Tafuta

Baba Mtakatifu amekutana na wajumbe wa Vikosi vya uokoaji kitaifa Italia Baba Mtakatifu amekutana na wajumbe wa Vikosi vya uokoaji kitaifa Italia 

Papa Francisko: Jitahidini kuzuia majanga, kukarabati na kulinda mazingira!

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kukutana na vikosi vya uokoaji nchini Italia, mjini Vatican tarehe 22 Desemba 2018, mawazo yake yamewaendea waathirika wa majanga ya asilia katika maeneo tofauti kwa mwaka huu na kuvipongeza vikosi hivyo kwa jitihada zake na ukarimu katika mfumo mzima wa mshikamano was huduma na raia

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika fursa hii nzuri, inayochangamsha na ukaribu wa Noeli Takatifu, wazo kuu na maombi ni kuwakumbuka kwa mwaka huu wale ambao wameathirika kutokana na  majanga ya asili na ambapo tunahisi shauku ya kuwakumbuka hata wale waokoaji ambao wamepoteza maisha wakati wanaokoa wengine. Ndiyo Maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo anza nayo wakati wa hotuba yake kwa wanavikosi vya uokoaji na ambavyo vinaunda kwa ujumla huduma ya uokoaji kitaifa. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican tarehe 22 Desemba 2018.

Kwa pamoja na waokoaji na watu waliokolewa

Walikuwa karibia watu 6,000 waliokutana na Baba Mtakatifu. Hawa wanawakilishwa na mashirika ya kujitolea, jumuiya za kisayansi, Vikosi vya Zima Moto, Vikosi vya Polisi na wanajeshi, kadhalika taasisi mbalimbali mahalia za Mikoa, wilaya na makampuni mbalimbali ya huduma. Kwa pamoja na waokoaji na watu waliokolewa na familia zao wameweza kufanya kumbukumbu ya kipindi kigumu, kilicho sababishwa na tetemeko la ardhi, maporomoko na mafuriko. Na kabla ya Baba Mtakatifu kuingia katika ukumbi huo, kwanza wamaeshirikishana kumbukumbu yao ya kuokolewa, lakini hata uchungu na hisia za shukrani. Kadhalika Shukrani  zimewandea watu wote, waume na wanawake wa vikosi mbalimbali vya kuokoa, zilizotolewa na Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Italia, Kardinali Gualtiero Bassetti ambaye pia ameshuhudia mwenyewe alipotembelea watu wa Norcia waliokumbwa na tetemeko la ardhi.

Muungano nyeti unaotengenezwa na mshikamano wa umma

Baba Mtakatifu katika hotuba yake, ameelezea kuwa kikosi cha kuokoa ni kiungo muhimu, ambacho kina mfumo wa mshikamano wa raia, kwa ajili ya ulinzi na usalama binafsi na kwa ujumla. Mfumo huo ni msingi katika maeneo, kama ilivyo kwa nchi ya Italia yenye mazingira mazuri  na mtazamo lakini  ambayo ni hatarishi. Na ili kuweza kukabiliana na hatari hizo, Baba Mtakatifu anabainisha kwamba ni lazima kuwa na umakini wa kila wakati wa kusimamia na kulinda mazingira.

Kikosi cha uokoaji nchini Italia hakikosi kamwe kukumbusha kuwa, kulinda maisha ya binadamu na maeneo yake, kuanzia majengo isiwe ni shuguli ya wakati wa dharura, bali iwe ni shughuli ya kila wakati na kwa kila mtu ili kuweza kuzuia au kurudia hatua nyuma na zinachukua muda mrefu wa kukarababti na wakati huo huo ni ngumu zaidi ya isivyotarajiwa.

Inahitajika mshakamano wa pamoja katika maeneo yote

Haitoshi shughulikia dharura, Baba Mtakatifu anabainisha kwa kujikita katika wosia wake wa Laudato Si: Inatakiwa mtazamo tofauti wa mawazo na siasa, mpango wa elimu, mtindo wa maisha hata ule wa kitasaufi, kwa ajili ya kutafuta si tu namna ya kusaidia kiufundi kwa  kila tatizo, bali hata katika kila hali ya mazingira yanayojiwakilisha. Hiyo ina maana ya kuchanganua mambo katika hali halisi bila kufikicha ukweli wake na unyeti wa matatizo ya mfumo huo wa dunia.

Umuhimu wa kuelimisha jamii na hasa watoto shuleni

Katika kusisitizia hilo, Baba Mtakatifu anasisitizia juu ya elimu kwa watu wote hasa kuwalenga zaidi vijana katika mashule na kama ilivyo umuhimu wa ukuu wa huduma ya Vikosi vya kuokoa na ambavyo vinachangia sana. Na kwa upande wa vijana wote Baba Mtakatifu ameeleza wajikite zaidi kupenda na kulinda mazingira, kukuza thamani ya kuishi kwa pamoja, ili kamna kwamba wanafanya  shughuli hiyo kila mmoja aweze kuishi katika dunia ya mshimakano na ya usalama.

Hata hivyo katika hilo, Baba Mtakatifu ametoa wito kwa taasisi za ngazi zote ili kufanya kazi pamoja kwa kuweka mipango ya dhati hasa katika matumizi ya maneo, kwa ajili ya shughuli za kidharura na kujibu dharua nyingi. Na mwisho amesisitiza misingi ya ushirikiano katika mashirika ya vikosi vya kuokoa na ambapo amesema wanaweza kushirikiana na sekta nyinga za maisha ya umma. Ukaribu wa hali halisi za kila siku ni rahisi zaidi, hasa kwa  kutazama mbele yetu na si matatizo peke yake lakini hata watu waweza kuwa na utambuzu wa utume kama huduma mwafaka ambayo inatoa faida ya jumuiya nzima.

Baadhi ya malekezo kuhusu mkutano huo

Kuhusiana na mkutano huu, ulikuwa hufanyika kunako mwaka 2916 mwaka maalum wa Jubilei ya huruma, lakini kwa bahati mbaya hakufanyika  kutokana na kuzuka kwa  tetemeko la Ardhi katika eneno la Kati ya Italia. Kutokana na fursa hiyo watu wa kujitolea zaidi ya 3,500 wamehudhuria, maofisa 350 wa Idara ya Ulinzi na Usalama, wawakilishi zaidi ya 1,500 wa Kamati ya Uendeshaji ya Ulinzi wa raia, ikiwa ni pamoja na Wazima Moto, polisi, Jeshi la Anga, Jeshi baharini na katika Mamlaka ya Maji. Wengine ni wawakilishi 350 wa Vikosi vya Polisi kati yao wa mapato, Polisi wa Upelelezi na Polisi ya Serikali na uwepo wa jumuiya ya kisayansi. Hatimaye, meya  takribani 140 wa manispaa zilizokumbwa na tetemeko la ardhi la mwaka 2016 katika nchi ya Italia ya Kati na la moja lililokumbwa huko  Ischia kwa  mwaka 2017.

22 December 2018, 16:17