Cerca

Vatican News
Yesu hakujibakiza na akaweza kukomboa maisha ya asili ya binadamu katika ujio wake, kwa maana hiyo watu wote wafungue mioyo yao katika usiku wa kuzaliwa kwa Bwana Yesu hakujibakiza na akaweza kukomboa maisha ya asili ya binadamu katika ujio wake, kwa maana hiyo watu wote wafungue mioyo yao katika usiku wa kuzaliwa kwa Bwana  (Vatican Media)

Papa:Jikabidhi kwa Mama Maria na Mtakatifu Yosefu

Katika salam zake Baba Mtakatifu kwa mahujaji na waamini toka pande zote za dunia, mara baada ya katekesi tarehe 19 Desemba 2018, amewaomba wajikabidhi kwa Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu ili waweze kufundishwa namna ya kukaribisha zawadi kuu ya namna hiyo yaani Emanueli, Mungu pamoja nasi

Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya katekesi yake, amewasalimia mahujaji wote kutoka sehemu mbalimbali za dunia, wakiwemo makundi mbalimbali ya maparokia, vijana na chama cha Kitaifa cha waathirika wa vita vya kiraia.

Vile vile mawazo yamemwendea kwa vijana, wazee, wagonjwa na wanandoa wapya. Baba Mtakatifu Francisko anasema: Katika sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana iliyo karibu, hata kwa mwaka huu, usiku huo uweze kuamsha nyoyo zetu wote upendo wa Mungu kwa binadamu, kwa maana Yesu hakujibakiza, na akaweza kukomboa maisha ya asili ya binadamu katika ujio wake. Baba Mtakatifu anaombea wote na ili kujikabidhi kwa Mama Maria na Mtakatifu Yosefu, ili waweze kutufundisha kwa namna ya kukaribisha zawadi kubwa ya namna hii, yaani Emanuel Mungu pamoja nasi.

19 December 2018, 13:34