Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu na wanashirika la Mercedari mjini Vatican, wakati wanaadhimisha jubilei ya miaka 800 tangu kuanzishwa kwake na Mtakatifu Petro Nolasco wa Uhispania Baba Mtakatifu na wanashirika la Mercedari mjini Vatican, wakati wanaadhimisha jubilei ya miaka 800 tangu kuanzishwa kwake na Mtakatifu Petro Nolasco wa Uhispania 

Papa:Kuweni karibu na watu wanaopoteza imani na kubaguliwa!

Papa amekutana na mapadre wa Shirika la Mercedari Vatican, tarehe 6 Desemba 2018 katika fursa ya kuadhimisha miaka 800 tangu kuanzishwa kwakwe.Katika hotuba yake kwa lugha ya kispanyola amewashauri kuendekeza karama za mwanzilishi hasa ukaribu kwa wakristo katika hatari ya kupoteza imani, kubaguliwa,wafungwa, watoto yatima na wanao nyanyaswa

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 6 Desemba 2018, Baba Mtakatifu amekutana na mapadre wa Shirika la Mercedari mjini Vatican, wakiwa katika fursa ya  kuadhimisha miaka 800 tangu kuanzishwa kwa shirika lao (1218-2018). Katika hotuba yake kwa lugha ya kispanyola amewashauri waendelee na utume wao, hasa kuwa karibu na wakristo  ambao wako katika hatari ya kupoteza imani na kubaguliwa, wafungwa, watoto yatima na wanaonyanyaswa. Baba Mtakatifu akizungumza na Mapadre karibu 120 wa Shirika la Mercedari, shirika La Bikira Maria wa Mercede, amewaomba kwa dhati kuwa makini kabisa na wakristo ambao wako kwenye mitego na kuishia katika mamia ya mambo ya kidunia na hawajuhi kwa namna gani ya kuondokana nayo kwa maana ni mtindo wa utumwa.

Milango ya huruma ya Mungu waliobaguliwa

Akiendelea kutoa ushauri katika mstari wa utume wa Shirika hili lililoanzishwa kunako mwaka 1218 ulitokana na janga hasa watumwa wkristo : Pamoja na nadhiri ya umaskini , utii na usafi, wanaweka nadhiri ya nne ya wokovu, ambayo inawabidiSHA wawasaidiE watu waliofungwa ambao wako katika hatari za kukana imani. Baada ya kusitishwa utumwa kwa karne ya XIX, shirika hili limeeneza utume wake hasa kujikita kwa wafungwa na familia zao ili kuwasaidia wakristo wanaoteseka. Baba Mtakatifu anawaalika wapeleke wokovu wa Bwana kwa wafungwa, wakimbizi na wahamiaji ambao wanajikuta wemenaswa na mitego ya biashara ya binadamu  watu wazima waathirika, watoto yatima na wanaonyanyaswa. Wawasaidie wote na kuwapelekea ukarimu wa huruma ya Mungu wote walio baguliwa na jamii.

Leo hii kuna wafunga zaidi

Baba Mtakatifu akitazama juu ya nadhiri ya nne wanayoiweka anasisitiza kwambaa kumfuasa Kristo maana yake ni kutoa maisha ili kuokoa roho na kwamba wasipange maisha yao kama vile Yesu ndiye afuate  mipango ambayo wanafanya wao. Hata hivyo katika hilo Baba Mtakatifu ameongeza kusema ni  kwa jinsi gani watawa walivyo wajeuri. Hiyo haina maana ya mtindo tofauti, bali kwamba wamwache nafasi Bwana awaongoze katika njia anazojua yeye wakati wa kutoa huduma yao kwa watu. Ni lazima kuhamasisha hadhi ya binadamu  ili kuweze kusitisha utumwa wa kiroho au kumwili  unakwisha kwa walioathirika katika jamii yetu anasisitiza Baba Mtakatifu Francisko!  Kwa maana hiyo anasema Baba Mtakatifu kwamba familia ya wamercedari, watawa na walei wanapaswa kujiachia katika ubunifu wa Mungu na kufuata ushauri, hasa kwa kujikita katika karama ya shirika na kurudi katika asili yake ambayo ndiyo mwito wa Mungu!

06 December 2018, 14:52