Tafuta

Baba Mtakatifu amekutana na sekretarieti Kuu ya Vatican kwa ajili ya matashi mema ya Kuzaliwa kwa Bwana Baba Mtakatifu amekutana na sekretarieti Kuu ya Vatican kwa ajili ya matashi mema ya Kuzaliwa kwa Bwana 

Papa kwa Sekretarieti: mwanga una nguvu zaidi ya giza!

Kwa misingi ya kwamba daima mwanga ni wenye nguvu zaidi ya giza, Baba Mtakatifu ametaka kujikita kutafakari juu ya mwanga unavyounganishwa na Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana kwa watu wote ambao wanatoa huduma katika Sekretarieti Kuu

 Sr.Angela Rwezaula - Vatican

“Usiku umezidi sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza na kuzivaa silaha za nuru”. (Rm 13,12). Tukiwa tumejazwa furaha na matumaini yanayoangazwa na uso wa Mungu mtoto, tunakutana kwa mara nyingine tane mwaka huu kubadilisha matashi mema ya sikukuu, kiwa tumejazwa uzito wa mambo mengi na furaha za ulimwengu na Kanisa. Ninawatakia matashi mema kwa moyo wote wa Sikukuu Takatifu Noeli, kwa  wote wanaoshirikiana kutoa huduma katika Sekreatarieti Kuu,  Wawakilishi wa mabaraza ya Kipapa na wahudumu wote katika ubalozi. Ninapenda kuwashukuru ninio nyote kwa kujikita kila siku katika huduma ya Vatican, ya Kanisa na Mfuasi wa Petro, Asante sana! Ni maneno ya hotuba yake aliyoanza nayo Baba Mtakatifu Francisko, tarehe tarehe 21 Desemba 2018 alipokuta na Sekretarieti Kuu ya Vatican kwa ajili ya kuwatakia matashi mema ya sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana.

Baba Mtakatifu katika fursa hiyo amemkaribisha Katibu Mpya msaidizi wa Vatican, Askofu Mkuu Edgar Peña Parra

Baba Mtakatifu katika fursa hiyo amemkaribisha Katibu Mpya msaidizi wa Vatican Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, ambaye ameanza kutoa huduma yake nyeti na muhimu tangu tarehe 15 Oktoba 2018. Nchi anayotoka ya Venezuela, Baba Mtakatifu amesema, inamulika ukatoliki wa Kanisa na ulazima wa kufungua daima upeo hadi miisho ya dunia. Karibu mheshimiwa na kazi njema! Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana inatujaza furaha na kutupatia uhakika ya kuwa hakuna dhambi yoyote itaweza kuwa kubwa zaidi ya huruma ya Mungu na kuna tendo la kibinadamu linaweza kamwe kuzuia kuchanua mwanga wa Mungu na kuzaliwa kwa upya katika mioyo ya watu. Ni sikukuu inayotualika kupyaisha shughuli za kiinjili na kutangaza Kristo Mwokozi wa dunia na mwanga wa ulimwengu. Iwapo kwa dhati “Kristo, Mtakatifu asiye kuwa na hatia na dhambi (Eb 7,26) hakujua dhambi, (2Kor 5,21) na alikuja kwa lengo la kukomboa watu dhambi zao  ( Eb 2,17), Kanisa linalotambua katika umbu lake la dhambi na hivyo ni takatifu na pamoja daima na linalohitajikita kujitakatifuzana linaendelea na safari ya toba na kujipyaisha, Baba mtakatifu amesema.

