehe 8 Desemba 2018, kwa waamini na mahujaji amejikitia kuelezea majibu ya Adam na Maria waliyotoa kwa Mungu. Adam alijibu hapana na Maria asiye na dhambi akaitikia Tazama mimi hapa nitendewe kama ulivyosema. Anawaalika waamini kuitikia ndiyo kila siku kwa Mungu kama Mama Maria

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Leo hii Neno la Mungu linawakilisha na majibu mawili tofauti. Katika Somo la kwanza linaonesha mtu kwa  asili, alimjibu Mungu hapana. Na katika Injili yupo Maria ambaye wakati wa kupashwa habari  njema anaitikia ndiyo. Masomo yote mawili yanaonesha kuwa Mungu anamtafuta binadamu. Lakini katika kesi ya kwanza inamlenga Adam, mara baada ya kutenda dhambi, Mungu anamuuliza “huko wapi?” (Mw 3,9) na anamjibu; nimejificha (Mw 3,10). Katika kesi ya pili, inamwendea Maria asiye na dhambi, ambaye alijibu; “ Tazama mimi ni mjakazi wa Bwana” (Lk 1,38). Tazama mimi, ni kinyume na nimejificha. Tazama mimi inafungulia Mungu wakati huo huo dhambi inafunga,  inaleta upweke na kubaki peke yako umejifungia binafsi katika upweke.

Tazama mimi hapa ni ufunguo wa maisha

Tazama mimi ni neno au ufunguo wa maisha. Ni alama ya hatua ya maisha yenye upeo, juu yake hasa katika mahitaji na maisha yaliyonyooka kuelekea upeo kwa Mungu. Tanzama mimi hapa ni kuruhusu kuwa na Bwana, ndiyo kushinda ule ubinafsi, ambao pia ni kama dawa ya kushinda ile tabia ya  kujitosheleaza katika maisha, na ambayo wakati mwingine ni kukosa kitu. Tazama mimi, ni kuamini kwamba Mungu anahesabiwa zaidi ya umimi. Ni kuchagua kutoa ahadi kwa Mungu, mnyoofu na mwingi wa mishangao yake. Kwa njia hiyo kusema tazama mimi hapa, ni sifa zaidi na kubwa ambayo tunaweza kuitoa.

Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, tarehe 8 Desemba 2018, kwa waamini na mahujaji wote katika kiwanja cha Mtakatifu Petro, wakati Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili. Baba Mtakatifu akiendelea kuelezea juu ya neno tazama mimi anasema: Swali: je kwanini usianze na siku namna hiyo? Ingekuwa vema kusema kila asubuhi; tazama mimi ee Bwana, mapenzi yako kwangu yatimie”. Hata hivyo tutasema  wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, lakini hata sasa tunaweza kurudia pamoja: Tazama, Bwana leo hii mapenzi yako yatimie!

Shetani anatambua kujaribu imani kwa Mungu

Baba Mtakatifu akifafanua zaidi anathibitisha kuwa: Maria anaongeza kusema mapenzi yako yatimie kama ulivyonena; Yeye hakusema: “yatimie kwa mijibu wangu”, bali kwa ajili yako”. Hakumwekea Mungu vikwazo ; Hakufikiri kwamba ninaitikia kwake kidogo; nina harakisha na baadaye nafanya kile ninachotaka”. Hapana, Maria hakumpenda Bwana alipokuwa anataka au kidogo kidogo. Yeye aliishi kwa kuamini Mungu kwa kila kitu. Tazama ndipo kuna siri ya maisha. Yeye ni mweza yote, na  unaweza kuamini Mungu kwa kila kitu. Lakini Bwana, anataseka tunapomjibu kama vila Adam: nimeogopa ndiyo nikajificha”. Mungu ni Baba, mpendelevu wa mababa na anatamani kuona imani ya wana wake. Baba Mtakatifu anauliza swali: Ni mara ngapi badala yake tuna wasiwasi nayena tunafikiri kuwa anaweza kutoa majaribu, kunyima uhuru na kutuacha? Lakini huo ni uongo mkubwa, ni kishawishi cha asili, ni kishawishi cha shetani. Shetani mara nyingi anatafuta kuondoa imani katika Mungu. Maria alishinda kishawish cha kwanza kwa njia ya kuitikia tazama mimi hapa. Kutokana na hili Baba Mtakatifu anashuru kuwa:” Leo hii tutazamae uzuri wa Maria aliyezaliwa bila dhambi  na daima ni mpole na muwazi kwa Mungu.

Fikirieni Mtakatifu Yosefu, je watu wangesema nini?

Lakini hayo yote Baba Mtakatifu Francisko, amesisitiza, haikuwa na maana ya kwamba maisha yake yalikuwa rahisi. Kuwa na Mungu siyo suala la kutatua matatizo hivi kama  vile mazingaombwe. Sehemu ya mwisho ya Injili inakumbusha leo hii kuwa: “Malaika alienda mbali naye”. Aliondoka kwenda mbali, ni neno la nguvu. Malaika alimwacha Bikira peke yake katika hali ngumu.  Yeye kwa namna ya pekee aliambiwa na Malaika kuwa angekuwa Mama wa Mungu, na Malaika hakuwa amewasilimulia wengine. Lakini matatizo yalianza haraka. Fikirieni hali halisi  yakanuni kwa mujibu wa sheria,iliyokuwa ikimsumbua Mtakatifu Yosefu, katika mipango ya maisha iliyojitokeza, je watu wangeweza kusema nini… Lakini Mama Maria aliweza kuwa na imani kwa Mungu mbele ya matatizo hayo. Yeye alichwa pembeni na Malaika, lakini anaamini kuwa  naya na kubaki na Mungu kwa maana nyingine anaamini. Ni uhakika kuwa katika Bwana, hata kama hakuwa anatarajia, mambo yote yatakwenda vizuri. Baba Mtakatifu anasisitiza, Tazama huo  ndiyo mwenendo wa hekima, ambapo si kuishi kwa kufikiria matatizo, kwa maana likiisha moja linaingia jingine na kuendelea, lakini ni kuishi kwa kumtegemea Mungu kila siku. Tazama mimi hapa! Ni neno, ni sala na hivyo Baba Mtakatifu anahitimisha akisema tumwombe Mama Maria Mkingiwa dhambi ya Asili neema ya kuishi hivyo.

08 December 2018, 12:53