Baba Mtakatifu amekutana na wahudumu wote wa Vatican na familia zao Baba Mtakatifu amekutana na wahudumu wote wa Vatican na familia zao 

Papa kwa wafanyakazi Vatican:Ondoeni hofu ya utakatifu na kuweni na furaha!

Tuombe msamaha na kwenda mbele.Tuwe tayari kujiachia ili kuambukizwa na uwepo wa Yesu kati yetu. Kuwa tayari kukimbilia kwake kama walivyofanya wachungaji na kuona tukio hilo.Lakini sisi tuna hofu ya kuwa watakatifu,japokuwa ndiyo uhakika wa njia ya furaha. Ni hotuba ya Papa alipokutana na wafanyakazi wa Vatican na familia zao ili kuwatakia sikukuu njema ya Noeli

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ninawashukuru kufika kwenu kwa wingi mkiwa na familia zetu. Nimefuhia kusalimia familia moja lakini kwa kuipongeza zaidi kwa bibi mwenye miaka 93 na mtoto wake akiwa naye ni bibi na wajuuu. Ni vema kuwa na familia nzuzir hivi. Na ninyi mnafanya kazi kwa ajili ya familia na watoto ili kupeleka mbele familia. Ni neema na ulinzi wa Familia. Sikukuu njema!  Ndiyo mwanzo wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko alipokutana na wafanyakazi wote wa Vatican wakiwa na familia zao, ili kutakiana matashi mema ya sikukuu ya Krismasi. Mkutano ulifanyika katika ukumbi wa Papa Paulo VI, tarehe 21 Desemba 2018.

Sikukuu kwa kawaida ni furaha japokuwa mambo mengi yanatuondolea furaha

Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake, anasema Sikukuu kwa kawaida ni furaha japokuwa mara nyingi tunajikuta sisi binafsikatika mambo mengi na mwisho wake furaha haipo na hata kama ipo basi ni ya kijujuu: Je hii ni kwanini? Baba Mtakatifu ili aweze kuelezea hivyo amemtumia mwandishi mmoja wa Ufaransa Leon Bloy kwamba: hakuna furaha bali ni huzuni (…) wa kutokuwa mtakatifu”. Kwa maana hiyo kinyume cha huzuni ni furaha, anathibitia Papa na kusema kuwa ndiyo inaungana na utakatifu  pia ni furaha ya Noeli.

Tutazame pango, ni nani mwenye furaha?

Ni nani mwenye furaha katika pango? Baba Mtakatifu Francisko ameuliza swali hilo watoto wanaopendelea kutazama sanamu ndogo kwa utukutu… kupenda kuzishikilia na kupangua hadi kuwafanya wazazi wakasirike kidogo! Mwenye kufurahi ni nani?  Maria na mtakatifu Yosefu wamejazwa na furaha. Tutazame mtoto Yesu, kwa wote ni wenye furaha, mara baada ya maelfu ya matatizo mengi walipokea zawadi hii ya Mungu, kwa imani kubwa na upendo mkuu baba; Mtakatifu anathibitisha. Walijazwa na utakatifu na hivyo furaha.

Utakatifu siyo wa kuzaliwa, bali ni kugeuka kuwa mtakatifu

Swali la kujiuliza je ni kwa nguvu ipi, Maria na Yosefu wanafurahi? Tusifikiri ilikuwa rahisi, kwa maana utakatifu auzaliwi nao bali unageuka  kuwa mtakatifu na hivyo hata kwa waa ilikuwa hivyo Baba Mtakatifu amesema. Pia wachungaji wamejazwa na furaha. Na wao ni watakatifu kwa maana walijibu tangazo la malaika, na kukimbia hupesi katika pango na kutambua ishara za mtoto mchannga holini.

Masengenyo kazini yanaleta huzuni na kutengenisha

Baba Mtakatifu Francisko, pia amesema kuna jambo fulani linaloleta huzuni katika kazi na kuwafanya utawale na uwe  ugonjwa katika mazingira ya kazi, jambo hili ni masengenyo. Ameonya wafanyakazi waache tabia ya kusema wengine vibaya. Kuchambua wengine, bali wasali kwa ajili ya mtu anayewakwaza. Ni muhimu kukabiliana naye uso kwa uso kuliko kumsema nyuma kwa maana hiyo inaharibu na kuleta uadui. Ameaomba wawe wazi kati yao.

Wapo watakatifu hata katika mazingira ya kazi

Licha ya hayo lakini Baba Mtakatifu amesema kuwa katika maeno ya kazi kuna hata utakatifu uliolezwa katika wosia wa (taz Gaudete et exsultate, 6-9). Hata mjini Vatican, yeye binafsi anaweza kushuhudia kuwa anatambua watu kati yao kama mfano wa maisha. Wanafanya kazi kwa ajili ya familia, daima kwa tabasamu, na kujitoa bila kubakiza. Huo ndiyo uwezekano wa utakatifu. Ameongeza kusema Baba Mtakatifu kuwa huu ni mwaka wae wa sita akiwa askofu wa Roma na  akiadhimisha sikukuu hii, kwa maana hiyo ameshawatambua watakatifu hao katika kazi mjini Vatican.

Watakatifu wanaoishi vema ukristo, wakitenda jambo baya, wanaomba msamaha na wanaendelea mbele na familia yao, na wanauwezo wa kuishi kwa namna hiyo. Ni neema na ndiyo jambo jema. Lakini watu hao mara nyingi hawajioneshi, ni watu rahisi, lakini wanafanya kazi vizuri, na kuwa na mahusiano mazuri na wengine. Na zaidi ni watu wenye furaha, si kwamba wanacheka daima, bali ndani ya roho zao, wanaonesha utulivu kwa wengine. Je huo utulivu unatoka wapi? Unatoka kwa Yesu, Mungu pamoja nasi. Yeye ndiye kisima cha furaha, kibinafsi, kifamilia na katika kazi.

Matashi mema ya Baba Mtakatifu uili wawe watakatifu na wenye furaha

Kutokana na maelezo hayo, ndipo Baba Mtakatifu Fracisko amewatakia matashi mema ya kuwa watakatifu na wenye furaha. Wasiwe watakatifu kama wale wa sanamu. Bali wakatifu wa kawaida.  Utakatifu wa nyma na mfupa. Katika tabia yetu, madhaifu na hata katika dhambi zetu, amesisitiza. Tuombe msamaha na kwenda mbele. Tayari kujiachia ili kuambukizwa na uwepo wa Yesu kati yetu, kuwa tayari kukimbilia kwake kama walivyofanya wachungaji na kuona tukio hilo. Ishara ya kiajabu ambayo Mungu alitupatia. Na kwa upande wa Malaika, Baba Mtakatifu anaongeza kusema : ninawatangazia furaha kubwa ambayo ni kwa ajili ya wote (Lk 2,10) Twende tukaone? Au tutakuwa tumejikita katika mambo mengine? Baba Mtakatifu amethibitisha kuwa sisi tuna hofu ya kuwa watakatifu lakini anahakikisha kuwa hiyo ni njia ya furaha.

21 December 2018, 15:25