Kanisa linaendelea na hija yake kati ya mateso na faraja za Mungu

Kanisa, linaendelea katika hija yake kati ya kuteswa duniani na faraja za Mungu kwa kutangaza mateso na kifo cha Bwana hadi yeye atakaporudi tena (1Kor 11,26). Kutoka katika fadhila za Bwana inavutia nguvu ili kushinda kwa uvumilivu na upendo katika masumbuko na matatizo ambayo anakuja kutoka ndani au nje, ili kuweza konesha katikati ya dunia na kwa uaminifu hata kama sikwa utilimifu, lakini hadi kwamba mwisho wa nyakati yote hayo yatoneshwa kwa ukamilifu wa mwanga wake (CONC. ECUM. VAT. II, Cost. dogm. Lumen gentium, 8). Kwa misingi ya kwamba daima mwanga ni wenye nguvu zaidi ya giza. Baba Mtakatifu ametaka kujikita kutafakari juu ya mwanga unavyounganishwa na Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, na kwamba ,kwanza alikuja kwa unyenyekevu na mwisho wa kufika kwa Bwana mara ya pili atakuja kwa njia ya utukufu na ambapo ni uhakika wa matumaini yasiyo katisha tamaa kamwe. Matumaini ambayo yanategemea maisha ya kila mmoja na historia nzima ya Kanisa na ulimwengu.

Yesu alizaliwa katika hali hali ya kisiasa, kijamii na kidini katika mivutano

Kwa hali halisi Yesu anazaliwa katika hali ya kisiasa, kijamii na kidini iliyojaa mivutano, mahangaiko na giza nene. Kuzaliwa kwake, kwa upande mwingine, alikuwa anasubiria na kwa upande mwingine anakataliwa na kwa mantiki ya Mungu ambayo haijali ubaya, lakini inabadili kwa kina na taratibu kuwa wema hata kwa mantiki ya ulaghai ambayo kwa taratibu unabadili wema katika ubaya, na kupelekea ubinadamu kubaki katika mahangaiko na katika giza: Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuweza kupokea.  (Yh 1,5.

Kila Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana, Baba Mtakatifu anendelea, inatukumbusha kuwa wokovu wa Mungu uliotolewa bure kwa ubinadamu wote, kwa Kanisa na kwa namna ya pekee sisi , watu tuliotiwa wakfu , hautolewi bila kuwa na utashi wetu, bila ushirikiano wetu, bila kuwa na uhuru, bila kuwa na juhudi za kila siku. Wokovu ni zawadi ambayo lazima ipokelewe, ilindwe na kutoa matunda (Mt 25, 14-30). Kuwa wakristo, kwa ujumla na kwa ajili yetu kwa namna ya pekee, walioweka wakfu kwa Bwana haina maana kuwa ni wenye kupendelewa zaidi na wao kuamini ya kuwa Mungu yuko ndani ya mifuko yao, hapana Baba Mtakatifu amekuzia, badala yake , hao ni watu ambao wanajitambua kuwa wamependwa na Bwana, licha ya kuwa ni wadhambi na kutostahili. Kila aliyejitoa kwa Bwana, kwa dhati atambue kuwa ni mtumishi katika shamba la Bwana, ambalo lazima liweze kutoa matunda kwa wakati wake, kukusanya kile kinachopatika na kumpatia mkuu wa shamba hilo( Mt 20,1-16).

Biblia na historia ya Kanisa

Baba Mtakatifu anendelea, kuonesha kuwa mara nyingi hadi wale walioteuliwa katika njia ya kumfuasa Kristo, wanaanza kuamini na kuwa na mtindo wa kuishi kama ambao tayari wana wokovu, na siyo waliofadhiliwa, au kujifanya ndiyo wakaguzi wa kazi ya Mungu na siyo wanyenyekevu wa kuweza kugawanya, au  kama walinda mipaka ya Mungu na si kama wahudumu wa mazizi waliyokabidhiwa. Mara nyingi hata kuzidisha kipimo Baba Mtakatifu ambainisha kuwa  badala ya kufuata Mungu na kujiweka mbele yake kama Petro aliyeambiwa na Mwalimu na akimkaripia vikali kwa nguvu zote: “Nenda nyuma yangu wewe ni Shetani, kwa sababu hufikiri kwa mijibu wa Mungu bali kama binadamu ( Mk8,33). Baba Mtakatifu Francisko katika  hotuba yake anasema katika dunia iliyowaka moto, mtumbwi wa Kanisa mwaka huu imefanya uzoefu wa kipindi kigumu na imekumbwa na dhoruba na upepo mkali. Wengi wamejikuta wanauliza Mwalimu ambaye alijifanya kusinzia: “Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia? (Mk 4,38). Na wengine kwa mshangao wa habari, walianza kupoteza matumaini na kuliacha; na wengine kwa hofu, kwa manufaa na kwa lengo binafsi wamejaribu kuuumiza mwili wake na kuongeza majeraha; wengine hawakuficha kuonesha furaha yao ya kuona mtetemeko huo; wengine wengi lakini wanaendelea kuparamia Kanisa hilo kwa ukakika kuwa: “wala milango ya kuzimu haitalishinda (Mt 16,18). Na zaidi ya hayo Mchumba wa Kristo anaendelea na hija kwa furaha na masumbuko, kati ya mafaniko na matatizo ya ndani na nje. Kwa uhakika matatizo ya ndani yanabaki ya uchungu na ya uharibifu

