Angelus prayer Angelus prayer 

Papa:moyo wetu ukiwa na Mungu ndiyo furaha tele!

Kupaza sauti kwa furaha na kushangilia ndiyo wito unaotujia kutoka katika Liturujia ya Dominika ya Tatu ya Majilio. Katika fursa hiyo Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana hakukosa kukumbusha waamini nini maana uwepo wa Mungu kati yao na ambaye ni kisima cha furaha ya dhati na amani

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Domenika ya tatu ya Majilio, liturujia inatualika kuwa na furaha. Sikilizeni vema. Nabii Sefonia anaelekeza maneno hayo katika kundi dogo la Israeli kwamba: “Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, Ee binti wa Sayuni. Watu wa Sayuni wapaze sauti na waimbe kwa furaha, kwani Mtakatifu wa Israeli yupo katikati yao. Kupaza sauti kwa furaha na kushangilia ndiyo wito ambao unasikika katika Jumapili hii. Wakazi wa mji Mtakatifu wanaalikwa kufurahi kwa sababu Bwana ameziondoa hukumu zao. Bwana amewasamehe,hakutaka kuwaadhibu! Kwa sababu hiyo watu hawana sababu ya kuwa na huzuni na hakuna sababu ya kukata tamaa, bali yote hayo yanageuka kuwa shukrani na furaha kwa Mungu ambaye anataka kuwaokoa daima na kuwapenda.

Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, kwa waamini na mahujaji wote waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 16 Desemba 2018, wakati mama Kanisa anaadhimisha Dominika ya tatu ya Majilio, ambayo inajulikana kama Dominika ya Gaudete au Dominika ya furaha. Hii pia ni kwa sababu Antifona katika misa, inatualika “tufurahi katika Bwana daima na tena tufurahi kwa sababu Bwana yupo karibu nasi”.

Upendo wa Bwana kwa watu wake

Baba Mtakatifu Francisko, akiendelea na tafakari yake anasema, upendo wa Bwana kwa watu wake, hauna kikomo na unafanana na: upendo wa baba na watoto wake, bwana arusi na bibi arusi, kama asemavyo nabii Sefonia kuwa: “Atakufurahia kwa kuimba. Nitapyaisha kwa upendo wake na kushangilia kwa ajili yao na kupaza sauti ya furaha”. Baba Mtakatifu anaongeza kusema: “Na ndiyo inaitwa Dominika ya furaha; Dominika ya tatu ya Majilio kabla ya Kuzaliwa kwa Bwana”. Wito huo wa Nabii ni kwa namna ya pekee wa kipindi hiki ambacho kinatengenisha kati ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, kwa sababu ni kuhisi  ukaribu wa Yesu, Emanueli, Mungu pamoja nasi. Uwepo wake ni kisima cha furaha. Kwa dhati Sefonia anatangaza: “Mfalme wa Israeli ni Bwana katikati yake”, na baadaye kidogo anarudia kusema: “Bwana Mungu wako yuko katikati yako na ni mwokozi na mwenye nguvu”. Ujumbe huo unapata ujazo tangu wakati ule wa Malaika alipo mpasha habari Maria kwa mujibu wa Injili ya Luka. Maneno ya Malaika Gabrieli kwa Bikira Maria Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, ni kama mwangwi wa nabii. Je Malaika Gabrieli alimwambia nini? Alisema: “Furahi, umejaa neema, Bwana yu nawe” (Lk 1, 28).

Malaika anamweleza Maria furahi umejaa neema

Baba Mtakatifu anaendelea kueleza kuwa: Katika mtaa wa pembeni mwa Galilaya, Malaika alimwambia Maria furahi. Katika moyo wa kijana mwanamke asiyejulikana duniani, Mungu aliwasha cheche za furaha kwa dunia nzima. Leo hii tangazo hilo, linahusu Kanisa na kualikwa kupokea Injili kwa sababu Injili hiyo iweze kuwa nyama na maisha ya dhati. Anazungumza kwa Kanisa na kwa maana hiyo kwa watu wote, kwamba furahini jumuiya ndogo ya kikristo maskini na wanyenyekevu. Mungu anasema kitu kizuri katika macho yangu Baba Mtakatifu anasisitiza, kwa sababu shauku ya utashi wa ufalme wa Mungu, bado unagatawaliwa na njaa na kiu ya haki, dunia inayosubiri kwa uvumilivu kuwa na amani. Husifuate wenye nguvu, bali hubaki na uaminifu karibu na maskini. Na kwa maana hiyo mtu kama huyo haogopi chochote, bali anakuwa na moyo wa furaha. Iwapo sisi tutaishi kwa namna hiyo, yaani kwa uwepo wa Bwana, moyo wetu daima utakuwa na furaha. Furaha ya hali ya juu, hasa iwapo imejaa na furaha ya unyenyekevu wa kila siku na amani. Amani na furaha ni ndogo, lakini ni furaha, Baba Mtakatifu amethibitisha.

Mtakatifu Paulo anashauri kutojisumbua kwa neno lolote

Naye Mtakatifu Paulo kwa Wafilipi, Baba Mtakatifu anaendelea kusema kuwa, anatoa ushauri kwamba: “Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. (Fil 4,6) na Hivyo Baba Mtakatifu anasema kwamba kuwa na utambuzi ya kwamba hata katika matatizo, tunaweza daima kumwelekeza Bwana na yeye hamkatalii kamwe mtu maombi yake, na ndiyo sababu ya furaha. Hakuna mahangaiko, hakuna hofu inaweza kutuondolea utulivu iwapo hatokani na mambo ya binadamu, kwani inatoa faraja ya binadamu, anakuwa na utulivu maana inatokana na Mungu na ndiyo utambuzi ya kwamba Mungu anaongoza upendo wa maisha yetu na anatenda daima. Hata mbele ya matatizo na mateso kuna auhakika huo unaoongeza matumaini na ujasiri.

Mbele ya mwaliko huo inahitajika watu walio tayari

Ili kuweza kukubali mwaliko wa Bwana wa furaha, Baba Mtakatifu Francisko anaendela na tafakari kubainisha kuwa inahitajika kuwa na watu walio tayari kujiuliza. Nini maana yake? Hiyo ni sawa na kufanya tendo lile hasa watu baada ya kusikiliza mahubiri ya Yohane Mbatizaji: “Makutano wakamwuliza Yohane, Tufanye nini basi? (Lk 3,10). Je mimi ninaweza kufanya nini? Swali hili ndiyo hatua ya kwanza ya uongofu ambao tunaalikwa kutenda katika kipindi hiki cha Majilio. Kila mmoja ajiulize: ni kitu gani nifanye basi? Jambo moja dogo sana, lakini jambo gani? Na Bikira Maria ambaye ni mama yetu, anatusaidie kufungua mioyo yetu kwa Mungu anayekuja kwetu ili aweze kutujaza furaha ya maisha yetu yote.

 

 

17 December 2018, 10:22