Baba Mtakatifu ameeleza mateso

Mateso ni mengi Baba Mtakatifu Francisko anathibitisha na kuyataja. Ni wahamiaji wangapi wamelazimaka kuacha makwao na kuhatarisha maisha, wakikumbana na kifo au wangapi wameponea chupuchupu, lakini wakakumbana na milango iliyofungwa na ndugu katika ubinadamu ambao umejikita katika masuala ya kisiasa na mamlaka kwa maslahi yao.  Hofu na hukumu ngapi ni watu wangapi na watoto wangapi wanakufa kila siku kutokana na ukosefu wa maji, chakula na madawa! Umaskini na taabu nyingi! Vurugu nyingi dhidi ya wadhaifu na dhidi ya wanawake! Ni matukio mangapi ya vita vilivyotangazwa na visivyo julikana: je ni damu ngapi isiyo na hatia inamwagika kila siku! Ni kiasi gani kisicho cha ubinadamu na ukatili unatuzunguka kila upande! Ni watu wangapi kwa mifumo ya kupangwa wanaoteswa hata leo katika vituo vya polisi, magereza na makambi ya wakimbizi katika sehemu mbalimbali za dunia!

Kadhalika, tunaishi kipindi halisi cha nyakati za wafia dini. Utafikiri ni ukatili na mateso  wa utawala wa kirumi usiotambua mwisho wake. Bado wanazaliwa Neroni wapya ambao wanaendelea kukandamiza waamini kwasababu ya imani yao katika Kristo. Makundi mapya ya kiitikadi yanazidi kungezeka na kuishi kwa hasira, na chuki ka kulipiza visasi kwa Kristo, Kanisa na waamini. Ni wakristo wangapi leo hii wanaishi chini ya mzigo wa mateso, wamebaguliwa, hawana haki, pande nyingi za dunia! Licha ya hayo wanazidi kwa ujasiri kukumbatia kifo na ili wasimkane Krsto. Ni matatizo mangapi na magumu bado leo hii  yapo ya kuishi bila  uhuru wa kidini  katika sehemu mbalimbali za dunia, mahali ambao upo ukosefu wa kuishi uhuru wa kidini na uhuru wa dhamiri! Kwa upande mwingine, ipo mifano ya ushujaa wa wafiadini na idadi kubwa ya wasamaria wema. kama vile vijana na familia, vyama vya kitume katika upendo, watu wa kujitolea, waamini wengi na watawa japokuwa, wengine hawawezi kusahalisha ukosefu wa ushuhuda na kashfa za baadhi ya wana na wahudumu wa Kanisa.

Kuhusu janga la manyanyaso na ukosefu wa uaminifu

Kanisa kwa miaka kadhaa inajikita kutika juhudi za kupambana na ili kuondoa mzizi wa ubaya wa manyanyaso ya kingono, kwa waathirika wanao paza sauti ya kulipiza kisasi kwa Bwana, kwa Mungu ambaye asahau kamwe mateso ya wadogo yaliyosababishwa na makleri na watu walitiwa wakfu: manyanyaso ya malamka, dhamiri na kingono. Baba Mtakatifu Francisko akifikiria uchungu huo, wazo limemjia akilini, na kukumbuka  sura ya Mfalme Daudi aliyekuwa wamepakwa Mafuta na Bwana (taz 1 Sam 16,13; 2 Sam 11–12). Yeye ambaye ni uzao wa Mungu mwana, anayeitwa hata Mwana wa Daudi. Licha ya kuwa alichaguliwa kuwa mfalme aliyepakwa mafuta ya Bwana, alitenda dhambi mara tatu, yaani dhambi kuu tatu za manyanyaso; nyanyaso la kingono, mamlaka na dhamiri. Manyanyaso hayo matatu ni tofauti, lakini yamepangwa pamoja. Baba mtakatrifu amefafanua zaidi juu ya historia ya Mfalme Daudi na dhambi zake (taz 2 Sam 11). Kwa maana hiyo aliyetiwa wakafu mara baada ya kutenda dhambi anasema  aliendeela na utume wake, utafikiri hakuna lolote lililotukia, kwa maana alitaka kuokoa sura yake na unafiki tu lakini kwa sababu  mara nyingi wadhambi wanaishia kuwa wafisadi (Esort. ap. Gaudete et exsultate, 164).

Hata leo hii wapo waliopakwa mafuta ya Bwana

Hata leo hii Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa, wapo waliopakwa Mafuta ya Bwana, waliotiwa wakfu, ambao wananyanyasa wadhaifu, kwa kutumia madaraka yao kimaadili na ulaghai. Wanatimiza ubaya mkubwa wakati huo huo wanaendelea na utume wao  kama vile hakuna baya lilitoendekeka, hawaogopi Mungu au hukumu yake, wanachoogopa ni kugunduliwa tu machoni pa watu . Huduma ya namna hii inaumiza mwili wa Kanisa na kusababisha kashfa katika utume wa wokovu wa Kanisa na sadaka ya ndugu zao wengi. Baba Mtakatifu amethibitisha. Hata leo hii kuna Daudi wengi na wanaingia katika mtandao wa ufisadi, wanasaliti Mungu na wito wao, wito  wa Kanisa, watu wa Mungu na matumaini ya wadogo na familia zao. Mara nyingi nyuma ya ulhaghai huo kuna picha ya ukarimu, au shughuli na sura ya kimalaika wakati huo huo wanaficha uchafu na ulagahi kama ule wa  mbwa mwitu ambaye yuko tayari kukurarua roho isiyo kuwa na hatia. Dhambi za uhalifu wa watu waliotiwa wakfu,utafikiri zimepakwa rangi ya kuchovya,lakini wanakosa uaminifu, ni aibu na kutengeneza uso wa Kanisa usio wa kuaminiwa. Kwa dhati Kanisa pamoja na watoto waaminifu, ni waathirika wa ukosefu wa uaminifu wa mambo haya ya kweli ya kihalifu, Baba Mtakatifu amesisitiza.

Manyanyaso yaliyotokea yanapingwa vikali na Kanisa, kamwe yasitokee

Akiendelea na hotua yake, Baba Mtakatifu ametakamka kuwa Kanisa haliwezi kuvumilia yoyote anayetenda uhalifu huo, na kuhakikisha kwaman kuna ulazima wa kuwafikiasha katika vyombo vya hkai,kwa kila yoyote mhalifu. Kanisa kamwe halifuniki kwa mchanga au kadharau kesi kama hizo. Haiwezekani kukataa kuwa baadhi ya wahusika wa nyakati zilizopita, wengine walikuwa wepesi, wagyumu kuelewa, kutoamini, bila kuwa na maandalizi, bila kuwa na uzoefu, au uzoefu wa kiroho na kubinadamu, wamejihusisha na kesi hizi bila kuchukulia suala hili maanani uzito wake na bila utayari. Lakini hayo yote, Baba Mtakatifu amethibitisha kuwa yasitokee kwa mara nyingine tena. Huo ndiyo uchaguzi na maamuzi ya Kanisa zima!.

Maamuzi ya Kanisa wakati wa Mkutano mwezi Februari 2019

Baba Mtakatifu amesema,mwezi Februari ujao, Kanisa litatoa msimamo wake na utashi wa mchakato wa kuendelea nao kwa nguvu zote  juu ya njia ya utakaso. Kanisa litajiuliza, kwa kushirikiana na wataalam, kwa jinsi gani ya kuweza kuwalinda watoto; ni jinsi gani ya kuzuia balaa hili na kwa nmna gani ya kupanua ushirikiano, kushirikisha waathirika; na ni jinsi gani ya kuimarisha mafunzo katika seminari. Kanisa litatafuta namna ya kubadili makosu yaliyotokea na ili kuweza kuondoa mzizi wa janga hilo na  si katika mwili wa Kanisa, lakini pia hata katika jamii nzima. Kwa dhati, katika suala hili kubwa  hivi Baba Mtakatifu amesema limefikia kushambuliwa hata kwa baadhi ya wahudumu waliotiwa wakfu, na ambao ni kujiuliza ni kwa jinsi gani inaweza kuathiri kwa kina jamii na familia zetu? Kanisa kwa namna hiyo haliishi tu katika kuponya, bali hata katika kukabiliana na ubaya ambao unasababisha kifo cha taratibu kwa watu wengi kwa ngazi ya kimaadili, kisaikolojia na kibinadamu.

Kashfa iliyo kubwa ni ile ya kufunika ukweli

Wakati wa  kuzungumza juu ya janga hili, Baba Mtakatifu amesema, baadhi ya watu hata ndani ya Kanisa wamekasirikia baadhi ya wahudumu wa mawasiliano katika vyombo vya habari , kwa kwashutumu ya kwamba  pamoja na janga hili, lakini  wamedharaua sehemu kubwa ya manyanyaso na kwamba haikutendwa tu na baadhi ya wahudumu wa Kanisa, kwa maana ya kua na nia mbaya ya kutoa sura ya uongo, kama vile ubaya huo umekumba Kanisa Katoliki peke yake. Lakini Baba Mtakatifu Francisko, kinyume chake amependa kuwashukuru wale wote wahudumu wa vyombo vya habari na hasa wenye nia njema ambao wameweza kutoa viinimacho na kuwafunua ili kuweza kuwa upande wa sauti ya waathirika. Baba Mtakatifu ameongeza kusema, hata kama ingekuwa  ni kesi moja ya manyanyaso, kwayo inawakilisha jambo baya sana na Kanisa haliwezi kunyamaza, bali ni  kupeleka mbele katika mwanga, kwa maana kashfa kubwa katika suala hili ni ile ya kufunika ukweli!

Wahalifu wanatambua kujificha, hadi ndugu, jirani aliye karibu

Katika ufafanuzi wake Baba Mtakatifu anasema; “Tukumbuke wote ya kwamba ni kwa njia ya neema ya Daudi kukutana na nabii Natan, aliweza kutambua ubaya mkubwa wa dhambi zake. Kwa maana hiyo kuna haja leo hii ya kuwa na Naatan wapya ambao waweze kusaidia Daudi wengi na kuwaamsha kutoka usingizi wa maisha ya kinafiki na ugeugeu. Baba Mtakatiti anaomba kusaidia Mama Mtakatifu Kanisa katika shughuli yake ngumu, iwe ya kutambua kesi za kweli na kuzibainisha na zile za uongofu, shutumu za uongo, hasira, masengenyo na kugushi. Ni kazi ngumu sana kwa maana ya wahalifu wanajua kujificha sana, hadi kuona wanawake wengi, mama wengi, dada wengi wanashindwa hata kuwagundua watu walio karibu nao: waume zao, baba zao, babu zao, wajomba, kaka, jirani, walimu… hata waathirika nao wanachagua kubaki kimya, hadi kufikia hatua ya kuwa na hofu, wanabaki na aibu nyingi hasa ile sababu ya kufikiriwa wataachwa peke yao.

Wahalifu, ongokeni, na jiandaeni katika hukumu ya Mungu

Kwa wale wanaowanyanyasa watoto wadogo, Baba Mtakatifu amewambia kwamba “ongokeni na jikabidhi katika vyombo vya haki ya kibinadamu na jiandae katika hukumu ya Mungu, kumbukeni maneno ya Kristo:“atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari. Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha!” (Mt 18,6-7).

Janga jingine la ukosefu wa uaminifu

Baba Mtakatifu katika hotuba yake aidha , amethibitisha ya kuwa kuna janga jingine linalohusu ukosefu wa uaminifu kwa wale ambao wanasaliti wito wao, kiapo chao, utume wao , kujiwekwa wakfu kwa Mungu na kwa Kanisa: wale ambao wanaficha nyuma nia nzuri ili kuwashutumu ndugu zao na kupanda magugu mabaya, migawanyo na mivutano; watu ambao daima hupata sababu ya kusema, hadi kufikia kutumia mantiki za kiroho, ili kuwezza kuendelea katika njia isiyopitika na ya kupoteza. Hii si jambo jipya la historia ya Kanisa Baba Mtakatifu Francisko amethibitisha. Mtakatifu Agostino, akitafakari juu ya ngano njema na magugu, anasema: Mnaamini labda ndugu zangu kuwa magugu mabaya hayawezi kupanda hadi kufika kiti cha uaskofuni? Je mnaamini kwamba ni katika madaraja ya chini tu na siyo ya juu? Mnataka mbingu tunayokwenda, pasipo magugu! (…)   Hata juu ya viti vya kiaskofu kuna ngano na kuna magugu: na kati ya jumuiya mbalimbali za waamini kuna ngano na kuna magugu” (taz Sermo 73, 4: PL 38, 472).

Maneno ya Mtakatifu Agostino, Baba Mtakatifu anasisitiza, yanataka kutukumbusha msemo mmoja: njia ya jehanamu, ni rahisi na kuwa na nia njema”, na anatusaidia kutambua kuwa mshawishi, yaani  Mshtaki Mkuu ni yule anayegawanya, anapanda machafuko, anazidisha uadui analaghai watoto na kupelekea dukuduku. Kwa hakika nyuma ya wapandaji wa magugu mabaya , daima kuna sarafu therathini. Na tazama ndipo sura ya Daudi inatupeleka katika sura ya Yuda Iskarioti, sura nyingine iliyochaguliwa na Bwana na ambayo inamuuza na kumkabidhi katoka kifo mwalimu wake.

Daudi mdhambi, na Yuda Iskarioti, watakuwepo daima katika Kanisa

Daudi mdhambi, na Yuda Iskarioti, watakuwepo daima katika Kanisa, kwa maana wanawakilisha udhaifu; ni sehemu ya maisha ya kibinadamu. Hizo ni picha za wadhambi kwa uhalifu waliotenda kutoka kwa watu waliochaguliwa na kutiwa wakfu. Wakiwa wameungnana na dhambi kubwa, lakini wanatofautiana katika uongofu, Baba Mtakatifu amesema. Daudi aliomba toba na kujikabidhi kwa huruma ya Mungu, wakati Yuda Iskarioti akajiua mwenyewe. Sisi sote kwa maana hiyo ili tuweze kung’aa mwanga wa Kristo, hatuna budi kupambana dhidi ya ufisadi wa kiroho, ambapo ni ajali kubwa ya kuanguka katika dhambi, kwa maana hiyo ni upofu wa mambo madogo madogo yenye mtindo na badaye unakupeleka pabaya, “si ajabu, maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru ( 2 Kor 11,14) . Kwa njia hiyo Soloni alimaliza siku zake, wakati mdambi mkuu Daudi alkatambua kujitakasa makosa yake (taz Esort. ap. Gaudete et exsultate, 165).

Baba Mtakatifu Francisko hata hivyo ametaja matukio muhimu yaliyfanywa mwaka huu

Mwaka huu mambo mengi yametukia, kwa mfano, kumalizika vema Sinodi ya Maaskofu kuhusu vijana. Hatua ambazo hadi sasa zimetimizwa za mageuzi ya Sekratarieti ya Vatican; kwa mfano kazi za kuweka bayana na uwazi wa uchumi; pongezi za juhudi zilizotendwa na ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa mahesabu na kutoka kwa Mamlaka ya habari ya Fedha: matokeo mazuri yaliyofukiwa na Taasisi za Matendo ya Kidini; Sheria Mpya ya Mji wa Vatican; Hati juu ya kazi Vatican, na mambo mengi yaliyokamilishwa ambayo hayaonekani kwa macho. Kadhalika Baba Mtakatifu amekumbusha kutangazwa kwa wenye heri wapya na watakatifu ambao ni mawe yenye thamani, yanayopamba sura ya Kanisa na kuangaza dunia matumaini, imani na nuru.

Mashuhuda wafiadini, vijana wanaochagua utawa na ukuhani

Ametoa mfano na kuwataja wafiadini 19 nchini Algeria. Akifafanua juu ya wafia dini, Baba Mtakatifu amesema hawa walitoa maisha yao kwa Krsito , kwa ajili ya Injili na kwa ajili ya watu wa Algeria(…) mifano ya utakatifu wa pamoja, utakatifu katika mlango wa jirani ( (THOMAS GEORGEON, “Nel segno della fraternità”, L’Osservatore romano, 8 dicembre 2018, p. 6); Aidha kuna idadi kubwa ya waamini kwa mwaka ambao wanapokea sakaramenti ya Ubatizo, na kupyaisha ujana wa Kanisa ambalo ni mama; idadi kuwa ya watoto wameingia katika nyumba na kukumbatia imani na maisha ya kikristo; familia na watoto wanaoishi kwa kina imani na kuonesha kila siku kwa watoto wao furaha ya upendo (cfr Esort. ap. postsin. Amoris laetitia, 259-290); Ushuhuda wa vijana wengi ambao wanachagua kwa ujasiri maisha ya kitawa na kikuhani.

Baba Mtakatifu anakumbuka maparoko wanaojikita kuwa na watu wao karibu

Ni sababu kubwa ya kuwa na faraha kwa idadi kuwa ya watawa kike na kiume, mapadre ambao wanaishi kila siku wito wao kwa uaminifu, ukimya, utakatifu na kujinyima. Ni watu wanaoangaza katika giza la kibinadamu, kwa njia ya ushuhuda wao wa imani upendo mkuu na kujitoa. Watu ambao wanafanyakazi kwa uvumilivu, kwa ajili ya upendo wa Kristo na Injili, kwa ajili ya maskini, walemewao na mizigo, waliobaguliwa bila kujiweka katika sura za kwanza za magazeti au kutafuta nafasi ya kwanza. Ni watu ambao wameacha yote na kutoa maisha yao ili kupeleka mwanga wa imani mahali ambapo Kristo ameachwa pemmbeni, ni mwenye kiu, njaa, mfungwa na aliye uchi ( mt 25, 31-46). Baba Mtakatifu ameongeza kusema kuwa,anawakumbuka maparoko ambao wanatoa mifano yao kila siku kwa watu wa Mungu, mapadra walio karibu na familia, wanatambua majina yao oate na kuishi nao kwa maisha rahisi, imani, utakatifu na upendo. Watu ambao wamesahaluliwa na vyombo vya habari na mahali ambapo bila mapadre, maisha yangetawalia na kiza nene.  

Thamani ya mwanga katika kubadili uwajibu wetu na kulinda hadi siku ya mwisho

Wakati wa kuzungumza  juu ya mwanga, mateso na juu ya Daudi na Yuda, amependelea kuweka bayana thamani za utambuzi ambao lazima ubadili namna ya kuwajibika na kulinda hasa kwa upande wa walio na madaraka katika majengo ya Kanisa, watawa  na wanajikita katika huduma ya serikali. Kwa dhati nguvu ya kila taasisi haipatikani na watu ambao ni wakamilifu, kwa maana ya kwamba haiwezekani. Lakini pamoja  hiyo inahitajika utashi wa kuendelea kujitakasa; katika uwezo wake wa kutambua kwa unyenyekevu makosa na kuyasahihisha; katika uwezo wa kuamka tena baada ya kuanguka; kutazama mwanga wa Noeli ambao unaanzia katika Holi la wanyama huko Bethlehem, kupitia mchakato wote wa historia, hadi kufikia siku ya mwisho wa kurudi kwake.

Ni lazima kujifungulia katika mwanga wa Yesu Kristo, mwanga wa wema unaoshinda ubaya

Ni lazima kufungualia mioyo katika mwanga wa kweli, Yesu Kristo. Mwanga ambao unaweza kuangaza maisha na kubadili giza letu katika nuru: mwanga wa wema unaoshinda ubaya: mwanga wa upendo unashinda chuki: mwanga wa maisha inaoshinda mauti: mwanga wa Mungu unaobadili yote katika mwanga na kwa wote: mwanga wa Mungu wetu ni maskini tajiri, huruma na haki, aliyepo na aliyejificha, ndogo na mkubwa. Tukumbuke maneno mazuri sana ya Mtakatifu Makario Mkuu , Baba wa jangwa la Misri katika Karne ya IV akitafakari juu ya Noeli anasema: “ Mungu alijifanya mdogo!  “Hakuna mtu mbinguni na duniani anayeweza kuelewa utukufu wa Mungu na hakuna mbinguni na duniani anaweza kuelewa jinsi gani Mungu anajifanya kuwa maskini na mdogo kwa ajili ya masikini na kwa wadogo. Jinsi gani ilivyo ngumu kuelewa ukuu wake na kama ilivyo hata udogo wake”. (taz mahubiri  IV, 9-10; XXXII, 7:Katika Roho na moto. Mahubri ya Kiroho mkusanyiko wa II, Qiqajon-Bose, Magnano 1995, p. 88-89; 332-333).

Tukumbuke kuwa Sikukuu ya Noeli ni ikukuu ya Mungu anayejifanya mdogo

Tukumbuke kuwa Sikukuu ya Noeli ni sikukuu ya Mungu ambaye anajifanya mdogo na katika udogo wake auishi kuwa mkubwa. Katika lugha hiyo ya udogo ndiyo ukubwa na upo upendo wa Mungu. Ni Neno ambalo ulimwengu unataka daima kutoa katika kamusi, yaani upendo Baba Mtakatifu amesema. “Mungu mkuu anayejifanya mdogo na ambaye ni mkubwa anaendelea kujifanya mdogo na mdogo ni mkubwa”(taz mahubiri, Kanisa la Mtakatifu Marta, 14 Desemba 2017;  na mahubiri katika Kanisa la Mt. Marta , 25 aprile 2013).

Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana kila mwaka inatupatia uhakika kuwa mwanga wa Mungu unaendelea kung’aa licha ya udhaifu wa kibinadamu; uhakika kuwa Kanisa litajikwamua kutoka katika moto huo kwa mara nyingine tena na kuwa zuri kwa maana litakuwa limetakasika na kung’aa. Kwa sababu dhambi zote kuanguka na ubaya ambayo umetendwa na watoto wa Kanisa, hautaweza kamwe kuweka kiza nene katika uzuri wa sura yake, na badala yake ni kutoa uhakika kuwa nguvu zake bado zipo ndani watu na  zaidi katika Kristo Yesu, mwokozi wa dunia na mwanga wa ulimwengu ambaye anapenda na alitoa maisha kwa ajili yake na mchumba wake. Sikukuu ya Noeli ni jaribio kwamba, mabaya yote  yaliyotendwa na baadhi, hayataweza kamwe kuweka kivuli cha kila wema uliotendwa na unaendelea bure katika Kanisa lote duniani.  

Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, inatoa uhakika kuwa nguvu za Kanisa na katika kazi yetu ya kila siku, mara nyingi iliyofichama, kama ile ya Sekretarieti Kuu, mahali ambamo wapo watakatifu yupo Roho Mtakatifu ambaye ameongoza na kulinda kwa karne nyingi, na kubadili kutoka katika  dhambi kuwa na fursa ya msamaha, kutoka katika kuanguka kuwa fursa ya kujipyaisha, kutoka katika ubaya kuwa fursa ya kutakasika na ushindi! Asanteni sana na Sikukuu Njema ya Kuzaliwa kwa Bwana kwa wote!

Baraka na mwisho zawadi

Baba Mtakatifu mara baada ya Baraka amewachia kitabu cha Kitaalimungu cha Tanquerey, lakini ambacho ni toleo la hivi karibuni kilicho haririwa na Askofu Libanori wa Jimbo la Roma na Padre Forlai, Baba wa Kiroho wa Seminari Kuu ya Roma. Na kwamba anaamini ni kizuri. Amewashauri wasisome kuanzia mwanzo hadi mwisho badala yake wachague baadhi ya vichwa vya kitabu hicho kwa njia hiyo kitawasaidia kila mmoja katika badiliko ya kila mmoja na mabadiliko Kanisa  ambayo ni kwa wao.

21 December 2018, 15:56